
huyu ndiye alhaj maneno tamba. amini usiamini yanki huyu ni mganga wa kienyeji na amejipatia sifa kubwa ndani na nje ya nchi kwa utaalamu wake wa mitishamba. anaspeshalaizi zaidi kwa upande wa kufukuza majini pamoja na kutibu watu kwa kutumia matunda na miti shamba. ukiwa na shida yoyote ile mtafute kupitia + 255 713 616 069


Michuzi acha kututangazia matapeli kama mganga akasomee udaktari Muhimbili.
ReplyDeleteMbona hayo macho hakujitibu hadi akaenda kutibiwa hospitali alikopatiwa miwani? A u ndio mganga hajigangi? Makubwa!
ReplyDeletejamani aisifuye mvua imemnyea, Hivi ninyi hanjiulizi kila siku mkiwasha computer cha kwanza kuangalia ni Blog ya Michuzi, Shauri yetu Kazi ya Tamba hiyo. teh teh teh, Mi ntamtafuta anifanye nisahau hii bloguu
ReplyDeletejamani waislamu mnafukuza majini ama mnayakarisha?
ReplyDeletemganga ana O haya mambo gani tena michuzi, analipia matangazo
ReplyDeleteMichuzi, majini ni nini?
ReplyDeleteMichuzi wewe ni kaka na heshima zako na wabongo wote tulioko ndani na nje ya nchi yetu tunakufagilia kwa asilimia kubwa. Iweje leo uanze kuwaintatein waganga wa kienyeji watu wana wakimbia wewe unawakaribisha. tena kibaya zaidi unaandika hadi namba ya simu ili watu wamtafute waanze biashara hizo haramu. Michuzi hacha hizo unamuhitaji YESU.
ReplyDeletebrother michu,
ReplyDeleteunashukuriwa sana tena sana kwa kuweka mganga huyu number yake ya simu nitamtafuta maana na shida kila leo nawangiwa na mke mwenza wangu, wifi zangu, wakwe zangu na huku ughaibuni sina mganga hospitalini hata ugonjwa wangu hawaujulikani hope nitapona kwa huyu mganga. shukran sana tena.
ukisha sema mambo ya kufukuza majini basi tena ni direct disqualification. Uganga na uchawi vikiwa separated afrika itajivunia traditional knowledge. Tatizo wachawi bwana mchwiiiiiiii mimi wananiudhi!!!!
ReplyDeleteWaganga hawa ndio wametuharibia dada zetu, Masista Doo siku hizi wana roga kinoma ukichanganya hawa waganga na movie za kinegeria vinawatia uchizi wadau ole wenu masista doo wanawatia kwenye chupa siku hizi kila kona wanaroga imagine hata mashindano ya Umiss wanarogana hii balaa hii, haya bwana Tamba we Tamba tuu
ReplyDeletehivi michuzi wanakulipa hao? naona mpaka unapotosha maadili kwa kututangazia utapeli, majini ndio nini?
ReplyDeleteMwambie atafute kazi ya maana aachane na wizi huo
Huyu Maneno mi namuamini sana. Aliweza kumsaidia rafiki yangu aliyeugua kwa muda mrefu n kujaribu kupata tiba katika hospitali kadhaa ndani na nje ya nchi ikiwemo Afrika ya Kusini na ikashindikana, ni Dr. Tamba ndiye aliyemsaidia tena kwa matunda na ushauri wa kawaida tu. Si busra kusema yeye ni tapeli wakati humjui. Ila cha kumshauri tu ni kwamba anaweza kuongeza ujuzi wake kwa kurudi shule.
ReplyDeleteIla tu nauliza hivi - Tamba huyu ana uhusiano wowote wa kifamilia na Sultani Tamba?
Naomba kuwasilisha!!!!
Mimi sina la kusema its the matter of choice na ni uamuzi wa mtu
ReplyDeletehuyo mjinga wa tarehe 18/05/2007 wa saa 11:31 ana akili kweli? sasa waislam wanahusu nini? mbona kuna wata wana udini sana hivyo huyo uhakika hakuna shule hapo mjinga mjinga tuu.
ReplyDeleteKutumia miti shamba si tatizo, kama anafahamu ni sahihi kabisa, kwani hata madawa mengi ya kisasa yanatoKana na mimea ya asili. Ila anapoanza mambo ya MAJINI, hapo ndio anaharibu.
ReplyDeletewote mlioandika vibaya kuhusu tamba kaeni chonjo atawajia wote kwa zamu zamu. Mi simo
ReplyDeleteteh teh teh! sokolo nimecheka sana comment yako. anyway, kwa upande wangu siwezi kuzungumzia sana kuhusu kufukuza majini kwa sababu sina ninachokifahamu kuhusu hilo. lakini, kama jamaa anatumia miti, mizizi, majani, matunda na kadhalika kutibu watu mi nadhani hakuna neno hapo after all karibuni dawa zote ulimwenguni zinatokana na herbs na ndio maana siku hizi kumekuwa na kasi ya walimwengu kutumia vitu asili na ndio maana tunashuhudia Colgate herbal, herbal Tea, herbal Dettol na kadhalika na kadhalika..........
ReplyDeletemganga na mchawi ni mtu na mdogo wake.Nakushauri uende kwa Yesu, kuna msaada wa kweli.Tamba mwenyewe anamhitaji Yesu
ReplyDeleteWALLAHI AKITUTATULIA SHIDA ZIFUATAZO BASI HESHIMA MBELE; 1. MGAO WA UMEME USIRUDI TENA, 2.WALA RUSHWA NCHINI, WABUNGE NA VIONGOZI WETU WAKINAI HUO ULAJI WANAOPATA, 3.WAUZA UNGA WAKOSE SOKO, 4.KUSIWEPO NA MSONGAMANO WA MAGARI MJINI, 4.MADAKTARI NA WAUGUZI WAWE NA ROHO YA HURUMA, 6.WANAFUNZI SHULE YA MSINGI MPAKA CHUO KIKUU WASOME KWA GHARAMA NAFUU, 7.RVF, TAUNI, MAFUA YA NDEGE NA KIPINDU PINDU VISIRUDI TENA, 8.ANAYETAKA KUKUAMBUKIZA UKIMWI MAKUSUDI, MW'UME 'CHECHE YAKE' ISISIMAME, AU MW'MKE 'UKE' WAKE UZIBE, 9.ATAYECHUKUA MKE WA MTU POPOBAWA AWE HALALI YAKE, 10.HAYO YOTE NILOYATAJA NA AHADI ZAKE ZIWE KWELI!!!!
ReplyDeleteAnon wa 11:31:00 pm naona umejaa CHUKI,CHUKI,CHUKI,CHUKII,HASIRA,HASIRA na waislamu.Uislamu unaingiaje hapa? Waislamu wanahusikaje? Hivi mbona wana wakimajadili mzee Richmonduli, Mrahamba,Chengee,Mkaahapa, Zero na rushwa zao ukristo hautajwi?
ReplyDeleteNenda kwa Tamba ukawaone wateja wake,hutaamini.Wengi wanaenda rozari wamezificha ndani ya nguo zao.
Kweli best yangu Michuzi kuna wakati unachemsha mpaka una-bore, nini sasa kutuletea waganga wa kienyeji globuni, watu wengine huwa wanafanya mambo haya kwa siri kubwa sasa mwenzangu unaonyesha umefanikiwa sana mambo yako kwa kupia huyo mganga wako ndio maana unataka tufuate nyayo zako, utawakamata wajinga ila mimi simo. Yaani nimeku-undergrade kichizi nilikuona bonge la muangaikaji na umefanikiwa kwa kuangaika. KUMBE UNAMGANGA WAKO? Pu@3#%vu
ReplyDeleteAcheni mambo ya dini hapa hatutaki kila mtu ana yake na tuheshimu dini za wengine.
ReplyDeleteAcheni ushamba nie, kuna tofauti ya mganga anaye tibi kwa miti shamba. mchawi anaye amini kwamba anaweza kuroga mtu na mganga anaye kufanya uaamini kwamba anaweza kukupa super natural powers!
Hao wawili wa mwisho ni imani tu hamna lolote!
Kutibu kwa miti shamba ni ujuzi wa mizizi au majani gani yana tibu ugonjwa gani ambao kwa kawaida mtu hujifunza kutoka kwa mababu.....
Kwani madawa ya hospital yanatengenezwa na raw materials gani? fanyeni uchunguzi pigmies wanaishi potini kwa madawa ya miti shamba na wana afya kuliko mimi na wewe. Madawa ya kisasa ya mejaa side effects.
Kueleza mengi hapa hapatoshi lkn kama Tamba anatibu kwa miti shamba na afanikiwa kuna ubaya gani? Hata majini labda kuna majani/mizizi ile harufu inafukuza. Chaguo lako.
Anon hapo juu hata kama unamwamini Yesu ukiungua si unakwenda hospital? Msichanganye mambo jamani.
Waridi
wewe Michuzi acha hizo za kuwaweka waganga wa kienyeji ktk blog hata kama ni yako. Unasema amespecialize kutoa majini. majini ni nini? au yeye ndiye baba lao hao majini. mimi nilikuwa nakuheshimu sana. sasa naona umenogewa pesa na unaanza kutuonyesha ulikoanzia.
ReplyDeleteSir ISSA…SAANECHA ANAIMBA…MZEE WA BUSAARA HOO…. “..KWA KUSAFIRI SAFIRI NA UNGO MPAKA UBUNGO..”, MCHANA HAONeKANI LAKINI USIKU DOO…!!!!! HII SOO…!!!! LAKINI JANA USIKU TULICHANJWA CHALE SITA TUKASEMA NANI KAPITAA..???…RASHIDI MLANGO KAFUNGA, SASA KAPITAPITAJE....?? KWENYE KUTA KWENYE NYUFA ...???… SHEMEJI AKILEWA KILASIKU ANAPIGWA KABARI…. AU TUAMINI KULALA NA MIFUPA YA NGURUWE NA GANJA…ILI .”.TUOKOKE..” MAISHA HAYA..??? NA TENA MAJIRANI “….WANAHISI HUYU BWANA MWANGA…”.. MZEE WA BUSAARA HOO ….samahani…Bongo flava idumu.
ReplyDeleteCan he make my Dick long and larger?... i heard that, africans folks can do that.
ReplyDelete/Andersson