MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Mbeya imewataka wakazi wa Kasumulu na maeneo jirani kuzingatia sheria na taratibu za forodha katika shughuli zao za biashara ili kudhibiti magendo, kuzuia ukwepaji wa kodi na kulinda mapato ya Serikali.
Akizungumza wakati wa zoezi la elimu kwa wananchi, Meneja Msaidizi wa TRA Mkoa wa Mbeya, Mohamed Tukwa, amesema biashara za magendo zinaathiri ukusanyaji wa mapato ya Serikali na kusababisha ushindani usio wa haki kwa wafanyabiashara wanaozingatia sheria na amewasihi wananchi kushirikiana na maafisa wa forodha katika kupambana na vitendo hivyo.
Aidha, Tukwa amewataka wananchi walioingiza vyombo vya moto nchini bila kufuata taratibu za forodha kutumia fursa ya utaratibu maalumu wa miezi mitatu ulioanza Oktoba Mosi, 2026, unaowawezesha kukamilisha taratibu husika bila kutozwa adhabu.
Vilevile amesisitiza umuhimu wa wananchi, hususan wa maeneo ya mipakani, kutumia elimu inayotolewa na TRA, kufuata taratibu za uingizaji wa bidhaa nchini na kutoa taarifa za vitendo vya magendo kwa mamlaka husika ili kuimarisha biashara halali, kulinda mapato ya Serikali na kuchochea maendeleo ya taifa.


.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...