dah! wadau acheni roho ya korosho. yaani hata kunisifia nilivyotoka na kanzu yangu. nikivaa viatu vya mchikichini, mashati ya mbowe, tai za samora na suti za jojiz grili mnaosha sana vinywa. hebu acheni hizo...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Kanzu gani hilo oversize kwako hilo.Mimi sikujua ni wewe Michuzi nilifikiri ni mja mzito wa Huko Dubai amevaa nguo la maternity wanalovaa wajawazito.Kumbe ni wewe Michuzi, Kaka Michuzi una vituko!Bado siamini kama ni wewe.

    ReplyDelete
  2. ha ha ha , umependeza na hiyo kanzu mazee. nadhani watu hawajatoa comment kwa sababu hawana uhakika ni chata gani. yawezekana ni nike, tommy au rocawear hiyoo ?... just kidding, hongera , nakutakia maisha mema .

    ReplyDelete
  3. Asante kwa kutuletea nyuuz za dumila, na kweli umependeza hiyo kanzu!!

    Michuzi, umetuonyesha maeneo ya ya biashara na kiutawala zaidi. hebu jaribu kutembelea manzese na buguruni za huko ili tuone maisha ya mwana-imarati wa kawaida yakoje maeneo ya pembezoni...! pamoja na shughuli zao za kiuchumi mf. mama-lishe, uchuuzi, chips-kuku, machinga, kilimo n.k.

    ReplyDelete
  4. Huko hakuna wana blog au wabongo? mbona hatuoni picha zao au wanakaa manzese na wewe unatembelea posta mpya ya huko? ukikutana nao tunaomba sura zao hata kama wanapiga box

    ReplyDelete
  5. Mashaalah kanzu nzuri lakini Rangi mwinyi wangu ni dizasta

    halafu nadhani unajua ni akina nani wanavaa kazi zenye mikono mifupi

    nenda kanunue kanzu rangi nyeupe yenye mikono mirefu

    mikono mifupi shekhe msikitini kwetu itabidi uswali peke yako yaani sala ya fardhi hatuwei kukubali

    ReplyDelete
  6. ustaadhi michu, utamu wa kanzu ni kuwa na kobazi na baraghashia!! vipi ulisahau kuulizia? pamoja na yote, umependeza mshkaji!!!

    ReplyDelete
  7. 1. Rangi rasmi ya kanzu ni ipi, hebu tusaidieni wale tusioelewa!

    2. onyesha picha za watu na maeneo ya watu wa kima cha chini, pamoja na shughuli zao; au wote huko dubai wameuchinja?

    ReplyDelete
  8. kweli kanzu imekupendeza,umekuwa kama shehe ubwabwa, sijui kama ulikumbuka japo ndizi.

    ReplyDelete
  9. mzee mwenyewe hiyo kanzu niya kulalia (pajama)tena unavaa kwa yenyewe wamanga, kweli ni kichekesho.

    ReplyDelete
  10. Sheikh wangu hilo kanzu ni la kulalia yakhe hawajakushangaa wamanga huko usinde nalo tena masjid ustaadh,kwa huku bongo poa tu lakini huko noma.

    ReplyDelete
  11. Hatuna usemi kwasababu tukisema tutaitwa wanga. Naona umependa hii rangi kweli mara tumeona picha ya kanzu rangi hii hii na mikono mirefu sasa tena naona hii na mikono mifupi.

    Ukweli umependeza ila sijui kanzu rangi zake ni zipi au kuna options? Mimi nataka kanzu ya pink

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...