prof. mark mwandosya akipeana mkono na makongoro nyerere siku uwanja wa ndege wa dar ulipobatizwa upya

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 03, 2006

    I.M said...
    Michuzi samahani kwa kuandika hii habari hapa,kuna habari nimeisoma kwenye nipashe la leo asubuhi kwenye mdaharishi wao.I nasema kwocha msaidizi wa chelsea amekuja nchini kuja kuongea na Jamaa wa TFF...Kwenye timu ya chelsea hakuna mtu kama huyo ambaye anajiita Jeff Bookman. Hawa jamaa watakuwa matapeli na wanakuja nchini kwetu kutapeli naomba uwezu kuliwasilisha hili jambo kwa mwandishi aliyeandika habari Majuto Omary. Na kwa ushaidi mzuri jina lake hata kwenye website ya chelsea halipo na mimi pia nimfanyakazi katika hotel moja ambayo wachezaji na viongozi mara nyingi wanafikia hapa chelsea sijawahi kumsikia huyu mtu na wala hayupo chelsea...Naomba uweze kumfahamisha huyu mwandishi wa hii habari kama utakuwa unamjua

    Kocha wa Chelsea kuteta na Stars leo

    2006-05-03 09:03:35
    By Majuto Omary


    Kocha msaidizi wa mabingwa wa soka wa England, Chelsea, Jeff Bookman aliwasili nchini juzi na leo atazungumza na uongozi wa Shirikisho la Kandanda la Tanzania, TFF, na wachezaji wa timu ya taifa, Taifa Stars.

    Bookman amewasili nchini akiongozana na kocha wa timu ya watoto ya Tottenham Hotspurs, Ose Aibangee kwa mwaliko wa kampuni yenye lengo la kusaka wachezaji wenye vipaji hapa nchini, Global Scouting Bureau (T) Limited, GSB.

    Makamu wa Rais wa GSB, Jack Pemba alisema jana kuwa makocha hao watawasilisha programu ya miaka mitano iliyoandaliwa na kampuni yao kwa TFF yenye lengo la kuiwezesha Tanzania kushiriki katika mashindano ya Mataifa ya Afrika ya mwaka 2008 na vile vile Kombe la Dunia.

    Pemba alisema kuwa mbali ya programu hiyo, makocha hao watazungumza na wachezaji wa timu ya taifa jinsi ya kuwa na wachezaji wa kulipwa na mambo mengine mengi ya kiuchezaji.

    Alisema kuwa pia watazungumza na TFF kuhusu jinsi ya uanzishwaji wa mipango endelevu ya timu za watoto, elimu kwa makocha na mambo mengine mengi muhimu kwa maendeleo ya soka la Tanzania katika mkutano huo uliopangwa kuanza saa 6:00 mchana.

    Msemaji wa TFF, Florian Kaijage amethibitisha hayo.

    Alifafanua kuwa makocha hao wana uhusiano mzuri na kampuni yao na ndiyo maana Bookman ameamua kuachana na sherehe za ubingwa wa timu yake na kuja nchini kutoa mada za maendeleo ya soka.

    Kwa mujibu wa Pemba, GBS itaendesha mpango wa kusaka wachezaji chipukizi na kuwatafutia masoko nje ya nchi, mbali ya kuunganishia wachezaji watakaokuwa na mpango wa kwenda kucheza soka la kulipwa.

    Alisema kuwa Tanzania ina wachezaji wengi wenye vipaji, lakini hawajijui na kujikuta wanaishia kucheza hapa hapa nchini.

    ’Lengo langu ni kuendeleza soka la hapa nchini, na kazi ambayo nimeifanya kwa muda nchini Marekani na Uingereza na wachezaji kibao wamefanikiwa,’ alisema Pemba.

    Kampuni hiyo inatarajia kukusanya jumla ya wachezaji 440 ambao watatafutiwa masoko nje ya nchi katika mpango wake maalum ambao utakwenda sambamba na kuwaendeleza kielimu.


    SOURCE: Nipashe

    2:35 AM

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 03, 2006

    Michuzi,
    Tafadhali deili noizi hebu fanyieni kazi habari hiyo tupate ukweli, maana hawa nipashe wamekuwa wavivu kupita kiasi. Nakubaliana na mtu mmoja aliyewahi kusema TZ kuna reporters siyo journalists. Yaani mtu anaingia press bila hata kujaribu ku-collaborate habari yake!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 03, 2006

    I.M said...
    hIYO HAPO CHINI NDO LIST YA MANAGEMENT YA CHELSEA MPAKA JANA WAKATI ANACHEZA NA BLACKBURN...Na hii ndo imekuwa list ya management kwa season nzima ya league hajaondoka mtu wala kuongezeka

    The Management

    Jose Mourinho (Manager and First Team Coach)

    Baltemar Brito (Assistant Manager)

    Steve Clarke (Assistant Manager)

    Silvino Louro (Goalkeeping Coach)

    Andre Villas (Assistant Coach/Scout)

    Rui Faria (Fitness Coach)

    Ade Mafe (Assistant Fitness Coach)

    Mick McGiven (Reserve Team Coach)

    Brendan Rodgers (Youth Team Coach)



    Medical Department

    Bryan English (Chief medical officer)

    Dean Kenneally (First Team physio)

    Mike Banks (Reserve Team physio)

    Alex Nieper (Reserve Team Doctor)

    Ian McCurdie (Rehabilitation Doctor)

    Thierry Laurent (Rehabilitation)

    Rob Brinded (Rehabilitation)

    Billy McCulloch (Masseur)

    Stuart Sullivan (Masseur)

    Mauro Doimi (Masseur)

    Pedro Phillipou (Masseur)

    2:43 AM

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 03, 2006

    Michuzi,
    nataka kujua hilo shati la Makongoro kalipata wapi?

    ReplyDelete
  5. ndesanjo u hai? bwana ashukuriwe! nadhani mako alipitia kwa alinda sawe na mwafrika merinyo kule afrika sana. ila siku hizi kuna mtu aitwa ashura kawawa anatisha kwa mavazi kama haya. yeye anayatoa zairwaaa kwenyewe na ni babu kubwa. ukitaka kontakti zake sema

    ReplyDelete
  6. AnonymousMay 05, 2006

    mbona wanakuja kama wanasaka watumwa? Kwanza waafrika bado wanapata ubaguzi wa kutupwa huko ulaya halafu wanatuletea ahadi. Haya, nendeni mkazisaidie timu kupanda madaraja au zisiteremke kama kina okocha na kanu!

    Mimi ni more pan african. Nadhani tungejenga ligi zetu wenyewe, ndani ya nchi na kati ya nchi za africa. Tuongeze sponsorships na maslahi. Kwa nini tuwapelekee wazungu burudani, kuna mwingine aliyewahi kufikiri hivyo?

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 05, 2006

    Naungana na anony hapo juu! wakati umefika kwa sisi waafrika kujenga uwezo wetu ndani ya bara letu, na wao sasa waje kwetu, kweli huo ubaguzi kwenye soka unatisha, na si soka tu katika maeneo mengi tunashuhudia, kwenye treni mtu akikuta ni mweusi kwingine wanashuka, kwingine wanakutukana, sasa sisi afrika tuna rasilimali zote Mungu ametujalia, viongozi wetu waache ubinafsi, waache kujifikiria wenyewe, we can make it, kwani wao wazungu bongo zao ziko vipi wafanikiwe sisi tushindwe?

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 05, 2006

    the name is too long I propose mwalimu Nyerere stadium

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...