niko na mama kafanabo ubalozi wa bongo umoja wa mataifa hapa newala
a

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. mamaq kaenda shule huyo.

    ReplyDelete
  2. Unayo CV yake? Hebu nieleze kwa ufupi tafadhali.

    ReplyDelete
  3. Huyo mama yuko fiti, amewahi kuwa Lecturer IDM Mzumbe, vile vile anayo kitu kama CA au CMA ya Canada. Wabongo lazima mkubali vitu vya watu waliopiga shule.

    ReplyDelete
  4. Hata kama kasoma wapi huyo ni bwengo tu hana noma michuzi jitahidi tu,si unajua bwengo tena.

    ReplyDelete
  5. hivi Michuzi unapotoa picha za watu unaomba ruhusa zao kweli?maana unaweza ukamchafulia jina huyu mama wa watu maana si unajua tena kwenye hii blog kuna watu wamekaa kwa ajili ya kuchafua majina ya watu,wenyewe huwa hawana hata moja zuri la kusema, maana kama picha ya your nanihii, ona watu wanavyomsema, wkt anaonekana yupo fine kbs, watu wanataka tu kuchafua majina ya watu.

    ReplyDelete
  6. Huyo mama alikuwa mwalimu wangu Mzumbe. Ni mwalimu anayejua accounting kama alizaliwa naya. alihamasisha sana masuala ya usawa wa wanawake hapa chuoni. baada ya hapo amefanya kazi kwenye mashamba ya mkonge kuhamasisha wanawake katika maendeleo yao kiuchumi. Alikuwa pia mkuu wa kitengo cha jinsia. natumaini ulimuona kwenye kipindi cha tujisahihishe cha Utumishi. Nilikuwa sijui kuwa yupo huko ubalozini. lakini kama ilivyosemwa ndugu Michuzi umuondoe huyu mama maana kuna watu wanaopenda kuchafua majina ya wenzake. Sisi wanafunzi wake tutaumia sana ikitokea hivyo.
    anonymous

    ReplyDelete
  7. Ni kweli Michuzi, toa picha ya huyo mama, kwani watu wenye midomo michafu wamekwishaanza kumwaga matusi. Mimi pia ni malimu wangu pale Mzumbe miaka ya 1984-85. Hiki ni kichwa kati ya vichwa vilivyopo kwenye ardhi ya Tanzania lakini si bwenga bali ni Mngoni kutoka mkoa wa Ruvuma

    ReplyDelete
  8. Jamani kwa Watanzania wenzangu mnaotaka kuchangia hoja kwa sababu Michuzi anaamua kutuwekea picha zisizo na akili mi naona nitoe changamoto la kuanzisha hoja wenyewe.Kwa kuanzia niwaombe watu wote mnaotaka kutoa hoja sio mashindano bali tutoe mawazo kama tunayo bila matusi wala kejeli kwa mtu yoyote.

    Hivi karibuni nilikuwa naongea na marafiki huku US juu ya wabongo tulioko huku na nchi nyingine popote duniani, Baada ya kukaa huku kwa miaka mingi bila kumaliza shule na kujikuta wanafanya kazi za (manual labor), kwa makisio angalau asilimia 80 ya waTZ walio huku ndio wanachofanya,na kupata kwa huku US unapata angalau kwa kisio la chini $1600 kwa mwezi sijui nchi nyingine, Je ni wazo la maana kufikiria kurudi TZ ambako hata ukibahatika ukapata kazi hupati hata robo ya hiyo au wabongo waendelee kufanya tu hizo kazi. Mpaka lini?. Kwenye hoja zenu tuzingatie hiki wengi kati ya watu walio huku hawajatoka kwenye familia zenye uwezo na wakirudi nyumbani wanaanza wapi?.
    Hili suala kweli lina nitia huzuni nikiwawaza hawa vijana wetu waliopo kwenye hii njia panda ngumu, karibuni lakini nasisitiza tena kama huna hoja au unaona hili suala sio la maana kwako tujitahidi kulifumbia macho na kama unachangia toa point zako bila matusi wala kumkejeli mtu.

    ReplyDelete
  9. hili swala ni gumu zaidi kutokana kila mtu ana maoni yake. mimi pia nipo huku Marekani nasoma kwa scholarship, maana wazazi wangu hawana uwezo mkubwa wa kunilipia, ila nina marafiki wangu wapo huku wanasoma lkn ndo hao ambao hawamalizi shule wanaishia kufanya kazi, lkn ukiangalia huko Tanzania ni wametoka kwenye familia zinazojiweza kbs(si unajua tena kuna wabongo huku wanaishi maisha ya tabu wkt home ni wametoka kwenye familia nzuri), sasa mimi watu kama hao ndio huwa ninawashangaa, kwa sababu naona kama wanavoishi huku ni kupoteza muda, kwa sababu hawana cha maana wanachofanya, zaidi ya kushindana nani kanunua nguo ya bei aghali, wkt wakirudi bongo, na kumalizia elimu yao wanaweza kupata kazi nzuri( si unajua tena bongo wazazi wako wakiwa wanajulikana kuna chance kubwa ya kupata kazi nzuri)kwaio mimi kwa hawaatu ushauri wangu ni afadhali kurudi home na kufanya kitu cha maana. kama ulivoongelea khs baadhi ya watu wametoka ktk familia ambazo hazijaendelea sana huko bongo, mi naona kama huku alipo anapata kahela hata kadogo na kanamsaidia kuliko angekaa home na kutopata kazi nzuri mimi sioni ubaya wa yeye kuendelea kuishi huku na kuwa na maisha mazuri,

    ReplyDelete
  10. Michuzi tafadhali sometimes wengi wape toa picha ya huyo mama japokuwa mi binafsi simfahamu but she doesnt deserve all this crap,just because she took a picture with you or at least agreed to, usipoangalia sasa watu wataanza hata kukukimbia wewe ukitokea na kamera yako.

    ReplyDelete
  11. Nafikiri wakati umefika kuzibandua hizi picha za marais katika kuta za ofisi za serikali na badala yake tuweke alama za taifa kama vile court of arms(Tanzania nafikiri ni watu wawili na meno ya tembo), kitu ambacho raia wote (I mean 100% of the people) wanaiamini na kuithamini. Picha za maraisi zinawakilisha utawala(Dynasty), hivyo ni vizuri zikawekwe kwenye ubao wa historia.

    ReplyDelete
  12. La msingi hapa si kubandua picha ya mama Kafanabo, ila kuna wale vihiyo ambao hawakwenda shule kabisa na kuna wale wengine waliokubali matokeo na kuishia kuwa wajinga. Watu hawa wanatoka kwenye familia zenye uwezo TZ na wengine walikuwa na kazi nzuri sana Bongo na sasa hivi hawajitofauti na wale vihiyo kabisa.Muda unakwenda kila siku, uzee ndio huo unazidi kupiga hodi, utabeba boksi mpaka lini? hata kama huna "paper" kuna njia nyingi za kujiendeleza. Haya maisha ya kununua nguo nzuri,TV kubwa sio maisha kwa sababu mtu yoyote hata kama aliyekuja leo kutoka Bongo anaweza kuwa navyo. Jamani wabongo tupige hatua nyingine, hatua ya kwanza ilikuwa ni kuingia ughaibuni, na sasa tuko wengi sana kila mahali, lakini tunatakiwa tuanze kufanya kazi za "Professionals" ambazo uwongo mbaya zinalipa kishenzi na heshima unapata. Mwacheni mama Kafanabo ale matunda ya shule yake, wanafunzi wake tunathibitisha hilo.

    ReplyDelete
  13. mimi nakubaliana na wewe, khs watanzania kujiendeleza. Mi nafikiri ile enzi ya kutambiana nani ana hiki ni vitu vya zamani. mi nakwambia huku kuna watu wanavaa nguo za bei, wana maplasma lkn karibuni kila siku anakuja kukuomba umkopeshe hela ilipe rent, sasa we unajiuliza inakuaje bwana,maana ukiangalia vitu vyake vyote vimeenda shule(aghali), kumbe ye anaishi kwa mashindano, ndio maana hatuendelei. lkn hili tatizo si nje tu, hata bongo lipo sema bongo wengi(hasa vijana) wanatoa hela kwa wazazi wao, sasa huku wapo wenyewe ndio maisha magumu zaidi,lkn huku sio watanzania wote wapo hivi. mimi kuna baadhi ya watanzania nawajua wapo simple kweli, hizo hela wanazozipata wanasave na kutumia kwa manufaa zaidi na ukiangalia hao ndo at least wameendelea kimaisha huku.halafu mtoa maoni hapo juu amesema kufanya kazi za proff. mi nakuambia huku tena hii miaka kupata kazi ya ofisini huku marekani ni ngumu sana, maana baada ya sept 11, wamekua wagumu sana, na tena ukipata ni bahati yako, sasa huku utakuta kuna watu wamesoma hadi masters, na kila siku wanatafuta kazi hapa lkn hawapati, wengine wanakaa hata mwaka bila kazi ya maana, halafu anaishia kufanya kazi isiyo na maaana (sio ya elimu aliyosomea)sasa ukimwambia kwa nini asirudi bongo ambapo chance kubwa ya kupata kazi ipo , anakataa kurudi, kwaio inaelekea watu wengine hawapendi kbs kurudi home, kwaio wapo radhi kufanya hizo kazi, mimi nafikiri katika akili zetu tuna fikra kwamba maisha bongo hali ni ngumu sana, maana ukimwambia bongo mshahara mtu unapata laki 3 anafikiria sana, wkt hiyo hela anapata kwa wiki huku, lkn wanasahau kua hali ya maisha huku ni aghali zaidi kuliko ya bongo, pmj na bongo maisha ni expensive kama ukiwa unataka starehe, kwaio hii nafikiri ndio inayoogopesha watu, lkn kwa mtazamo mwingine huku kuna wabongo walioendelea kwa kufanya kazi hizihizi kwaio hapo sina maneno..

    ReplyDelete
  14. watanzania,
    Bado tuna mawazo ya kuwa ma kuli tu? Hivi kwani kila aliesoma shule lazima aajiriwe? Kama ametafuta kazi amekosa kwa nini asijiajili? Tofauti kubwa hapa ni kujiajiri na kuajiriwa.

    Hii mentality ya kuajiriwa tumeitoa kwa wazazi weti ambao kutwa nzima walituhimiza tusome ili tupate kazi nzuri.Lakini hatujui kuwa wazazi wetu walipata hiyo mentality toka kwa wakoloni ambao walitutumia sie kama makuli, wao watawala na wahindi kama wafanya biashara.

    Sasa mbongo akishasoma anaona ni haki yake kunyaka mzigo.Asipopata anaanza kuona dunia imeisha.Anashindwa hata kufikiria afanye nini.

    Moja ya story zinazofurahisha sana ni story ya Founder wa Walmart Sam Walton.Alipomaliza shule(university) alikosa kazi kabisa na kuanza kulalamika kwa baba yake.Baba yake akakuambia kama hawataki kukupa kazi kwa nini usi create your own job? Hapo jamaa alipata usongo na kuamua kuingia kwenye ulimwengu wa biashara.Leo hii nani asiejua Walmart?

    Mie nawapa changamoto wabongo msitegemee kuajiriwa sana.Watu wengi walioajiriwa hawatakufikia hata robo kama ukiingiakwenye ulimwengu wa biashara.Angalia Forbes magazine list ya watu matajiri na wote wale wamejiajiri.

    Kwa hiyo tieni akili na jaribuni kujenga utamaduni wa kujiajiri na sio kuajiriwa.

    mturutumbi

    ReplyDelete
  15. Nadhani ndugu yangu hapa juu umetoa ushauri mzuri kuliko wote juu ya kuanza kufikiria kujiajiri wenyewe wabongo huku tulipo.

    Lakini baada ya kusema hivyo nadhani pia niongeze kwamba watanzania lazima tukubali kwamba lazima tukae na kukubali kwamba ni muda wa kusaidiana na kuanzisha kitu kitakacho tusogeza mbele popote tulipo.

    Ninachozungumzia ni tujaribu kupatiana ushauri na kumsupport mtu ili angalau tuweze kupata pa kuanzia. Kwa sababu najua huku tumejaribu kuanzisha ushirikiano mdogo mdogo mara nyingi lakini huvunjika hata kabla haujasimama wenyewe kwa ajili moja tu ya kila mtu kutaka kujua zaidi na kutotaka kusikia mtu mwingine anatoa idea asiyoikubali, kwa sababu bila kushirikiana safari ni ndefu, na ukweli ni kwamba watanzania tuisogope kuingia kwenye biashara tujaribu kuresearch njia tofauti za kupata mikopo huku na tupeane usaidizi jamani.

    ReplyDelete
  16. Mimi nimekuwa nawaona vijana wengi sana wanaokatalia marekani, na nchi mbali mbali za ulaya wakati wana masters, phd na hawana kazi za maana hawa ni wale wasioweza kukabili challenge na kukubaliana na ukweli.

    Ushauri wangu wenzenu walioko tanzania pamoja na pesa ndogo siyo kwamba wanatembea hila wanakimbia pamoja na pesa ndogo wanayoipata lakini nawaambieni wanaitumia inavyotakiwa na naona wako better uzeeni kuliko kusubiri uzeeeke ukiwa ugaibuni.

    Mmesikia baadhi ya shule zetu, vyuo vyetu havina walimu sasa changamoto ni hii jitahidini rudini mkajenge taifa lenu.

    Taifa lenu bado linawaitaji sana mimi nashauri siku hivi utandawazi umetusaidia tumepata mawasiliano pepe tafuta mbinu mbali mbali za kupata ajira za kibongo msisubiri ukaletwa huku ukiwa mzee, ukafikia kwa brother wako au mjomba, ndugu zangu fikirieni hili suala, mkituma pesa sisi twala.

    tengenezeni maisha yenu sasa hivi.Jengeni tanzania sasa.

    wakati unaokuja ni wakati wa mashindano ya kitechnologia, hakikisha hayakukuti nje. kama ni kuanzisha kakampuni kako bahati nzuri huko nchi zilizo na technologia tumia mwanya huo kuleta technologia ya kukusaidia nchini mwako.Au potelea mbali tafuta pesa za kuagiza tractors hili ukifika ukaanzishe kilimo cha kisasa, tanzania ardhi ni tele yenye rutuba sehemu nyingi siwezi taja na kumaliza.

    Asanteni naomba msinishambulie.

    ReplyDelete
  17. Mimi siku zote nashindwa kuelewa kwa nini watanzania tuko so opinionated , kwanini siku zote tunajifanya tunajua kitu gani ni kizuri kwa mtu mwingine ! kwa nini ? Jamani ni lazima tukubali ya kuwa kutokana na maendeleo ya teknolojia ulaya & marekani sio mbali kama watu wanavyosema .Mbona wazazi wetu walitoka vijijini kuja kutafuta maisha mjini?

    Mnasema watu warudi nyumbani wakati hapa ninaivest hela zangu kwenye 401k na social security by the time nikiretire napata hela nzuri .

    Vipi kuhusu watoto wangu wanaosoma shule nzuri na wana uhakika wa kusoma mpaka college hata kama bahati mbaya nikiwa sina hela . Msiangalie upande mmmoja tuu , angalieni pande zote ! Huyo mtu mnayesema anabeba boksi anaweza kumsomesha wadogo zake hapo chuo , kitu ambacho ni kigumu kwa mfanyakazi wa kawaida hapo nyumbani.

    Watu warudi Tanzania kufanya nini , wakati viongozi wetu hawainvest katika future , wanafikilia kujenga bandari bagamoyo wakati tuna bandari Kubwa na yenye kina kirefu mtwara .Wanafikiria kununu lada kulinda anga wakati ndege zinazotua ni kumi , wanafikiria kununua jeti wakati inaweza kutua kwenye viwanja vinne !

    Mnasema uchumi unakua , uchumi utakuaje kama huna huduma muhimu kama umeme?

    ReplyDelete
  18. Anony sep 24th, 2.00 am, umeongea point, tena kwa njia raisi na nyepesi kueleweka zaidi ya waandishi wa habari wengineo humu ndani.

    ReplyDelete
  19. kwanini mtung'ang'ania turudi turudi jengeni nchi yenu kama mna uwezo kumbe mnajua tuna umuhimu eeee msituchoshe sisi kila mtu katika maisha yake ana malengo na nia ya kufanya jambo fulani sula si kufanya kazi tuu CRDB nikifika miaka sitini nistaafu eti nilipwe hela ya uzeeni hayo ni mawazo ya chini sana na inasikitisha sana....

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...