Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein na mkewe Mama Mwanamwema Shein, wakiangalia mitego ya nyuki katika kituo cha msitu wa Muganza Wilayani Kibondo wakati alipotembelea kituo hicho kwa lengo la kuona maendeleo ya mradi huo leo.
Makamu wa Rais Dk Ali Mohamed Shein akisalimiana na mtoto Elius Chegecha ( 10) anaesoma darasa la kwanza katika Shule ya msingi Kakonko Wilayani Kibondo wakati alipofika katika kijiji hicho kwa ajili ya kuangalia hifadhi ya maendeleo ya mradi wa msitu wa asili wa Muganza Wilayani Kibondo leo.
Mke wa Makamu wa Rais Mama Mwanamwema Shein akicheza ngoma na wasanii wa kijiji cha Kakonko katika uwanja wa ukumbi wa vijana Wilayani Kibondo alipowasili kwa ajili ya mkutano wa Hadhara leo. Mmoja wa wazee wa kijiji cha chokabongo Wilayani Kibongo Mkoani Kigoma Bibi Hamisa Mrisho akimkabizi zawadi ya Mahotpot Mke wa Makamu wa Rais Mama Mwanamwema Shein alipotembelea katika kijiji hichi kuangalia miradi ya maendeleo leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Kaka michu naona hapo mke wa Mh Makamu wa rais anapewa Nyungo sio Mahot pot. Ama kibongo bongo inakuweje hapo?
    Mdau Ughaibuni

    ReplyDelete
  2. Jamani picha ya tatu Mrs Shein viatu vyake mbona sivielewi

    ReplyDelete
  3. michu huyu baba kwli ni mwana chukua chako mapema, kwani hawa watu kambarage ndo alikuwa anawatafuta mtizawe mke wake jamani mh baba wa watu hana makubwa

    ReplyDelete
  4. Anon. wa pili inabdidi uelewe tu kuwa huyo ni bi mkubwa wetu, sasa hivi stileto hazimfai tena,

    Pia ni utamaduni wa wazanzibar walioupokea enzi za usultan, wa kuvaa mitarawanda na makubadhi hivyo si shani kwao viatu vya mchuchumio au dumbukiza kila wakati, na ukichunguza kwa makini wengi wa wakaazi wa huko hata ikiwa kiatu kina kisigino bado kitakuwa cha kuchomeka, na hiyo ni kwa kurahisisha kwa matembezi na urahisi wa kuvua kwa haraka anapotaka kuingia ndani ya nyumba yake au nyumba ya ibada upo hapoooo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...