Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji. Rose Ambrose akizungumza wakati wa mkutano ulioandaliwa na Tume ya Tume ya Bonde la Ziwa Victoria (LVBC) inayosimamiwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki na kufanyika katika Banda la Tanzania Novemba 13, 2026 pembezoni mwa Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa wa Mkatab awa Mabadiliko ya tabianchi unaoendelea katika Mji wa Antalya, Uturuki.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jackson Kiswaga akifuatilia mkutano ulioandaliwa na Tume ya Tume ya Bonde la Ziwa Victoria (LVBC) inayosimamiwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki na kufanyika katika Banda la Tanzania Novemba 13, 2026 pembezoni mwa Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa wa Mkatab awa Mabadiliko ya tabianchi unaoendelea katika Mji wa Antalya, Uturuki.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Prof. Pius Yanda (kushoto) akifuatilia mkutano ulioandaliwa na Tume ya Tume ya Bonde la Ziwa Victoria (LVBC) inayosimamiwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki na kufanyika katika Banda la Tanzania Novemba 13, 2026 pembezoni mwa Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa wa Mkatab awa Mabadiliko ya tabianchi unaoendelea katika Mji wa Antalya, Uturuki.
Makamu Mwenyekiti wa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maji na Mazingira ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Prof. Pius Yanda (kushoto) akimsikiliza Naibu Katibu Mtendaji wa Tume ya Bonde la Ziwa, Mhandisi Coletha Ruhamya (katikati) wakati wa mkutano ulioandaliwa na Tume hiyo inayosimamiwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki na kufanyika katika Banda la Tanzania Novemba 13, 2026 pembezoni mwa Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa wa Mkataba wa Mabadiliko ya tabianchi unaoendelea katika Mji wa Antalya, Uturuki.
Baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakifuatilia mkutano ulioandaliwa na Tume ya Tume ya Bonde la Ziwa Victoria (LVBC) inayosimamiwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki na kufanyika katika Banda la Tanzania Novemba 13, 2026 pembezoni mwa Mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Mataifa wa Mkataba wa Mabadiliko ya tabianchi unaoendelea katika Mji wa Antalya, Uturuki.

TANZANIA imewasisitiza umuhimu wa mifuko ya fedha ya mabadiliko ya tabianchi kuwezesha upatikanaji wa shilingi bilioni 317 ili kutekeleza wa mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Rose Ambrose amesema hayo Novemba 13, 2026 wakati wa mkutano uliondaliwa na Tume ya Bonde la Ziwa Victoria (LVBC) inayosimamiwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki pembezoni mwa mkutano wa 31 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi.

Ameeleza umuhimu wa mifuko hiyo kutimiza ahadi ilizotoa kwa Tanzania kuhusu utekelezaji wa mradi huo uliopo katika awamu mbalimbali za utekelezaji na kutolea mfano mradi wa maji wa Simiyu, Mara na Kagera.

Ameitaja miradi mingine kuwa ni utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi wa kituo cha kusafisha maji Butimba kilichopo Mkoani Mwanza ambacho kinahudumia takribani watu 450,000 na kueleza kuwa miradi hiyo ina umuhimu mkubwa kwa maendeleo ya watu na rasilimali zilizopo.

Amesema Tanzania inatambua ulinzi wa rasilimali za Ziwa Victoria ni nguzo muhimu katika kufanikisha ajenda ya usalama wa maji kuwa msingi wa taifa kama ilivyoanishwa katika Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050.

Amefafanua kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na Nchi Wanachama wa Kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria ili kuimarisha usimamizi wa rasilimali zilizopo katika ziwa hilo ambalo linahudumia takribani wananchi milioni 45.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Andrea Malueth amesisitiza umuhimu wa ushirikiano katika mashirika ya fedha ya kimataifa kuongeza uwekezaji na ufadhili wa miradi ya maendeleo katika nchi zilizopo katika ukanda huo.

Amesema jumuiya hiyo itahakikisha mpango mkakati wa LVBC ili kuimarisha urejeshaji wa mifumo ikolojia, miundombinu inayostahimili mabadiliko ya tabianchi, mnyororo wa thamani wenye ushindani na kuimarisha mfumo wa kitaasisi.

“Mkakati umeweka wazi mahitaji ya dola bilioni 8, hivyo hii inatoa fursa ya kuainisha vipaumbele vya kitaifa na matarajio ya maendeleo ya kikanda na kuhamasisha usimamizi wa rasilimali kuelekea matokeo na maendeleo ya pamoja baina ya Nchi Wanachama” amesema Dkt.Malueth.

Jamhuri ya Muungano ya Tanzania inatumia fursa ya mkutano wa COP 31 kuimarisha diplomasia ya kimataifa ya mabadiliko ya tabianchi, kutafuta fursa za fedha, utafiti, teknolojia na kujenga uwezo kwa wataalamu.

Kaulimbiu ya Tanzania katika mkutano huo inasema Hatua jumuishi za Tanzania za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa ajili ya dira 2050: Kujenga Taifa Imara la Kijani na lenye ustawi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...