malkia wa taarabu aliepata mafunzo toka kwa malenga siti binti saadi, bi. kidude baraka, akiwasili ngome kongwe tayari kwa sauti za busara mwaka juzi.


nabandika insha hii fupi ya picha kumuenzi bi. kidude ambaye amepeperusha sana bendera ya bongo nje ya nchi kwa miongo kibao, na hadi sasa ambapo ana umri wa zaidi ya miaka 80 anaendeleza libeneke, ingawa nasikia afya yake safari hii kidogo inasumbuasumbua...
kesho tamasha la nnne la sauti za busara linazinduliwa rasmi na waziri wa habari, utamaduni na michezo mh. muhammad seif khatibu na zaidi ya vikundi 40 toka ndani na nje ya nchi vitatumbuiza wiki nzima hapo ngome kongwe.
filamu ya bi. kidude inatarajiwa kufungua dimba la tamasha hili ambalo linachangia kwa kiasi kikubwa biashara ya utalii visiwani na bongo nzima kwa ujumla.
tamasha hili litafungwa rasmi huko kendwa beach siku ya wapendanao kwa burudani ya usiku kucha katika kukazia ule usemi wa waandaaji wa 'hakuna kulalaaaaaaa!'
kiingilio ni bure kati ya saa 12 jioni hadi saa 2 usiku ambapo baada ya hapo inabidi utoe kitu kidogo. panapo majaaliwa nategemea kuwa huko wiki nzima hivyo stei tyuund...


kwa khabari zaidi bofya www.busaramusic.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. NAOMBA KUELIMISHWA HUYU NANI, MIE NIKO CANADA.
    NA NI KABILA GANI,:? MNYAMWEZI NINI, ANA SURA MBAYA HIYO.

    ReplyDelete
  2. Tuekee basi kavideo clip kidogo ka huyu malkia. Inaelekea watu wanafaidi sana. Sasa hata sauti au kitu kidogo. Kam vile ulivyotuwekea jiji la musoma sijui mwanza kule wakila samaki wasio na minofu vile basi nadhani unaelewa ninachoomabapoa basi


    natanguliza shukurani kwa yote unayotuwekea huku.....

    ReplyDelete
  3. Duh! Ila mbaya sio utani. Mbona hana viatu?

    ReplyDelete
  4. SELEBRITE WETU HAPO NDO KAPOZI ANAPITA KWENYE RED KAPETI TIHIII TEHEHEEEEE.... KEEP UP GOOD WORK BI KIDUDE...

    LOVE YAAA YIP YIP YIPPPPPPP HUREEEE

    ReplyDelete
  5. INASIKITISHA SANA KUMWONA HUYU BIBI YETU AKIWA KATIKA HALI HII. Hao wanao andaa hayo matamasha nafikiri wanaangalia kujaza mifuko yao na sioni kama watakuwa wa msaada sana kwa huyu bibi. Wakati kukiwa na function ndio wanatafuta hawa mabibi lakini baada ya hapo ni kwaheri. Utashangaa anachokifaidi kwenye hili tamasha/busara.

    ReplyDelete
  6. NYI MNAOSEMASEMA MAMBO YASIOELEWEKA! hivi nyie hamjui vibibi kama hivi shauri yenu kama hamjavimba midomo.

    ReplyDelete
  7. huyo anaitwa BI KIDUDE

    naona michuzi blog yako imejaa watindiga

    sasa fanya mipango kesho uposti picha ya SHAABAN ROBERT

    utaona watakavyo kuuuliza hivi ni nanii eeeh?

    ReplyDelete
  8. Nilipokuwa kijana nilipata kuwa na mpenzi wa Kiingereza mwenye asili ya Kiyahudi. Moja ya fasili alizonipa ambayo mpaka leo naikumbuka ni fasili ya neno la Kiingereza CUTE. Fasili yake iliyonipa: Cute means ugly but interesting!

    Bi Kidude anafanana na ile fasili aliyonipa mpenzi wangu wa ujanani!

    Masalaamia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...