nampenda rais tarja wa finland. niligongana nae mitaani hivi... ila nilimstukia jamaa aliyevaa jaketi jekundu ni jamaa-flani, au vipi mtimkubwa. huyu bibie anasahau yalomkuta palme wa sweden?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Mbona huweki wazi kitu ulichompendea hasa ni nkipi mpaka uamue kumuita Raisi wako kama vile hii Tanzania yetu haikuhusu!!!!

    ReplyDelete
  2. Yaliyomkuta Olof Palme na Anna Lind ni mattukio adimu sana katika nchi za Nordic.

    Rais Tarja Halonen unaweza kukutana naye kwenye foleni ya kulipia bili, ndani ya basi, disko, au mahala pengine popote. Chizi mmoja siku kadhaa zilizopita alimpiga picha na kuituma magazetini alipomnyaka akicheza mashine ya kamali kwenye duka moja.

    Halafu moja ya hobby zake ni kucheza ngoma za Kiafrika. Huwa anahudhuria darasa la ngoma za Kiafrika kila Jumanne na Jumatano jioni.

    Mifano ya viongozi wa nchi za Nordic ndiyo ya viongozi wa watu waliotoka kwa watu ambao bado wapo na watu. Ikitokea ukawastukiza kuwauliza bei ya kilo ya mchele au nauli ya dala dala baadhi ya mawaziri wetu wa Tanzania, hautashangaa kwamba watakuwa hawajui.

    F MtiMkubwa Tungaraza.

    ReplyDelete
  3. fikrathabiti, swali lako kanijibia mtimkubwa. asante kwa kuuliza

    ReplyDelete
  4. viongozi wetu wanapesa kuliko viongozi wa nchi nyingi tu za ulaya!wakati nchi imechoka mbaya. je wanapata wapi? angalia masuti waliovaa kila malecela hapo juu linganisha na koti la mama terja.

    ReplyDelete
  5. maana yake ni raisi wa watu! chukulia kwa mfano unguja vigogo wa serekali wanajiongezea ulinzi! chanzo ni nini? na raia watafanyaje? wachilia mbali tena feza zinazowazunguka kati kati ya masikini! ila Jk akiendelea anavyoendelea anaweza kuwa raisi wa pili wa Afrika kukatiza mitaani na kisimtokee kitu! nadhani wa kwanza alikuwa Thomas Sankara ambaye si tu alikuwa anakatiza bali pia na kabito kake spana mkononi!

    michuzi! hii picha ni bomba sana! ni makala nziiito sana!

    ReplyDelete
  6. kikwete ni tapeli mwingine tu, ila anapewa sifa nyingi kwa sababu ya tabasamu yake nzuri,hakuna cha ajabu hata kimoya alichofanya hapo, zaidi ya sifa nyingi tu ambazo hakuna msingi wake. kila rahisi angefanya alichofanya hata wengine zaidi. je ni kipi kipya alochofanya? mawaziri wake ni walewale, wapo zaidi ya miaka 15 ofisini.rushwa palepale
    "ukiwamaliza wafisadi wote hapo nchini kamwe utakaa utembee mtaani kama mama tarja ila ukila nao sahani moja utatembea mtaani bila shaka" jj-jamjuah

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...