Mzee Kingunge Ngombale Mwiru akiapa mbele ya Rais Kikwete kuwa Waziri ktk Ofisi ya Rais. Yeye hakutumia Msahafu wala Biblia kama wenzie wote....alipiga kavukavu tu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Bwana Michuzi,

    Mbona unataka kunivunja mbavu? Unasema Mzee Ngombale alipiga kavukavu?

    Wacha maneno yako bwana.

    Tunashukuru sana kwa picha. Tafadhali usichoke Bw. Michuzi.

    ReplyDelete
  2. Lakini cha kufurahisha ni baada ya hapo kumaliza kuapa kavukavu akasema "EWE MWENYEZI MUNGU NISAIDIE"

    ReplyDelete
  3. swafi kwa kumleta mzee kingunge. huyo ajue amewekwa hapo kutokana na kuheshimiwa nafasi yake katika jamii. yeye atashughulikia siasa na mahusiano ya vyama. nina imani kabisa japo alishindwa kumkiri mungu, ataweza kuwa baba wa wote na sio wa CCM. nina imani hatakuwa akitetea mambo ya chama chake kwenye utendaji wake. nia ya mzee huyu kama ni hiyo ni vyema ili afute ile kauli POTOFU NA YA AIBU YA MWALIMU KUWA MAPINZANI NI MBWA....au RAISI BORA NI WA CCM TU!! iliyowafanya hadi leo wanademokrasia na manaupinzani waonekane WAHAINI, WASALITI, WAVUNJA AMANI NA UTULIVU, NA WASIOPENDA MAENDELEO. kwa kuwa dawa ya moto ni moto, basi, kama nyerere alikuwa ni mzee hata huyu ni mzee, anaweza kuuzima moto ule ulioua demokrasia...

    tnategemea pia waandishi watajirekebisha. sielewi kwanini waandishi bado wana ushenzi wa kudhalilisha wenzao kwa namna hii mfano huyu mwandishi aliyesema seif ameangukia pua miezi mitatu imeeishapita baada ya uchaguzi.

    http://www.ippmedia.com/ipp/nipashe/2006/01/06/57289.html

    je mnafahamu kuwa pamoja na kurig uchaguzi zanzibar, na waandishi kuficha kiini cha matatizo ya zanzibar, seif bado ana asilimia 46 % ? je huko ndio kuangukia pua au ni chuki zenu binafsi? mimi sio CUF lakini sioni kama mnatenda haki kwa jamii ya tanzania. mzee kingunge pamoja na mengi ya kuyafanya ni kuwabana ninyi waandishi wa habari wa tanzania.

    cheers

    ReplyDelete
  4. Mimi binafsi sikupenda Kingunge arudi ulingoni kwani anastahili kuwaachia nafasi vijana wa "ARI MPYA NGUVU MPYA NA KASI MPYA" sidhani kama mheshimiwa atakuwa na nguvu mpya nadhani Mh. Kikwete kazi anayo maana siku anaapisha baraza lake alisema waziri mvivu hatamaliza miaka 5. Ila mheshimiwa alitoa kali kwa staili yake ya kuapa.

    ReplyDelete
  5. Hapo ndo JK kachemsha,mzee Kingunge
    amechoka sana hizi siasa za kufadhiliana zife kama tunataka nchi yet iendelee tuache kupeana vyeo kwa upendeleo,Kingunge age yake yote imepanguliwa yeye anataka afie madarakani.Serikali imempa miradi ya ubungo bus stand.
    kwenu vijana ambao bado ni wadogo hamkuwepo enzi za sabini Kingunge aliwahi kufukuzwa CCM,na hata akanyang'anywa kadi,hilo mnalijua vijana mwulizeni mambo ya Tanga(alipoku mkuu wa mkoa).Vijana tafuteni kuwajua hawa wazee msiwaone hivyo wengine ni chui ndani ya ngozi ya kondoo,ndiyo maana nchi yetu iko hivyo.Michuzi wasaidieni vijana wajue ya kale (old is gold).Kama mtaelewa historia ya hao mnao waona ni viongozi wetujeni up and down zao.

    ReplyDelete
  6. ANONYMOUS WA JANUARY 31 2006 NAKUUNGA MKONA KABISA VIJANA LAZIMA WAFAHAMU WATU HAWA WANACHUKUA UONGOZI KATIKA SERIKALI YETU NI CHUI WENYE NGOZI YA KONDOO MFANO MZURI MWINGINEWE PIA NI WAA BRO DITO EEH WAMELEWA MADARAKA. HAYA WEE

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...