MAMA HILDA FLORENCE MARUMA-WAKATI
1943-2007

MDAU MWENZETU MANDELA KENNETH DAVID WAKATI AMEFIWA NA MAMA YAKE MZAZI LEO. NA TUJUMUKIE NAYE KWENYE WAKATI HUU MGUMU WA MAJONZI. MIPANGO YA MAZISHI INAFANYIKA KWENYE MAKAZI YA FAMILIA PLOT 1073 MSASANI PENINSULA DAR ES SALAAM.



HESHIMA ZA MWISHO ZIMEPANGWA KUTOLEWA ALHAMISI TAREHE 22 FEBRUARI KUANZIA SAA TANO ASUBUHI. BAADA YA HAPO MWILI WA MAREHEMU UTAPELEKWA KANISA LA MTAKATIFU ALBAN KWA MAOMBEZI SAA NANE MCHANA, KABLA KUELEKEA KUPUMZISHWA MAKABURI YA KINONDONI

MUNGU AILAZE PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU MAMA YETU

AMIN
-------------------------------------------------------

With deepest sadness and heavy heart, we regret to announce the death of our beloved Hilda, which occurred on Monday the 19th of February, 2007. Funeral arrangements are being held at the family residence Plot 1073 Msasani Peninsula. Last respects will be held on Thursday the 22nd of February from 1100 hours. Thereafter the body will be taken to St. Alban’s Cathedral for funeral service at 1400 hours before being laid to rest at the Kinondoni Cemetery.
May our Almighty God rest her Soul in Eternal Peace
AMEN

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 20 mpaka sasa

  1. yeees bro kenneth, karibu kwenye maisha ya uyatima, I hope now utaelewa nini maana ya kuishi bila mama, nashauri tuanzishe chama chetu, amen!

    ReplyDelete
  2. Poleni sana kwa msiba huu mkubwa uliowafika. Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Mandela, mimi pamoja na kuwa mbali na nyumbani, lakini naungana na familia yako, wafiwa wote, pamoja na wale wote walioguswa na msiba huu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi. Mungu atawaongoza, atawapa nguvu, ujasiri na kuwapunguzia machungu. Siku zote tutamkumbuka mama yetu Hilda Wakati katika sala zetu. Mungu ailaze roho ya mama yetu mahali pema peponi - Amen

    ReplyDelete
  3. Poleni sana. Tunajiunga nanyi kuomboleza kifo cha mama.

    ReplyDelete
  4. Poleni sana wafiwa. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Marehemu alitoa mchango mkubwa sana katika maendeleo ya sisi vijana wakati akiwa UN information centre (UNIC)

    ReplyDelete
  5. Poleni sana - Mungu awape ujasiri wakati huu mgumu. Mumshukuru Mungu kwa kila jambo

    ReplyDelete
  6. Anon wa kwanza, sidhani kama una akili timamu. hili si jambo la kufurahia hata kidogo, kama mna ugomvi na David ni bora umtafute mmalizane, lkn kusema yeeees kubwa hapa inatupa picha mbaya sisi wengine.
    Wafiwa poleni, msijali maneno ya hawa manungayembe yasiyo na mioyo.

    ReplyDelete
  7. Poleni sana Mandela, Biko, Kuchi na familia nzima wa Mzee Wakati. R.I.P

    ReplyDelete
  8. Pole sana Mandela ,

    Tuko pamoja nanyi kwenye msiba huu mzito

    Jirani Zetu 72 - 78 oystebay

    Mshomi's

    ReplyDelete
  9. "Pumzika kwa amani mama"
    Baada ya hapo nina wasi2 na baadhi ya wadau. Mbona mnajifanya kuonyesha utu sana ktk msiba huu? Au kwa vile alikuwa matawi ya juu?
    Ww fadhili kiswahili gani tena hicho-eti kwa niaba yangu na ya familia yangu. Kwa niaba vp wkt ww ndiye uliandika?
    Kamala si fresh kwa namna ulivyokomenti.
    Nasign off.

    ReplyDelete
  10. Wewe JK KAMALA ni mpumbavu usiekuwa na mfano duniani,na nina hakika kabisa wewe uliokotwa jalalani,na umshukuru sana aliekuokota,maana ungekuwa umekufa kenge mwekundu wewe usie na wazazi.
    POLENI SANA WAFIWA...MWENYEZI MUNGU AWAPE UJASIRI.{samahani kaka michuzi ujumbe huu mfikishie huyo kenge alieongea taka}

    ReplyDelete
  11. Poleni sana ndugu zangu wafiwa, katika dunia hii sote twapita.. Mwenye Enzi Mungu awape mioyo ya ujasiri katika hiki kipindi kigumu cha msiba na amjaalie marehemu malipo yalio mema...Amen!

    ReplyDelete
  12. Pole Mandela na familia yote. Mungu awatie nguvu katika hili.

    ReplyDelete
  13. INNA LILLAH WAINNA ILLAH RAJIUNA,SISI SOTE NI WA MWENYEZI MUNGU NA KWAKE TUTAREJEA TUJIWEKE TAYARI MAANAHATUJUI SIKU WALA SAA.MUNGU AWATIE NGUVU WAFIWA WOTE KWANI KAZI YA MUNGU HAINA MAKOSA,TUISHI TUKIMTUMAINIA MUNGU KWANI YEYE TU NDIYE AJUE SIRI ZA MAISHA YETU.
    nyamsisi

    ReplyDelete
  14. Pole sana Ken nakuombea utiwe nguvu uweze kumudu hiyo khali ngumu iliyo mbele yako. Nina kukumbusha tu kwamba Mama yetu mpendwa ametutoka tukiwa bado tunamuhitaji ingawaje kipindi kimefika kama ujuavyo life expectancy yetu ni finyu sasa miaka 64 ni mingi mno. Pole Ken!!

    ReplyDelete
  15. Dear Ken and family. I am sorry for your loss. Mama will live on in the hearts of everyone who loved her. May God guide and give you strenght during these trying times. Be blessed.

    ReplyDelete
  16. poleni wafiwa, mungu atawapatia mama mwingina kwa sababu ndiye aliyemchukua bila izini yenu, au km vp mfuateni huko mume kubwa kwa nini anawaingilia na kumchukua mama yenu na kusababisha akina jlkamala kuawaita mayatima! kweli ilo ni jina la kumwita mtu ka nyie? mfuatine sagod ua hakujui kenneth nini?

    ReplyDelete
  17. MIJITU MINGINE SASA ANGALIA HILO LI RIWA HAPO NDIYO COMMENT GANI HIYO SASA KAMA HAUNA CHA KUSEMA KAA KIMYA SHENZI MKUBWA...

    ReplyDelete
  18. acheni kutumia majina ya watu kuweka comment sijui unapata nini halafu cha ajabu unajulikana i feel sorry unahasira na dunia

    ReplyDelete
  19. Bwana Kenneth Wakati,

    Msiba ni kitu cha huzuni sana katika maisha ya binadamu hapa duniani. Angalia mfano wa Yesu katika Biblia, alipoambiwa kuwa rafiki yake Lazaro (wa Biblia) amefariki, alilia sana kabla hajamfufua.

    Tunapokuwa na ndugu zetu tunatamani tungekuwa nao milele kwa kuwa tumeshawazoea, lakini Mungu aliyetuumba ana mipango tofauti na mawazo yetu. Kwa kuwa hakutuumba tuishi milele duniani bali mbinguni ndio maana muda unapofika ni lazima tuondoke.

    Najua kifo cha mama yetu imekuwa huzuni ya aina yake katika maisha yako lakini kumbuka jambo moja kuwa, Mungu aliyemuumba ndiye ndiye aliyeamua kuwa arudi katika makao yake ya milele, kwa hiyo basi shukuru kwa kila jambo kwa kuwa ndiyo mapenzi ya Mungu kwako.

    Mungu mwenyewe aliyeumba kifo akupe faraja kuu katika kipindi hiki kigumu cha msiba na majonzi, ukizingatia sisi wote ni wapitaji na wasafiri katika dunia hii.

    Mungu Akubariki na kukufariji.

    Amina.

    Julius KAM mganga
    CMSA
    22/2/2007

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...