kule sitokihomu kuna duka linaitwa duka...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. hata hapa Malmo(lund) lipo hilo... big up kiswahili

    ReplyDelete
  2. Mi nadhani yanamilikiwa na mshtahiki Nyupi,halafu lipo zaidi ya moja pale stockholm.

    ReplyDelete
  3. Michuzi, Michuzi, wacha kukonskripti maneno ya lugha za nhi nyingine kuwa ya Kiswahili kwa sababu yanaandikwa kialfabeti sawa na maneno ya Kiswahili, na kuwafanya wengine wafikirie kuwa Kiswahili kinapamba moto duniani!

    Maneno mengi ya Kijapani (yakiandikwa kwa herufi za alfabeti) yanafanana sana na maneno fulani ya Kiswahili Je, Wajapani wamekopa maneno ya Kiswahili?

    Utakuwa ni ufinyu wa kutoelewa etymology endapo kila mara tutaamua kwa kuwa neno lafanana na neno fulani la Kiswahili, kwa hiyo, neno hilo ni la Kiswahili!

    Neno “duka” (kama lilivyo kwenye duka la mjini Stockholm na katika miji mingi ya Swedeni), ingawa lafanana na neno la Kiswahili, pengine, haina maana kuwa ni la Kiswahili.

    Labda ma-etymologists (wataalamu wa mianzo ya lugha) za Kiskandinavia na Kijerumani watusaidie. Kwa sababu, pengine, neno “duka” ni neno la Kiswideni, kama ukilinganisha na maneno haya yenye maana moja na “duka” katika lugha zifuatazo :

    dække (Kidenishi)
    dekken (Kidachi)
    decken Kijerumani)

    ReplyDelete
  4. kiswahili ni 60% kibantu then 40 inayobaki ni maneno ya lugha nyingine kana kiarabu,kihindi na nyinginezo

    ReplyDelete
  5. We born again pagan kweli ni pagan maana hata fikra zako ni za kipagan

    Mimi nilidhani unamaana ya neno duka huko uswidi, kumbe nawe ni longo longo tu. Sisi na michuzi tunachukulia kuwa ni neno la kiswahili mpaka uta kapo prove otherwise nyamafuu wee. Ndo nyie mnaokataa utamaduni wenu. Mtu akienda mjini babake akija mchafu mchafu anasema ni jirani yake, Alaaaa

    Tuambie kama una maana ya neno DUKA na sio kumwambia michuzi anawadanganya watu, si nawewe uaanzishe blogu yako ya kusema ukweli na ku research maana za maneno.

    Naomba kutoa hoja

    Asante

    ReplyDelete
  6. jamani neno "duka"ktika lugha hizo tatu ulizotaja hapo juu bwana Born again ni "doll" au mwanasesere kwa kiswahili,

    ReplyDelete
  7. DUKA hilo haina maana ya duka kwa kiswahili. DUKA wana maana duka(kwa kiswahili) la vyombo vilivyotengenezwa kwa kioo(glassware or crystals)

    ReplyDelete
  8. michuzi umesahau pia goteborg wana DUKA linaitwa DUKA,,well mi nimeshindwa kuencode huo mji,labda wewe...

    ReplyDelete
  9. Mrekebisha Tabia na Born Again Pagan, mna majina mazuri!!!!!!!!! Mmoja ni mrekebisha tabia...Ajabu ni nani kakupa uwezo huo? Mwingini ne mdini mlokoke.

    Anyway, ukimsoma vizuri Born Again Pagan anashauri tujihadhari sana kukurupia maneno yenye herufi za alfabeti za Kiswahili na ku-conclude kuwa ni ya Kiswahili.

    Katika lugha ya Kiswedeni, kuna neno "duka" lenye tafsiri ya Kiingereza "lay on the table". Tunaweza kutafsiri kwa Kiswahili kama "anika wazi" au "tandaza wazi" bila kuficha.

    Mtu kama wewe, Mrekebisha Tabia, ni sawa na wale wenye ufinyu wa kuelewa, kama Born Again Pagan alivyodokeza!

    Born Again Pagan katoa mjadala wa ki-intellectual. Wewe waleta mjadala wa mabarabarani na uliojaa matusi!

    Nikiwalinganisha wanyama wawili (skunk na paka), Mrekebisha tabia skunk na Born Again Pagan ni paka! Skunk anamtusi Paka kwa kuwa mchafu na mnukaji...Kumbe harufu inayotoka mkunduni mwa skunk...(ngoja niishie hapa!

    ReplyDelete
  10. Wewe, Mrekebisha Tabia, jirekebishe tabia yako ya kimatusi matusi. Maana ya neno duka kwa Kiswedeni ni DUKA (KWA KISWAHILI) la vyombo vya nyumbani. Otherwise, its meaning is a household accessory store!

    Kama unabisha waulize wenywe wakujibu.
    E-mail yao kundservice@duka.se

    ReplyDelete
  11. Jamani duka kwa kiswedish maana yake ni kuandaa meza. Hili duka linaitwa duka maana linauza vyombo vya nyumbani ila hamna maana yoyote ya kiswahili.
    Papaa J Lund Sweden

    ReplyDelete
  12. Ni kweli kabisa juu ya maana ya duka. Hata mie nilipoona miaka ya 90 nilienda moja kwa moja kwa Waswidi na kuwauliza maana nilishangaa na zaidi ya hapo kweli lilikuwa duka. Sasa hivi DUKA lipo nchi nyingii duniani na kampuni kubwa ingawa si sawa na IKEA, icar au wazee wa samaki ABBA ambao nasikia ilibidi watoe ruhusa kwa bendi ya ABBA kutummia hili jina. Waswidi hajambo?? .... Sikonge

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...