Home
Unlabelled
dawa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Hapo lazima jamaa wa secury wawe karibu, au wasikilize muziki wote ikinyamaza tu wanaangilia kunani, vinginevyo mtaji huo.
ReplyDeleteUlaji huo jama!! subiri wajuzi waikombe... :-) steved.
ReplyDeleteMvua za mafuriko zikipita hapo sijui tena ndio mziki umeisha. Au usiku wanaliingiza ndani na kulitoa nje asubuhi?
ReplyDeleteJamani bongo tuweni creative. Kwanza hapo ni njiani mtu akiumia nalo hivi watamlipa? au watamdai kwa kuharibu spiker lao.
Mbao mbili tu kidogo na kuliweka hapo juu hata hai cost hela nyingi.
We like easy and simple things.
Ni tabia mbaya sana. Inaonyesha jinsi Tanzania ilivyo nyuma. Sheria za hati miliki (Ikiwemo ya Tanzania the Copyright and Neighbouring rights Acts of 1999) inakataza public performance bila kuwalipa wahusika REASONABLY.
ReplyDeleteNiliwahi kufuatilia radio na Tv owners wanasemaje juu ya hilo wakasema wako tayari kuacha kupiga muziki wa watanzania kama watalazimishwa na COSOTA kuwalipa mrahaba wasanii. Naona kidogo wameanza kujirekebisha ila bado haitoshi. No free music these days my friend.
Bado mnawacheka wasanii wetu, mnalinganisha magari yao na ya matajiri wa US. Heshimuni haki miliki zao muone kama nao hawatanunua hayo ma mazda.
Lingeweka hapa mbona tungetajirika. Ningejiangusha kwenye hilo speaker halafu na sue...hapo ulaji mkubwa tu. Changamkieni vijana wala hamna ya kuliiba hili maji kidogo jiangushe halafu unasema umeumia mgongo...big money kwsho watajifunza kuliweka juu ya sehemu ya watu kupita...
ReplyDeleteAu itabidi waiwekee alarm, maana bila hivyo watu watazoa...wewe subiri, mtasikia kwenye ippmedia kuwa spika ya posta imeibiwa.. hata hivyo wakiweka alarm itabidi wasiweke mziki wowote ule unaofanana na mlio wa hiyo alarm, maana wajeuri watapigia timing tu pia huo mlio!! he he, steved.
ReplyDeletelazima kuna watu wanailia mingo hiyo spika
ReplyDeleteHili taifa letu sijui linakwenda wapi. Kampuni, taasisi au shirika likitaka kujitangaza kitu cha kwanza kuingia akilini ni kuchukua maspika na kupiga kelele. Well and good. Mimi naona hizo kelele zinaarifu wachache lakini zaidi ni burudani kwa wale wasio na kazi (idlers and lumpens) na vilevile ni kero kwa watu wenye kazi haswa za kutumia akili. Bila kuwasahau wagonjwa, wazee, watoto wachanga, wanafunzi wanaojisomea, n.k. Hivi hawa wanaotupigia kelele wanajua kwamba kelele ni aina ya pollution? Kwamba ni sawa na air pollution an environmental pollution za aina nyingine? Nadhani society at large haijui kwasababu the obsession na kelele hapa bongo is overwhelming.
ReplyDeleteKwa mfano, ninapokaa kule Kimara Baruti 770 kuna jamaa amefungua bar katikati ya makazi ya watu (yawezekana amepewa na leseni kabisa) na mara mbili kwa wiki kuna mkesha wa disco ambapo muziki unapigwa kwa sauti ya juu sana kuanzia saa 12 alasiri mpaka saa 11 alfajiri kesho yake. Japo nyumba yangu ina umbali wa mita 500 toka hii bar, muziki unapopigwa nashindwa kulala hata nikimeza dawa za usingizi. Sasa sijui nyumba ya pili ni vipi. Na hii hali inajirudia sehemu nyingi sana za Bongo. Sababu hawa wapiga kelele hawakemewi na majirani inanifanya niamini either wamezungukwa na watu waoga sana au hawa majirani ni idlers and lumpens hivyo wanafurahia hayo makelele. Pia kuna makundi ya dini yanayotumia maspika kupiga kelele na hata makampuni yanayozunguka Bongo nzima na malori yaliyopakia maspika huku yakipiga kelele.
Cha ajabu ni kwamba kuna sheria inayolinda wananchi dhidi ya noise pollution. Kwanini haitekelezwi? NEMC mpo? Jamii inayopiga makelele ovyo ifikiriweje? Are we serious? Haya makelele yanatuendeleza au ndo yanatudumaza akili na afya? Naomba mtu aninong'oneze majibu.
Bado tukidhania kwamba ni kitu kizuri lakini what about things like usumbufu wa kelele kwa watu wengine,wenzetu wana sheria ambayo hairuhusu sauti kubwa kwenye public places.
ReplyDeleteHuu ni ukosefu wa ubunifu,sasa maspika yanapiga kelele ni usumbufu mtupu. Hivi hawajui kuwa kuna speaker za ndani unaweka juu na zinakuwa na sauti ndogo ukiingia unapata mziki mwanana sio kufungulia speakers kubwa hivi na kusumbua mtaa mzima na business zingine. Kazi kweli kweli Bongo
ReplyDeleteWanalipa music royalties kweli hao?
ReplyDeletehawasumbui biashara zingine na sauti ya music wao?
Waweke Music wao ndani tu kwa wateja wao. Watu wa nje hawa stahili kusumbuliwa kabisa.
Hivi wasipoambiwa mapema je kila mtu akijiamulia kuweka lispeaker lake nje kweli hapo mjini patapitika?
naona watu mnakandia bure maendeleo ya bongo, vitu hivi hata london vipo kama mtu anabisha mwambie aende mitaa ya wood green maduka yote yana spika nje.halafu katika kumbukumbu zangu sehemu hiyo ilkuwa machangu doa wavizia watu kukaba.
ReplyDeletewanaokandi hawaishi london...london ya wabongo wanayoishi ni kama kariakoo...working class people ongelea ile london ya kule ukipita tu unashashanga kwenye majumba na hotel zaoa mara polise anakuuliza umepotea? unataka msaada nikupeleke wa kuonywesha unakoenda? bwana wangu sutasahau hiyo siku....
ReplyDeleteJama huko ni Woodgreen, siyo CanaryWharf au KnightsBrigde, je, posta mpya ki hadhi ni kama pahali gani? Tusilinganishe mahali jama,bali tulinganishe hadhi! SteveD.
ReplyDelete