KARIBU cha Taifa cha Taifa cha Kuratibu Biashara ya Kaboni kimesaini Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano (MoU) na Benki ya CRDB Makubaliano ya Ushirikiano ya miaka mitano kwa lengo la kuendeleza, kufadhili na kukuza miradi ya biashara ya kaboni nchini.
Utiaji Saini huo umefanyika leo tarehe 13 Novemba 2026, jijini Antalya Uturuki, pembezoni mwa Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP31), katika kikao cha pembezoni cha Benki ya CRDB kilichokuwa na kaulimbiu ya "Dira 2050: Financing Tanzania's Resilient, Green and Inclusive Future.
Akizungumza baada ya kushuhudia utiaji Saini huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Mhandisi. Hamad Yussuf Masauni, ameipongeza NCMC na Benki ya CRDB kwa kuanzisha ushirikiano unaolenga kukuza soko la biashara ya kaboni na kuongeza fursa za uwekezaji katika uchumi wa Kijani.
Mhe. Masauni ameipongeza Benki ya CRDB kwa kuunga mkono juhudi za serikali katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambapo amesisitiza makubaliano hayo yanaimarisha ushirikiano wa serikali na sekta binafsi katika kuimarisha soko la biashara ya kaboni nchini.
Akiongea awali, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dkt. Richard Muyungi amefafanua kuwa ushirikiano huo utawezesha utekelezaji wa Dira ya 20250 ambapo sekta ya biashara ya kaboni inaweza kuwa miongoni mwa nyenzo za kuvutia uwekezaji na kuchochea shughuli za uzalishaji.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa NCMC, Bi. Ngenda Kathryn Kigaraba, amesema hatua ya ushirikiano huo katika maendeleo ya soko la Biashara ya kaboni nchini utawezesha miradi ya kaboni kupata mitaji kutoka ndani ya nchi.
Naye Afsa Mtendaji Mkuu wa Benki ya CRDB Dkt. Abdulmajid Mussa Nsekela ameeleza kuwa ushirikiano huo utafungua fursa za uwekezaji, kuvutia mitaji na kuwezesha miradi ya kaboni yenye manufaaa kwa uchumi na jamii.




.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...