Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa James Kinyasi Millya (Mb.), amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Finland nchini, Mheshimiwa Anna Marrifield, pamoja na ujumbe wa CMI – Martti Ahtisaari Peace Foundation ulioongozwa na Bi. Tiina Kukkamaa-Bah. Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara, tarehe 18 Novemba, 2026 jijini Dar es Salaam.

Mheshimiwa Millya amesisitiza umuhimu wa kuandaa Mpango Kazi wa mwaka 2027 wa kutekeleza Hati ya Makubaliano kati ya Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt. Salim Ahmed Salim na CMI. Mpango huo utajikita katika mafunzo ya upatanishi kwa wanadiplomasia vijana na kuimarisha diplomasia ya kuzuia migogoro katika Ukanda wa Maziwa Makuu.

Balozi Marrifield ameishukuru Tanzania kwa kuendeleza ushirikiano na Finland katika biashara, uwekezaji na maendeleo. Pia ameeleza utayari wa Finland kuimarisha ushirikiano na Tanzania katika majukwaa ya kimataifa, yakiwemo yale ya Umoja wa Mataifa, kuhusu masuala yenye maslahi ya pamoja. Vilevile, ameeleza pia utayari wa CMI kushirikiana na Tanzania katika upatanishi na kuzuia migogoro kupitia majukwaa mbali mbali ya mazungumzo.










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...