
kipa wa simba john semainda akiokoa hatari langoni pake mbele ya beki omar choggo mluya a.k.a choggo chemba (kati) na mshambuliaji hatari wa cosmopolitan jumanne masimenti uwanja wa ilala a.k.a karume stedium.
leo nimeamua sio tu kuwaonjesha ya kale ambayo ni dhahabu bali pia kuwaambia mkae mkao wa kula kwani hivi sasa gazeti lako la daily news limeshakamilisha kuhifadhi kumbukumbu kama hizi katika mfumo wa teknolojia ya kisasa ya dijito na hivi sasa inaandaliwa maktaba ya online ili kuwawezesha wasomaji wapate vitu kama hivi kwa urahisi popote walipo.
namna ya mambo yatakavyokuwa na namna ya kuagiza picha ama makala za zamani itatangazwa hivi karibuni, hivyo kaeni mkao wa kula


jamaa walikuwa wameshiba haswa!! Duh!
ReplyDeleteMichuzi, mimi naomba picha tatu tu za kumbukumbu yangu ya Yanga na Simba, either 1980 or 1981, kutoka kwenye hizo archives.
ReplyDelete1. Zamoyoni Mogela, katoka nje kupata matibabu - picha inamuonyesha Chama kwenye touchline akimsubiri Mogela arudi.
2. Zamoyoni Mogela karudi uwanjani akiwa amefungwa bangage kuzunguka kichwa - picha inamuonyesha Mogela akicontrol ball na wachezaji watano wa Yanga (I think they were Charles Boniface, Ahmed Amasha, one of the Chamas, Juma Mkambi and Ishaka Hassan) wakiwa kama wanamuangalia kila move yake!
3. Ahmed Amasha anapewa kadi nyekundu baada ya kumvunja mguu yule beki mmoja wa CDA Dodoma (I want to say Charles Mgodo but I may be wrong)- picha inamuonyesha Amasha ameinamisha kichwa na refa kanyoosha mkono juu akiwa ameshika kadi nyekundu.
Memorable pictures for memorable times in Tanzanian football!!!
Amasha alimvunja mguu Yusuf Ambwene beki mahiri wa CDA ya dodoma nilikuwepo taifa sku hiyo
ReplyDeletehuyu jamaa jumanne hassan masumenti aliowa bonge la mtoto barabara ya nane dodoma aitwae sanura mohamed e bwana ee alikuwa anatesa mpirani na nyumbani pia !!!!
ReplyDelete