Home
Unlabelled
moooooo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Kaka afadhali umeweka ng'ombe nitoe maoni kuhusu Rift Valley Fever,maana naona wewe na Popobawa tu!Ni hivi,Juzi waziri wa Mifugo,Mh Diallo ametangaza serikali imeleta dozi milioni 2 za chanjo ya ng'ombe kwa ajili ya ugonjwa huu.Binafsi namshangaa sana Mh na watendaji wake.Hivi,walikuwa wapi wakati ugonjwa uko Kenya,kuleta chanjo ili kuchanja ng'ombe wa maeneo ya mpakani,gonjwa lisiingie kwetu?Na hakika kama chanjo hii ingekuja wakati gonjwa liko kenya,sasa hivi walla tusingekuwa tunahangaika.Tazama,sasa ugonjwa uko Manyara,Arusha,Kilosa,Dodoma na kwingineko ambako habari hazifiki,ndipo Diallo anakumbuka kuleta chanjo milioni2?!!Idadi ya ng'ombe inakadiriwa kuwa milioni 16 nchi nzima,sasa chanjo milioni mbili ni kitu gani kwa 16 milioni?Utaisambaza vp sasa?cha ajabu waandishi wa habari hakuna hata anaekemea,wao wamekalia kutafuta watu wamefumaniwa basi,ndio habari kwao!Ikumbukwe kuwa huyu Diallo ndiye aliharibu wizara ya maji 2000 - 2005,akapewa Utalii 2005 - 06 akaharibu tena,sasa mifugo nako ndio hivyo tena.Lakini aah,kwa kuwa anakichangia machapisho chama tawala basi,atahamishwa wizara zote ziishe!Jamani,nchi hii hawa bongolala wanapewa wizara wa nini?
ReplyDeleteKiutaalam ugonjwa wa mifugo ukiingia sehemu hutakiwi kuchanja wanyama, walitakiwa wachanje wakati bado uko Kenya, na RVF sio ng'ombe tu bali hata mbuzi, kondoo, nguruwe, swala, nyati n.k
ReplyDeleteHongera Michuzi Nimeamini Tanzania ni nchi ya kidemokrasia kila kiumbe kina uhuru wa wa kutumia bara Awe Raisi,Tajiri,omba omba wa kigogo na hata ng`ombe ana uhuru wa kutanua apendavyo barabarani.
ReplyDeleteBush na Tony Blair ni vizuri wakaja kujifunza demokrasia hapa.Hasa ile ya matumizi ya barabara watashangaa!! kuwa kweli hii ni democratic country.