Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Zainab Khamis Shomari, ameahidi kutumia nafasi yake ya uongozi kutetea na kuwawezesha wanawake kiuchumi ili waweze kujikwamua kupitia shughuli binafsi na vikundi vya ujasiriamali.

Ametoa ahadi hiyo Novemba 19, 2026, wakati akizungumza na wajasiriamali pamoja na wanachama wa CCM na UWT katika Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Zainab amesema lengo la Serikali na CCM ni kuhakikisha kila mwanamke anakuwa na shughuli ya kumuingizia kipato, akisisitiza kuwa uwezeshaji wa kiuchumi haupaswi kuzingatia itikadi za kisiasa.

Aidha, amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, kwa kuanzisha Mfuko wa Mwinyi Boost Fund unaolenga kuwawezesha wanawake kiuchumi, akieleza kuwa mfuko huo umekuwa msaada mkubwa kwa wanawake wengi visiwani Pemba.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...