Lori likiwa limebeba ngozi kupeleka bandarini tayari kusafirishwa nje ya nchi. Ukosefu wa viwanda vya kutosha kusindikia ngozi kunalazimisha bongo kupeleka nje mali ghafi hiyo na kununua inaporudi kama viatu au mikoba. wenzangu huko ughaibuni mnakubali hali hii iendelee wakati bongo ni ya pili Afrika kwa kuwa na ngo'mbe wengi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Michuzi tokea mwaka huu uanze umeshikia bango sana hii hoja yako ya kurejea Bongo. Leo nimeota suala fulani hivi na kufikia muafaka. Nitaandika kwenye Baragumu langu hivi karibuni. Kamtazamo kangu kanaanza kubadilika kidogokidogo, sio sana kuhusu hoja hii.

    Inshallah panapo mwisho wa mwaka huu tutakutunukia nishani ya uzalendo kwa kuanzisha vivutio vya aina ya pili. Kazi kubwa ya Serikali za Bongo, hasa hii iliyopita ya Prez Willy ilikuwa kuvutia wawekezaji wa kigeni kuja kuwekeza Bongo. lakini wewe umekuja na kasi yako, ari yako na nguvu zako kutangaza vivutio kwa wakezaji wa Kibongo (ambao kwa harakaharaka hawana mpango wa kurejea hivi karibuni) kuja kuwekeza Bongo.

    ReplyDelete
  2. Kama sikosei Rostham Aziz na Juma Ngasongwa waliwahi kuwa mameneja wa Kiwanda cha Ngozi! Kama nimepata au nimekosa naomba mniambie.

    F MtiMkubwa Tungaraza.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...