mwalimu alikuwa anajichanganya sana na viongozi wengine

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Jamani huo mkutano! Kaunda, Mobutu na Castro? mmmh! najaribu kufikiria ni nini hasa kilikuwa kinaongelewa hasa na huyo mwizi Mobutu wanaemsikiliza, hebu mwone alivyovaa, utawajua tu!

    ReplyDelete
  2. Mobutu peke yake ndiyo alyekuwa kavaa nguo za gharama wengine wote wamechoka na kaki zao za kichina!! Na cheki wanavyomsikiliza huyu mwenye noti.Hata Castro kabana mikono.Nyerere katoa macho anashangaa utajiri wa mwenzie kama yuko ferry.Kaunda anachekacheka tu hovyo.Kuna nini cha kuchekelea peke yake hapo.Ama kweli mwenye hela akisema hata kisicho cha kuchekesha lazima ucheke.

    ReplyDelete
  3. Joseph Desire Mobutu aka Mobutu Sese Seko Kuku Ngbeku wa Zabanga, Jogoo la majogoo wote, well...nadhani picha inajieleza hapo!

    ReplyDelete
  4. Ndio maana hatuendelei, hivi Mobutu nchi yake tajiri, maliasili za kumwaga lakini leo masikini na watu mamilioni wamekufa yote sababu ya utawala wake mbovu tunamshabikia nini? Mobutu akakubali kutumiwa na CIA wakamwangusha Lumumba, kisha nchi ikatumbukia kwenye uozo, wizi aliofanya, akisaidiwa na hawa wafilisi wenye makampuni makubwa, na uovu wote, eti tunashabikia nguo zake, utajiri na majina yake?
    Sawa hao wengine wamechoka, na itikadi zao hazikufanikiwa sana hasa kwetu lakini uovu wa kijinga haukuwepo. Fedha nini kama vifo vya mamilioni viko juu yako? zaidi ya yote, hao waliokuweka madarakani wanakugeuka, unaishia kufa tu kama wengine, unatuachia maisha mabovu!

    ReplyDelete
  5. Kuna watu wana sahau kuwa Mobutu hakuwa mjinga !Kumbuka viongozi wengi tulionao Afrika sio wajinga ,tatizo ni nini wanakipa kipaumbele na nini wakotayari kukikabili kwa faida ya wote. Katika picha si ajabu Mobutu ndio alikuwa anatoa pointi nzuri kabisa ambazo ni za kusaidia watu kwa ujumla kwa sababu alijua walio mzunguka ni akina nani.Hivyo siwezi kushangaa akisikilizwa. Halafu inawezekana kabisa wengine wote walikuwa wana mshangaa kuwa huyu mchekeshaji kwanini hafanyi ayazungumzayo! Yote tukiachia pembeni bado washindi katika kikao ni wawili. Cuba mpaka sasa hivi haijaomba msaada popote iwe chakula wala madawa. Nyerere pamoja na mengi kushindwa bado kuna mengi alifanikiwa na bado yana fanikiwa.

    ReplyDelete
  6. Kifo na maziko ya Mobutu Sesseseko wa Zabanga wa Dondo ni somo tosha kwa viongozi wa Africa na hasa TANZANIA kwamba kujilimbikizia Ukwasi wa kutosha hakukuakishii kifo/maziko mema. Nyerere hakuwa na mali lakini amekufa na kuzikwa kwa heshima zote.Kaunda nae hana kitu wala madaraka lakini anaishi kwa amani na heshima kwake Zambia.Mzee Fidel nae anapeta mpaka leo bila wasiwasi.

    ReplyDelete
  7. Hiyo picha ilipigwa 1978 Castro alivyokiamulia kuja Bongo bila mwaliko. Kaunda na Mobutu walikuwepo kwa ajili ya mkutano fulani.

    BANDUNDU

    ReplyDelete
  8. Hongera askari wa Rwanda na Uganda kumtimua Mobutu na wacheza ndombolo wa Kongo na kubaki Kongo mkifukua dhahabu tofauti na wazalendo wa JWTZ wa Tanzania.Majeshi ya Tanzania yangekuwa nayo yamebaki Kongo yakifukua dhahabu kama wenzao Tanzania ingekuwa mbali lakini tatizo la majeshi ya Tanzania yakipigana hayang`ang`anii kwenye migodi na kugoma kuondoka.Tabia mbaya sana hii.Ukishapigana fukua dhahabu ufidie gharama zako za vita.Tungeng`ang`ania Kongo sasa hivi Tanzania tungekuwa mamilionea iwe kupitia serikali au kupitia majenerali na wapiganaji.Vita siku hizi ni sehemu ya kujikomboa kiuchumi pia.JWTZ acheni kupigana vita ambazo haziingizi chochote kwenu binafsi kama jeshi au kwa uchumi wa nchi.Bush mwenyewe hapigani vita kisengesenge pamoja na kuwa nchi yake ni tajiri lazima ajue atapata nini kwanza.Kwa kubaki Kongo, Kagame hoyee!!!!Museveni hoyee! JWTZ ziii!!

    ReplyDelete
  9. Mobutu tatizo lake kubwa aliwafundisha wakongo Utapeli,Uchawi na kupenda utananashati na starehe sana ambazo ndizo sifa kuu za karibu kila mkongo utakayekutana naye. Kwa hayo matatu kila Mkongo ana sifa hizo Raisi Joseph Kabila pia akiwa mmojawao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...