Mamia ya madereva na watoto walikusanyika jijini Dar es Salaam Jumamosi iliyopita kwa ajili ya hafla ya Siku ya Familia ya Bolt, maarufu kama “Bolt Family Day”, iliyolenga kuzisherehekea familia za madereva wanaotoa huduma kupitia Bolt.

Hafla hiyo, inayofanyika kila mwaka, iliwakutanisha madereva, wake zao na watoto wao zaidi ya 130 katika michezo ya kifamilia, mechi za mpira wa miguu na mbio za mita 100. Iliwapa nafasi ya kufurahia muda pamoja nje ya shughuli zao za kila siku za kujipatia kipato.

Timu za madereva zilizoibuka washindi zilipokea vocha za kupata hadi lita 20 za mafuta kwa kila timu, pamoja na vocha za manunuzi na zawadi za maandalizi ya kurejea shuleni kwa watoto wao.

“Mwisho wa siku, familia ndiyo jambo muhimu zaidi,” alisema mmoja wa madereva, akieleza kuwa jukumu la kuhudumia wapendwa wao ndilo linalowasukuma kuendelea na kazi. Kwa mujibu wa kampuni hiyo, wengi kati ya madereva wake wanaofanya vizuri zaidi hupata kipato cha zaidi ya Sh milioni 3.5 kwa mwezi, kiwango kikubwa sana ikilinganishwa na wastani wa mishahara ya waajiriwa wa kampuni katika sekta rasmi.

Dereva mwingine, ambaye ni baba wa watoto watatu, alisimulia changamoto za kufanya kazi katika joto kali, kuharibika kwa magari na wakati mwingine kukutana na wateja wagumu kuwahudumia.

“Lakini hakuna biashara isiyo na changamoto, na kujua kwamba hatimaye familia zetu zinanufaika ndiko kunakotupa nguvu ya kuendelea,” alisema.

Meneja Mkuu Mwandamizi wa Bolt Afrika Mashariki, Dimmy Kanyankole, aliyehudhuria hafla hiyo, alisema: “Nyuma ya kila dereva kuna familia inayompa hamasa ya kufanya kazi kwa bidii kila siku. Tunatambua kuwa udereva si suala la kujipatia kipato pekee, bali pia kuhudumia wapendwa, kugharamia elimu ya watoto na kujenga maisha bora ya baadaye kwa familia zao.

“Kupitia shughuli kama Bolt Family Day, tunataka kuwathamini watu walio nyuma ya safari hizo na kuwapa madereva wetu nafasi ya kufurahia muda pamoja na familia zao. Pia, hii ni njia yetu ya kutambua na kuthamini mchango muhimu wa madereva katika kufanikisha usafiri katika miji yetu,” alisema Kanyankole.

Hafla hiyo iliangazia wajibu wa kifamilia unaoambatana na kazi ya udereva, huku familia zikishiriki michezo na kujishindia zawadi zilizolenga kusaidia gharama za usafiri na mahitaji ya shule ya watoto wao.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...