jk na mama salma kikwete wakimpa pole halima mchuka, mtangazaji maarufu wa
rtd ambaye anaugua kiharusi. halima ni mtangazaji pekee wa kike nchini, kama si afrika nzima, anayetangaza soka kwa ustadi wa hali ya juu. tumwombee apate nafuu haraka kwani tunammiss saaana

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 30 mpaka sasa

  1. Kiharusi ndio ungonjwa gani?
    Whatever it might be GET WELL SOO DEAR

    ReplyDelete
  2. Iwas wondering too...wishing you a quick recovary maam....

    ReplyDelete
  3. Kiharusi ni Stroke

    ReplyDelete
  4. Pamoja na kutakia Halima uuguwa pole napenda kumwambia mheshimiwa rais hii sasa ni too much with this cheap politics which will not take the country anyway. Rais ni mtu mkubwa saana sio kila mfanya kazi wa serikali akiugua lazima uende kumuona. Kama ulienda kuangalia huduma hospital ya Taifa hilo linaeleweka, lakini kama kwenda kumuona mtangazaji tu hapo kwakweli unashusha hadhi ya cheo chako na kuturudisha enzi zile za mzee rukhsa za kila msiba wa mtu anaetajwa redio lazima aende mpaka aliposhauriwa vinginevyo na JKN.

    ReplyDelete
  5. amekuwa too cheap,hata pm mwenyewe sio hivyo,au labda huyo mtangazaji ni ndugu yao.

    ReplyDelete
  6. Pole sana mgonjwa. Sipendi pia cheap politics za mtu huyu/waswahili. Nchi hii ina mambo mengi muhimu yanayohitaji seriousness lakini wanayatelekeza. Hawana priority! Hatuendi hivyo jamani.Nchi haitosonga mbele kwa mtaji wa kutofanyia kazi mambo mazito. Mnapewa miaka kumi mnatoka mifuko yenu tu ndio imejaa sisi mnatutelekeza!

    Misoup usipopublish hii mwanao na mwanangu wasisalimiane!

    ReplyDelete
  7. huyo anony wa hapo juu nadhani nae ana matatizo kwa sababu rais alikuwa na ziara za nje mkalalamika sasa hivi angalau yupo nyumbani na kuonesha uzalendo wake anakwenda kumsalimia mgonjwa ambaye ni mtu wa kawaida mnalalamika,angekuwa amemtembelea mtu wa cheo fulani wala msingelalamika.Binadamu wote ni sawa

    ReplyDelete
  8. Pole sana Halima Mungu atkunusuru nautapona.Wewe anony hapo juu rais anjishusha hadhi ya kwenda kumuona mgonjwa unaonyesha ni kiasi gani ulivyo wa ajabu!Mheshimiwa rais ni kawaida yake hata kabla hajawa raisi alikuwa hivyo kwa hiyo hawezi kuacha asili yake,nyie ndiyo wale watu ambao mkipata madaraka hata ndugu zenu kuja majumbani kwenu kwa appointment.Kazi kubwa kujikweza tu mnataka mnyenyekewe kama mungu watu,Kikwete siyo wa aina hiyo

    ReplyDelete
  9. mmmh ur right anony 7:22:34, rais anazidi ss, kuna mambo mengi yanayomuhitaji kuyafanya na si kwenda kumuona kila mfanyakazi anayeumwa..nadhani yule aliyesema jk anafikiri bado yuko kwenye kampeni was right..pfffffffffffff

    ReplyDelete
  10. Haha, ni kweli kabisa 7:22, ndiyo tanzania yetu hiyo. Tukisema Mungu ibaridi, we usually really mean it, kwa sababu kazi ipo si mchezo.

    ReplyDelete
  11. Mimi sioni shida president kumtembelea mtu kadiri anavyoona inafaa. Hebu chukulia halima ni ndugu wa familia, au ni rafiki wa familia. Kuwa raisi wa nchi siyo kigezo cha kukutenga na jamii inayokuzunguka. Tusisahau kuwa pomoja na urais kuwa nafasi muhimu katika nchi, lakini rais ni sehemu ya jamii inayomzunguka. Ni lazima awe na muda na watu walio karibu naye. Tatizo hapa ninaloliona mimi ni kitendo cha waandishi wa habari kufanya kila kitu anachokifanya rais ni habari ya magazeti. Ni tatizo la waandishi kushindwa kutathmini jambo gani ni muhimu na jambo gani siyo muhimu kuwahabarisha wananchi. Wakati mwingine, habari nyingine zinafanya vyuombio vya habari vionekan udaku tu kwa kutoa habari ambazo ni very personal. Na tatizo hapa inaokena kama rais anaiwakilisha nchi kwenda kumuona mtangazaji , wakati huenda alichokifanya ni very personal.

    ReplyDelete
  12. Anonym wa jan 10 time 10:21 AM hapo juu unaona mbali na unaakili kweli kweli;yaani mtu kuwa Rais basi akiuguliwa na ndugu jamaa haruhusiwi kwenda kuwaona simply because kikatiba siyo sawa?watu wa magazeti ndiyo wenye matatizo;udaku tu wa ku-publish kila kitu kifanywacho na Rais,kumbukeni"He's a Man and a Human being first before anything else" na hizo qualities hazimbadilishi mtu hata awe Pope.Nyerere mwenyewe alikuwa na personal visits kwa wagonjwa hospitalini kwa ndugu na jamaa zake;kikubwa cha kujiuliza ni je anakwenda kama Rais wa Nchi au kama jamaa wa yule mgonjwa? mimi nafikiri kwa issue hii ya JK,kwenda kumuona Halima amekwenda k.m ndugu au jamaa wa karibu na siyo Rais,ila magazeti na udaku wao nao hao lazima wanyake;Kitu ambacho labda ningemkosoa rais ,ni pale ambapo ukitokea msiba wa kitaifa;mfano yule driver wa daladala aliyepigwa risasi na mheshimiwa Ditto,pale k.m akienda ni kwamba anakwenda k.m Rais na si JK unless ana uhusiano wa karibu na ile familia;sasa kwenda yeye kutoa pole badala ya Waziri Mkuu;au Waziri wake anaehusika moja kwa moja hiyo kidogo iakuwa ni kushoto

    ReplyDelete
  13. Jamani, ikiwa ni sawa kwa rais kwenda kuona wagonjwa, kuhudhuria kila mazishi/msiba, kuhani kila wafiwa, basi kuna haja gani ya yeye kuwa na msururu wa body-guards na kuishi state house, na kuwa na ndege ya rais. si awe tu wa kawaida ili tujue kwamba yeye sio mtu maalumu!. lazima kuwe na tofauti bwana. he can always send a representative with a personally writen card or headed note. jamani, too much now

    ReplyDelete
  14. Raisi ni mtu wa pwani na ni mswahili pure. Na ndiyo maana anawathamini watu wote, kama hivi kwenda kuwaona wagonjwa. Raisi Mwinyi pia alikuwa hivi. Hawana makuu. Sasa sijui nyinyi mnao mlaumu raisi ana fanya uswahili ni wazungu? Hata hao viongozi wa nchi zilizoendelea ni jambo la kawaida kuwatembelea wagonjwa. Tembeeni muone.Mimi sishangai hata nikimuona anawatembelea wacheza bao, ni vizuri kiongozii kuwa karibu na watu. Huyu ni mtu wa watu.

    ReplyDelete
  15. POLE SANA HALIMA, MUNGU ATAKUBARIKI UTAPONA KWANI WEWE NA FAMILIA YAKO NI WAUNGWANA.
    NILIKUONA HAPA ARABELLA NA DADA YAKO WA AIR TANZANIA -MWAJUMA MCHUKA- AKISALIMIANA KWA KARIBU NA PETER RUPIA NA GIRLFRIEND WAKE IRENE. SIKU AMBAYO DR. ASHAROSE MTENGETI MIGIRO ALIPOKUWA MGENI RASMI KATIKA SHUGHULI, HAPA MIE NI MFANYAKAZI WA HAPA NA NILISOMA NA MAREHEMU MDOGO WENU YULE ZAINA MCHUKA, (FORODHANI HOTEL MANAGEMENT) SASA NIKO SEA CLIF, TANGU JANUARY MOSI.
    MUNGU AWE NANYI KATIKA WAKATI HUU MGUMU, NA AMPONYE HALIMA MCHUKA.
    POLENI SANA.

    ReplyDelete
  16. Toto zuri hilo!! Check Kikwete alivyolikumbatia.Mkono wa kushoto kalikumbatia kwa chini na mkono wa kulia kalikumbatia kifuani mbele ya mama Kikwete.Mama Kikwete kaduwaa hajui acheke au alie!!

    Michuzi kama Muhimbili kuna mitoto mizuri hivi mimi sasa hivi nitakuwa naenda kuangalia wagonjwa kila siku Muhimbili wallahi! Kuna watoto wazuri huko wamelazwa kuliko hivi vimiss nani sijui vinavyovaa visuruali vya jeans vya milegesheo vilivyokaukiana utafikiri vinakula nyau eti vinajidai English Figure.Uongo.Lishe duni tu havina lolote.Mbona huyo pichani ni mgonjwa na kanenepeana.

    ReplyDelete
  17. SIDHANI KAMA KUNA SHIDA RAIS KUMSABAHI HALIMA. KWANZA HATUJUI KAMA NI NDUGU AU VIPI. ILA KAMA IS JUST MTANGAZAJI MZURI WA MPIRA, NA RAIS KAFUNGA SAFARI RASMI TOKA IKULU JUST KUMUONA YEYE TUU BASI HAPO ITABIDI SISI WANANCHI TUTOE MALALAMIKO YETU KWANI TUNAELEWA SIO YEYE TUU BALI NI DELEGATION KUBWA - BOARDGUARDS, NA MAPOLISI KIBAO NA WAANDISHI WA HABARI NA VING'ORA KIBAOOO TOKA IKULU WHICH COSTS KODI ZETU. KAMA ALIKUWA ANATEMBELEA HOSPITAL KWA UJUMLA NA BY THE WAY AKAAMBIWA HALIMA YUPO PALE BASI AKAONA AKAMSABAHI BASI NA ADUMU!!

    SIJAWAHI SIKIA TONY BLAIR KAENDA HOSP KUMUONA INDIVIDUAL UNLESS KUNA A BIG ISSUE BEHIND IT... HATA WALIPOLIPULIWA JULY LAST YEAR ALITUMA SALAMU ZA JUMLA...

    ReplyDelete
  18. Mheshimiwa Raisi rudi ofisini ufanye kazi. Kututembelea watanzania Milioni 33 kila mmoja kwa wakati ukimaliza hiyo miaka 10 bado utakuwa hujatumaliza. Shughulikia maswala ya kitaifa SIO BINAFSI. Kama mtu mmoja alivyosema hapo juu HUU SIO WAKATI WA KAMPENI BABA. KAMPENI ZIMEISHA, tafadhali fanya kazi.

    ReplyDelete
  19. Mnaomtetea JK achani hizo. Kama ambavyo mchangiaji mmoja kasema hapo juu, hivi ni barabara ngapi zilifungwa kwa ajili ya msafara wake tu? Kwani simu na kadi ni za nini? Kwa nini asiige simu na kumtakia kupona haraka? Huyu Rais na mkewe ni washamba sana wamelimbukia Ikulu sasa wanafanya mambo ya ajabu ajabu. Hata Kama Bi Mchuka ni ndugu yake je ndugu zake wako wangapi na je atawatembelea wote?

    ReplyDelete
  20. Cheki, bro na sis, hayo makono ya Ikulu...dhahabu tupu! Heleni ndio hizooooooooooooooooooo! Hilo lipete la...(sijui nisemeje?) dole kulia...dhahabu tuuuupu!

    ReplyDelete
  21. Kama kawaida, watu washaanza kudiscuss mengine. Ama watu hawa ni wapotevu. Mnataka kusema kuwa katika mwaka huu mfanyakazi aliyeugua ni Mchuka peke yake? Mimi siamini hilo, inawezekana ni wengi tu wameugua lakini hatujasikia raisi ameenda kuwaona. Kwenda kwa Mchuka ni moja tu ya mambo ambayo amefanya kama JK na sio kama raisi. Kwani hapo mnaona body guard, acheni ujinga wenu hapa.

    Kikwete kama kikwete ni kama nyie wapumbavu wote, sema yeye ni raisi. Ana huruma kama wewe, na haujui Mchuka ni nani wake.

    Acheni ujinga wenu wa ku discuss pumba hapa. Ongeeni mambo ya maana.

    By the way Raisi hawezi akawa anafanya kazi masaa 24. Kuna nyakati atahitaji kutembea, kusalimia ndugu nk.

    Alaaaaaaaaaaaaaaaa, mnakuwa na mawazo ya kitoto hivi hivi tunaona.

    ReplyDelete
  22. Angeenda kumsalimia mtu mwenye jina kubwa mgesema. Ameenda kumsalimia huyu dada mnasema. Hao marepoter ndio wamezidi. Kumfuata mfuata kujua kila kitu. Sijui wanajua private time na public time he needs some privacy too. Reporter wanahitajika kujifunza public communication and public relationship too. Huyu raia na ana all the rights to talk to her president na many be ni family friend who cares..

    ReplyDelete
  23. lakini, waandishi wa habari au wapiga picha ni vipi wanapata ratiba (binafsi) ya rais?

    ReplyDelete
  24. weye MWANAHAMISI unaonekana kweli unafahamiana na hawa kina MCHUKA'S mana kweli walikuwa na mdogo wao mzuri sana ZAINABU MCHUKA, aliyefariki dunia mwaka 1989 kwa ugonjwa wa kisasa, mchumba wake NZUNDA alitangulia kwa ugonjwa huo huo.
    pole sana Halima Mchuka, mola yu nawe na utapona tu kuwa na subira. poleni wanandugu wote pia.

    ReplyDelete
  25. Michuzi you're becoming extremely annoying now. I posted a comment two days ago, a very basic and genuine comment, but it's nowhere to be seen.

    ReplyDelete
  26. ASANTE ANONY WA january 11, 3:4:00am NI KWELI KABISA NAWEWE YAONEKANA UNAWAFAHAMU PIA HAWA KINA MCHUKA, ZAINA ILIKUWA RAFIKI YANGU SANA, TULISOMA WOTE KAMA NILIVYOJITAMBULISHA AWALI, NA WOTE TULIKUWA TUNAISHI ILALA, NI FAMILIA NZURI SANA, NA SIKU YA MWISHO KUMTIA HALIMA MCHUKA MACHONI NI SIKU NILIYOIELEZA ARABELLA MWAJUMA MCHUKA WA AIR TANZANIA (DADA YAO MKUBWA ALIYEWALEA WOTE, MUNGU AMBARIKI) WALIKUWA WOTE NA ALIKUWA AKISALIMIANA KWA KARIBU NA PETER RUPIA NA GIRLFRIEND WAKE IRENE, NAPENDA KUSEMA KUWA NAMFAHAMU PIA IRENE LAKINI HAKUNIKUMBUKA, NA NIKAONA NOMA KUJITAMBULISHA KWANI WALIKUWA WENGI KWENYE MEZA, KAPENDEZA SANA NA YUKO MDOGO VILEVILE HAJABADILIKA INGAWAJE NASIKIA ANA WATOTO WATATU SASA. WALIKUMBATIANA KWA NGUVU NA SHANGWE NA MWAJUMA MCHUKA. NI WAUNGWANA HAWA TUWAOMBEE MDOGO WAO APONE KWANI UGONJWA WA KIHARUSI, NI MBAYA SANA, MUNGU AMSIMAMIE HALIMA MCHUKA APONE NA ATOKE SALAMA MUHIMBILI.

    ReplyDelete
  27. wewe Mwanahamisi, samahani naona kweli wajuana na hawa Mchuka's. Mana kila ulichosema ni kweli kabisa, lakiiiiiini unamjua kweli Irene huyo girlfriend wa Peter? mana mimi binafsi namjua, kweli ni mzuri na amejitunza vyema kwani ni mdogo vilevile na tena amezidi uzuri huwezi kuamini kazaa watoto. Lakini shosti mboni umekosea? kama kweli unamjua basi utajua kuwa ANA WATOTO WAWILI TU. sio WATATU, kama unatafuta tu ushosti kwa kumfagilia hapa sema, lakini inavyoonekana humjui vizuri huyu Irene. kutokana na fact hiyo. na je unafahamu aliolewa kwenye presidensial family?
    Samahani lakini imebidi nikukosowe hapo.

    ReplyDelete
  28. KWELI KABISA ANONY WA HAPO JUU , HATA MIMI INANISHANGAZA WAANDISHI WA HABARI KAMA AKINA MICHUZI WANAJUAJE ZIARA BINAFSI ZA RAISI????????? MAANA HIZI HUWA HAZITANGAZWI KABLA. HII INAWEZA IKAWA NI NJIA YA PUBLICITY TUU.

    ReplyDelete
  29. watu mnaongelea kufahamiana na mdogo wake migiro, mara girlfriend wa mdogo wake, so what??? ndio mahali pa kujadiliana hayo? Andikianeni 'emails'. Mara, oh ni mpole sana, hana maringo nk. Inasaidia nini ktk public page kama hii. Kama binadamu anaweza asiwe na maringo kwako kwasababu zake Na wengine watakwambia ana maringo vilevile. Ongeleeni vitu vya kujenga, sio umbeya, alaaaaa!
    Kuna siku watu mtaanza kusimuliana hadithi za utotoni katika blog hii. Try to respect the blog. Labda Michuzi ndio anataka hadithi kama hizo. Za Juma na Roza! tehe-tehe..... Ndio nyie mkitaka kazi mtaanza kumwambia mtu, oh, nimesoma darasa moja na mdogo wako boss, ana tabia safi sana, na alikuwa wa kwanza darasani kila mara. Hadi mtachemsha, sababu yeye atajua si kweli.
    mwelimishaji.

    ReplyDelete
  30. MWANAHAMISI INSELEKEA KWELI UNAIJUA HIYO FAMILIA YA KINA MCHUKA NA MIMI NAIJUA SANA NIMEISHI NAO ILALA SHARIFF SHAMBA NA NI WATU WANGU WA KARIBU SANA.
    UNAMZUNGUMZIA IRENE NI HUYU IRENE MABIBA? NI MIAKA MINGI SANA SIJAMUONA NILISIKIA TU KAOLEWA NA MTOTO WA MKUBWA. NI MSICHANA MZURI SANA NILISOMA NAE MSIMBAZI MSETO PRIMARY SCHOOL

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...