na huu ujumbe umeletwa mchana huu na mdau mmoja hivi...
Michuzi,
Blog yako iko juu mzee. Labda mwenyewe hujui tu.Angalia takwimu zako katika Alexa http://www.alexa.com/data/details/traffic_details?url=http%3A%2F%2Fissamichuzi.blogspot.com
Yaani blog yako inatembelewa na zaidi ya nusu ya watumiaji wa mtandao walioko nchini Tanzania, na karibu na watanzania wote walioko nje ya nchi. Kuhusu takwimu za watumiaji internet Tanzania wanakadiriwa kufika 330,000 (cheki hapa http://www.internetworldstats.com/stats1.htm)
Hongera sana Michuzi,
umekuwa Mzee wa Mafanikio na changamoto kwa wajisiriamali kama mimi.
//Dar Millionaire


Alexa.com inasema watumiaji wengi wako UK, wakati extremetracking wanasema ni wabeba box wa USA. Dar Mill, sema nani mkweli
ReplyDeleteHongera Michuzi,
ReplyDeletesasa anza kuweka advataizas upate malipo ya kazi yako.
Kip it ap!
Congratulations, I have seen it, that's a milestone. Keep it up Mazee.
ReplyDeleteU GO MICHUZIIIIIIIIII
ReplyDeleteMichuzi hii blog inasambaa kama virusi vya UKIMWI bwana. Yaani ukiipata tu imekuganda
ReplyDeleteHongera sana Michuzi!!!
ReplyDeleteHapa lazima tusheherekee. Kaza buti wengine tufuate nyayo!
/maggid
Hi Michuzi, Hongera sana mzee. Swali langu kwako ni kwamba unafanya juhudi gani ili hata siku ukiumwa(Mungu aepushie mbali) bado hii glob iwe hewani? Tafuta wasaidizi, sababu watu wameshakuwa addicted na glob yako. Naifungua after every 2 hours, na huwa sijilaumu. OC-Sinza, Dsm
ReplyDeleteHongera Michuzi, lakini bado sana. Nimetazama huko huko alexa.com na wenzako wako mbali. Wewe umepewa nafasi ya 1,264,5946134, DarHotWire wapo ya 267,075 duniani, nafasi ya 243 Tanzania na ya 230,410 huko kwa Bush. Bongo5.com wapo ya 264,266 duniani, ya 51 Tanzania na ya 67,239 kwa Bush. Kaza buti na utawafikia!
ReplyDeleteHope haimaanishi watu wale wale wamekuwa wakiiangalia blogspot yako over and over again kama ninavyofanya mimi !
ReplyDeleteThat means the figure wont be anywhere near the one unayojipigia kifua hapa !
Abdul
Anon wa Saturday, May 19, 2007 6:21:00 PM, ni kweli takwimu za Alexa.com zina walakini:
ReplyDeleteMoja - zinakusanywa toka kwa watumiaji wenye Alexa toolbar, na ambao wana Internet Explorer na Mozilla Firefox.
Pili - Alexa.com inaonesha blog ya Michuzi ilikuwa online toka 22-Jun-1999, wakati ukweli ni kuwa post ya kwanza kabisa kwenye hii blog ni tarehe 08-Sept-2005. May be data zimechanganywa na data za blogspot.com kwa sababu michuzi yuko chini ya hiyo domain.
Pili Alexa.com inaonesha 3-month avg ya blog ni 1,264,534 wakati counter ya chini ya michuzi inaonesha hii ni namba ya toka blog ianzishwe. (kama utakumbuka kuna 1M + ambayo ilifutika wakati fulani, kwa jumlisha na 265,000 + ya sasa)
Kwa upande mwingine sijajua extremetracking.com wanakusanya vipi data zao. Kwenye site yao hawaelezi. Nimewatumia e-mail wafafanue, ila kama unafahamu naomba unielimishe.
Kwa sasa napendekeza:
Moja - kwa ajili ya kumjenga michuzi kila mtu aweke Alexa toolbar ili kumpaisha michuzi kila unapofungua blog yake, kwa sababu data za Alexa ndio makadirio pekee yanayopatikana kwa umma wote wa watumiaji wa internet.
Pili - Michuzi nakuomba uongee na mtaalamu wako wa website atupatie takwimu halisi. Ukiwasiliana na wenye domain ya blogspot.com pia wanaweza kukupatia takwimu halisi pia. Ni muhimu sana kufahamu thamani halisi ya blog yako.
//Dar Millionaire
Michuzi unafanya kazi nzuri unastahili ongera sana kaka.
ReplyDeleteUshauri wa Dar Millionaire ni mzuri wa watumiaji wa Blog hii ya michuzi kuweka Alex tools but ungeweza kufafanua jinsi yakuweza kuweka hiyo kwani sio wote wataalamu ya haya mambo ili tumwakilishe mwenzetu. TUPO PAMOJA
Ndugu Anon wa Tuesday, May 22, 2007 12:14:00 PM.
ReplyDeleteAlexa toolbar inapatikana kwa link hii:
http://client.alexa.com/install/AlexaInstaller.exe
(copy hiyo link, paste kwenye address bar ya brower yako, kisha piga enter)
Ukishadownload install kama program yoyote.
Bila shaka haya maelezo yanatosheleza.
//Dar Millionaire