naomba nijichovye kwenye haka kamjadala kanakohusu lebo kwenye suti, kwani na mimi sijaondoa kwenye vimitumba vyangu kwa sababu lebo zake zimeshonewa kihasa. sasa kama ilivyo kwa masudi kipanya, mie pia kwa upande wangu nimeshachanganyikiwa; nizinyofoe ama niziache??? wadau naomba msaada...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Jamani hizo lebo ni za kuondolewa, hivyo mzee michuzi nenda kaondoe mchizi wangu !!!

    ReplyDelete
  2. Tazama email yako kaka michuzi.. Halafu hiyo Lebo iondoe...Unless unataka kuiuza tena hiyo Suti.... Hehehehe.

    ReplyDelete
  3. Mzee Michuzi, hiyo label unatoa, kama imeshonewa vizuri...kata taratibu usiharibu suti, ila label unatoa

    ReplyDelete
  4. Siku zote nilikuwa nakuheshimu sana. sikujua bado u mshamba kiasi hicho. Chini ya kilebo ndani ya mkono wa suti kuna vishina vya uzi unaoshikilia kilebo; wote tunakata kwa wembe na kinatoka huku nje bila mikwara yoyote. Rejesha heshima yako!!

    ReplyDelete
  5. Bwana mambo ya kuacha lebel nje ni ushamba Mzee Michuzi. maana watu wanavaa designer stuff na wala saa nnyingine huwezijua maana lebel zinakuwa ndani, mpaka uchungulie nguo ya mtu ndani ndio utajua kama ni CHRISTIAN DIOR, YVES SAINT LAURENT, RALF LAUREN,CHANEL,TUXEDO,GUCCI, PRADA, nakadhalika. na watu huwa hawajivuni wanaotilia viwalo heavy kama hivi wala huwezijua. sasa mambo ya kuachia lebel nje nakubaliana na waungwana wote hapa ni USHAMBA, Mzee kwa hiyo unatakiwa utoe hiyo lebel, lakini nyingine huwa zimeshonewa kwahiyo chonde chonde Mzee Michuzi taratibu tumia kiwembe ili usije ukaiharibu suti yako kwa kukosea ukaikata MAANA NAIONA HIYO SUTI ULIYOIVAA NI YA UHAKIKA, YA NGUVU NA KAMA SIKOSEI NI DESIGNER. Niambie basi ni designer gani, mimi nadhani ni Tuxedo au nimekosea?

    ReplyDelete
  6. Mchuzi, weka chini kamera yako! Wacha kuandika kwa komputa! Kimbia mara moja kwa fundi cherehani! Mwambie aiondoe hiyo label! La sivyo, nitakuja kuing'ofua!

    Case closed.

    Guys wenye hayo malebo, mnamkoga nani? It is an element of exhibitionism and unbecoming show-off! Simply put, fikira finyu!

    ReplyDelete
  7. weee kaka weeeee kelele za chura hazimzuwii tembo kunywa maji.... kwahiyo mwanangu weye tuu kama unataka lebo lako lionekane WHY NOT jirushe nalo mwanangu ila kama hutaki basi nenda kanyofoe!!! Hiyo ni idara binafsi na ni maamuzi binafsi!! Kuhusu ushamba ama sio hizo ni kelele za chura tuuu!! Kwa. nza kalebo kako kamekupendeza kweli kweli umemechi na viatu... huraaaaaaaaaaaaa. Ni mimi dadaako

    ReplyDelete
  8. Hakuna ushamba .Amua mwenyewe.Mbona mnavaa nguo zina majina ya watu hamuoni ushamba

    ReplyDelete
  9. Jamani Watanzania woe tulio nje ya nchi Bongo kuna raha ukiwa na kisu cha uhakika utaona hamna haja hata ya kuja ughaibuni au nchi yeyot ile.Nimekuja ughaibuni mwaka 1999 lakini nimerudi bongo mara 5 kwenda kula raha...na kufanya investments mapema kabla ya kuanza safari ndefu ya maamuzi ya kurudi kimoja.Bongo kama una hela utaenjoy..na hata ukiwa na elimu ukapata channel nzuri ya kazi utaenjoy sana.Ila cha muhimu zaidi ni kumuweka Mungu mbele.

    ReplyDelete
  10. Michuzi mimi ni yule yule ninayeongelea jinsi ambavyo unaweza ukaenjoy back home kama una kisu.Yes,hizo label toa kwa suti hatuvai suti na label zilizoko kwenye mikono.Usijali Michuzi kuuliza sio ujinga!!Na kutembea ndio kujifunza.Watanzania wenzangu msikae nje ya nchi mkaoza bila kuw ana paper za kuwafanya mrudi home na kuona hali halisi na kujua utafanya nini kuisaidia jamii yako na watanzania wote kwa ujumla.

    ReplyDelete
  11. Kaka Michuzi mimi huwa sipendi kuongea vitu tu, LAKINI nilipomweleza Kipanya kuhusu label ya suti nilikuwa NAMAANISHA inabidi iondolowe! Na kama sikosei, mimi nilikuwa wa kwanza kuwaeleza kuhusu hiyo label naye Zemarcopolo akasema HAITOLEWI. Lakini ndugu Michuzi, LEBO huwa inatolewa jamani. Revd.

    ReplyDelete
  12. ACHENI UTANI JAMANI,MICHUZI ANA SURA MBAYA!!

    ReplyDelete
  13. Michuzi sasa noan unaanza kuuza Sura!... sio mambo hayo...
    mtu mzima wewe

    ReplyDelete
  14. kama kuna mafundi washamba basi mafundi wa ughaibuni wamezidi, maana kila suti utaikuta ila label mkononi lakini kama utavaa suti aliyoshona fundi Massawe au fundi Mkude wala hutakuta kaweka label kwenye mikono

    ReplyDelete
  15. Michuzi naona unazuga tu.Tuambie umevaa lebo gani au designer gani

    ReplyDelete
  16. Michuzi, unaonekana dingi siku hizi! Hapo siyo Boston State House kweli?

    ReplyDelete
  17. Kuacha label nje ni ushamba tena sana, sasa li-label linaning'inia la nini? kama suti yako ni nzuri maaterial itaongea yenyewe.

    KIMBIA HARAKA SANA KWA FUNDI CHERAHANI AKUTOLEEE - TENA NISIKUONE KABISA,

    Usijefanya hadhi yako mahiri idondoke

    ReplyDelete
  18. Muhidini, Lakini label nyingine zinapendeza mpaka inabid ufikirie mara mbili kabla kubandua.
    Wazungu wanatuletea nguo halafu na mitihani ya jinsi ya kuvaa.-Regards Babu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...