rais wa zanzibar mh. amani abeid karume akimpa hati na zawadi abeid amani karume kwa kuwa mmoja wa wadau wa zenj waliochangia katika maendeleo ya michezo na utamaduni ikiwa ni mojawapo ya shughuli za kumkumbuka muasisi wa mapinduzi ya zenj sheikh abeid amani karume ambaye ni baba wa mh. amani na babu wa abeid.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Hawa nao na majina yao wanaboa. Hivi hakuna majina majina mengine mpaka watue hayo tu.

    ReplyDelete
  2. majina ya unga hayo we unafikiri wakitumia mengine nani atawajua kuwa ni roya family of zanzibar. we angalia hata wanamuziki utasikia kalala junior, banana zoro badala zahir, na mengine mengi. Hapo anaandiliwa huyo kurithi kiti cha baba yake 2010. Kazi kwenu wazenji.

    Ila nafagilia sana ukoo wa Mwalimu JK.

    ReplyDelete
  3. ROYAL FAMILY

    ReplyDelete
  4. Is there something wrong with this picture?
    - Baba anampa mtoto zawadi kwa kusherekea kumbukumbu ya babu yake! They could have done this at the privacy of their home.

    ReplyDelete
  5. Kila mtu anastahili haki yake kati jamii kwa nafasi yake aliyonayo.
    Kwa mapenzi ya mwenyezi mungu Mzee Abeid Amani Karume alijaliwa kumpata mtoto wa kiume ambaye ni Amani Abeid Amani Karume. Nae halikadhalika kwa mapenzi ya mwenyezi mungu alijaaliwa kupata mtoto wa kiume ambaye ni Abeid Amani Abeid Amani Karume, hili halina ubishi hata kidogo.
    Sasa tuangalie nafasi zao katika jamii:
    Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume ndiye aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar baada ya kufuatia mapinduzi ya Jan.12 (Huyu ni Rais wa Kwanza ni Taasisi)
    Mh. Amani Abeid Karume ni Rais wa sasa wa Zanzibar (Naye kama Rais ni Taasisi)
    Bw. Abeid Amani Karume ni mwananchi wa kawaida wa Zanzibar anayeipenda nchi yake kikatiba hakatazwi kufanya jambo lolote lolote ilimradi havunji sheria za nchi. Kuchangia maendeleo ya jambo lolote ni wajibu kama mwananchi mwingine yeyote. Kwahiyo basi anastahili kupewa tuzo kama mwananchi wa kawaida.
    Mapenzi ya mungu yalikwisha timizwa na historia imekwisha andikwa.
    Ni haki yake kabisa kwa Abeid Karume kupewa tuzo kutoka kwa Rais wa nchi yake katika kumbukumbu ya Rais wa kwanza wa Zanzibar.

    ReplyDelete
  6. Unajua hata mimi haya majina yalinichanganya. Sikujua hapa ni baba na mtoto nilizania kuwa huyo abeid aman na aman abeid wote walisha kufa kwa hiyo huyo ndio mjukuu anapokea tunzo. Sikujua yeye ndio anatoa tena na kwa mwanae.....hayo majinaaaaa.....Twist and turn

    ReplyDelete
  7. Mmmmmmmmmmmh that's true!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...