Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesisitiza umuhimu wa kulinda amani, umoja na mshikamano wa Taifa, akieleza kuwa ni msingi wa maendeleo endelevu, uwekezaji, biashara na utalii.

Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo tarehe 11 Novemba 2026, wakati wa Hafla ya Usiku wa QURAAN iliyoandaliwa na Jumuiya ya Bohra Tanzania, katika Msikiti wa Hakimi, Upanga, Dar es Salaam.

Amehimiza viongozi wa dini kuendelea kujenga maadili, uvumilivu na maridhiano katika jamii, huku vijana wakihamasishwa kuzingatia elimu, kujenga ujuzi na kutumia fursa za ujasiriamali kwa maendeleo ya Taifa.

Aidha, amewataka wananchi kudumisha amani na utulivu ili kuwezesha Serikali kuendeleza juhudi za kuboresha miundombinu na huduma za kijamii na kiuchumi.

Vilevile, Rais Dkt. Mwinyi ameshiriki chakula cha pamoja cha Jumuiya (Community Kitchen) na waumini na wageni waliohudhuria hafla hiyo.

Hafla hiyo imehudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Mahmoud Thabit Kombo; Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar, Mhe. Juma Malik Akil; Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe. Nassor Ahmed Mazrui; Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dkt. Abubakar Zubeir Bin Ally; Sheikh Zoebbhai Galiakotwalla, mwakilishi wa Jumuiya ya Bohra Dar es Salaam; na Qussay Bhai Saheb Jamaludin, mwakilishi wa Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Dawoodi Bohra Duniani, Sheikh Syedna Mufaddal Saifuddin, pamoja na wageni waalikwa kutoka sehemu mbalimbali duniani.


















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...