na huu ujumbe umeletwa mchana huu na mdau mmoja hivi...
Michuzi,
Blog yako iko juu mzee. Labda mwenyewe hujui tu.Angalia takwimu zako katika Alexa http://www.alexa.com/data/details/traffic_details?url=http%3A%2F%2Fissamichuzi.blogspot.com
Yaani blog yako inatembelewa na zaidi ya nusu ya watumiaji wa mtandao walioko nchini Tanzania, na karibu na watanzania wote walioko nje ya nchi. Kuhusu takwimu za watumiaji internet Tanzania wanakadiriwa kufika 330,000 (cheki hapa http://www.internetworldstats.com/stats1.htm)
Hongera sana Michuzi,
umekuwa Mzee wa Mafanikio na changamoto kwa wajisiriamali kama mimi.
//Dar Millionaire

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 19, 2007

    Alexa.com inasema watumiaji wengi wako UK, wakati extremetracking wanasema ni wabeba box wa USA. Dar Mill, sema nani mkweli

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 19, 2007

    Hongera Michuzi,
    sasa anza kuweka advataizas upate malipo ya kazi yako.
    Kip it ap!

    ReplyDelete
  3. AnonymousMay 19, 2007

    Congratulations, I have seen it, that's a milestone. Keep it up Mazee.

    ReplyDelete
  4. AnonymousMay 19, 2007

    U GO MICHUZIIIIIIIIII

    ReplyDelete
  5. AnonymousMay 19, 2007

    Michuzi hii blog inasambaa kama virusi vya UKIMWI bwana. Yaani ukiipata tu imekuganda

    ReplyDelete
  6. Hongera sana Michuzi!!!
    Hapa lazima tusheherekee. Kaza buti wengine tufuate nyayo!
    /maggid

    ReplyDelete
  7. AnonymousMay 20, 2007

    Hi Michuzi, Hongera sana mzee. Swali langu kwako ni kwamba unafanya juhudi gani ili hata siku ukiumwa(Mungu aepushie mbali) bado hii glob iwe hewani? Tafuta wasaidizi, sababu watu wameshakuwa addicted na glob yako. Naifungua after every 2 hours, na huwa sijilaumu. OC-Sinza, Dsm

    ReplyDelete
  8. AnonymousMay 20, 2007

    Hongera Michuzi, lakini bado sana. Nimetazama huko huko alexa.com na wenzako wako mbali. Wewe umepewa nafasi ya 1,264,5946134, DarHotWire wapo ya 267,075 duniani, nafasi ya 243 Tanzania na ya 230,410 huko kwa Bush. Bongo5.com wapo ya 264,266 duniani, ya 51 Tanzania na ya 67,239 kwa Bush. Kaza buti na utawafikia!

    ReplyDelete
  9. AnonymousMay 20, 2007

    Hope haimaanishi watu wale wale wamekuwa wakiiangalia blogspot yako over and over again kama ninavyofanya mimi !
    That means the figure wont be anywhere near the one unayojipigia kifua hapa !
    Abdul

    ReplyDelete
  10. AnonymousMay 20, 2007

    Anon wa Saturday, May 19, 2007 6:21:00 PM, ni kweli takwimu za Alexa.com zina walakini:

    Moja - zinakusanywa toka kwa watumiaji wenye Alexa toolbar, na ambao wana Internet Explorer na Mozilla Firefox.

    Pili - Alexa.com inaonesha blog ya Michuzi ilikuwa online toka 22-Jun-1999, wakati ukweli ni kuwa post ya kwanza kabisa kwenye hii blog ni tarehe 08-Sept-2005. May be data zimechanganywa na data za blogspot.com kwa sababu michuzi yuko chini ya hiyo domain.

    Pili Alexa.com inaonesha 3-month avg ya blog ni 1,264,534 wakati counter ya chini ya michuzi inaonesha hii ni namba ya toka blog ianzishwe. (kama utakumbuka kuna 1M + ambayo ilifutika wakati fulani, kwa jumlisha na 265,000 + ya sasa)

    Kwa upande mwingine sijajua extremetracking.com wanakusanya vipi data zao. Kwenye site yao hawaelezi. Nimewatumia e-mail wafafanue, ila kama unafahamu naomba unielimishe.

    Kwa sasa napendekeza:

    Moja - kwa ajili ya kumjenga michuzi kila mtu aweke Alexa toolbar ili kumpaisha michuzi kila unapofungua blog yake, kwa sababu data za Alexa ndio makadirio pekee yanayopatikana kwa umma wote wa watumiaji wa internet.

    Pili - Michuzi nakuomba uongee na mtaalamu wako wa website atupatie takwimu halisi. Ukiwasiliana na wenye domain ya blogspot.com pia wanaweza kukupatia takwimu halisi pia. Ni muhimu sana kufahamu thamani halisi ya blog yako.

    //Dar Millionaire

    ReplyDelete
  11. AnonymousMay 22, 2007

    Michuzi unafanya kazi nzuri unastahili ongera sana kaka.

    Ushauri wa Dar Millionaire ni mzuri wa watumiaji wa Blog hii ya michuzi kuweka Alex tools but ungeweza kufafanua jinsi yakuweza kuweka hiyo kwani sio wote wataalamu ya haya mambo ili tumwakilishe mwenzetu. TUPO PAMOJA

    ReplyDelete
  12. AnonymousMay 23, 2007

    Ndugu Anon wa Tuesday, May 22, 2007 12:14:00 PM.

    Alexa toolbar inapatikana kwa link hii:

    http://client.alexa.com/install/AlexaInstaller.exe

    (copy hiyo link, paste kwenye address bar ya brower yako, kisha piga enter)

    Ukishadownload install kama program yoyote.

    Bila shaka haya maelezo yanatosheleza.

    //Dar Millionaire

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...