mama anna mkapa akiwa na laura bush dar katikati ya mwaka jana ndo picha yangu binafsi bora kwani ni mie pekee nilieipata kwa kukisia kabla wangetokea kwenye kamlango na iliwachukua hatua takriban nane kuketi, hiyo ikiwa ni ya tano hivi. kikubwa walishikana mikono kwa sekunde kama tatu tu. wengine wote, hata wa kutoka marekani, walikosa hii ya kushikana. ndo maana ilipotoka ubalozi wakaja kuniomba

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Michuzi, aliyeanzisha mambo ya kublogu duniani alifanya jambo la maana sana. Lini tungefaidika na picha hizi ambazo wewe tu unazo?

    ReplyDelete
  2. Nashukuru sana kwa shukrani zako. Tangu nimeanzisha hii kitu sijamuona mtu yeyote akinishukuru, wewe ndio wa kwanza kufanya hivyo.

    ReplyDelete
  3. Ah Mija Shija sikujua kuwa Michuzi mwepesi hivyo . Hebu tusimulie zaidi.

    ReplyDelete
  4. Michuzi kwa picha za akina mama hana mpinzani kwa kweli!!!!!!!

    ReplyDelete
  5. Hivi ndugu yangu Michuzi huyu mama alila wapi sasa? Au pale kwenye ubalozi wao? Unakuta hata vile vitu vyetu vya pale mchikichini,Ilala unakuta alikataa kunywa (siunajua hawakawii kusema hazina viwango)...Isaac Mgwassa

    ReplyDelete
  6. anony. huyu mama kimaandishi alilala nyumbani kwa balozi, lakini magirini. mojawapo ya vituko ni kuja na gari lake, hapana, magari yake mwenyewe, na kila alipofika kufanya kitu mawasiliano yote (si simu za mkono wala rediokoo za polisi) yalikwamishwa. na ni waandishi wachache waliopewa nafasi kusogea karibu namna hiyo.

    ReplyDelete
  7. hapo naona mzee mwenyewe Bush alikuwa anapiga story na bwana Ben offisini sio!hivi first lady wetu mpya anajua kighaibu? tutafutie Cv yake kidogo maana huyu aliyepita twaijua. jj!

    ReplyDelete
  8. Jamjua polepole baba. Hujui Michuzi anaonwa na nani au anafanya 'kazi' gani.

    ReplyDelete
  9. cha kusikitisha ni kuona hata waandishi wa bongo hawawezi kuipa changamoto serikali na viongozi wao kuanzia pale juu kama tunavyoona wenzao wa ughaibuni wanvyofanya na hii sio chuki binafsi bali ni kwa faida ya umma. wakuu wanatakiwa wapate constanti presha mpaka wanapo maliza kazi, hakuna kulala. tusijidanganye bongo bado sanaaaa bado hakuna itu pale, mbona wenzetu kenya wameanza kuelewa somo! wanapeana moto! na kweli inakuwa kiti moto" "kura tutakupa lakini cha moto utakiona"jamjuah-jj

    ReplyDelete
  10. Huyu mama alikuja zanzibar lakini nachoweza kusema ni kero tu iliyowapata watu kwa siku ile.Njia ya kutoka uwanja wa ndege ilifungwa,wafanyakazi wa airpoert wakalazimishwa kuvua mavazi yao ya kawaida(siku hiyo buibui ilikua nooo).Hata mkuu wa mkuu na waziri flani walikatazwa kuingia uwanja wa ndege!!!!!!!!!!

    Sijui kama viongozi wetu wanapewa heshima kama hizi huko ughaibuni wakati wa ziara zao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...