hii si 'abstarct, bali ni kivuli ama kupiga picha kuelekea utokako mwanga (against the light) na kuzaa kitu kama hiki. hapa ni hamburg, ujerumani, kwenye kiwanda cha ndege cha airbus nilikotembela mwishoni mwa 2005

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Michuzi leo umenipa jibu ambalo hunisumbuga mara nyingi, kumbe picha za namna hii hupigwa kwa kuelekeza kamera utokako!!. Fungua kiungo hiki uone picha ambazo huwa sizielewi upigwaji wake.

    http://www.beczak.org/Sunrise%20&%20Sunset%20058.jpg

    **Swali: Je picha hizo za jua nazo hupigwa kwa namna hii uliyotueleza hapo chini?

    Mwalimu Michuzi naomba darasa.

    ReplyDelete
  2. hiyo picha ya jua litualo haina tofauti sana na hiyo yangu, ila sema imepigwa jioni sana ambapo mwanga wa jua ni hafifu na pia una rangi ya dhahabu. ili kupata picha namna hii yakubidi uwe pia na chujio (filter) ya mwanga-wa-anga (skylight) inayosaidia kuondoa ukungu ule wa buluu uonekanao kama wapiga picha uwanda wa nchi (landscape). nadhani tupo pamoja. lete tu swali lolote kuhusu picha za dijito ama asilia, ntajitahidi kujibu. nikishindwa ntakuomba tudese mahali

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...