mahandaki yanarudi tena dar taratibu kufuatia jamaa wanaotandika mabomba mapya ya maji safi na maji taka kutotengeneza kwa lami pale walipofukua. cheki shangingi la mh. jaji linavyosota kupita handaki hilo. yaani zali hili la kudhi lipo karibu kila barabara jijini - dc wa ilala mh. tsere na wenzio wah. ma-dc wa temeke na kinondoni mpoooo???

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 05, 2007

    Tatizo letu Watanzania Hatuna utamaduni wa kujali na matengenezo .Hii sehemu ikiwahi kutengenezwa haitakuwa tatizo kubwa wala kughalimu pesa nyingi lakini hapo kinachosubiliwa mpaka Rais au Waziri Mkuu apite na aseme kwamba kumeharibika hivyo mawaziri na wakurugenzi wote watashinda hapo kusimamia matengenezo.Hivi jamani hata matengenezo madogo mpaka viongozi wa juu waseme !!! nadhani wengine mkowapi jamaniiii

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 05, 2007

    Kwa utamaduni wetu hapo tunamngoja JK au waziri mkuu apite na wawaambie watendaji wao kuwa kumeharibika na kunahitaji matengenezo kwani hapo ni karibu sana na ofisi ya waziri mwenye dhamana ya Barabara lakini aoni hilo shimo mpaka wapite wakuu wake.Jamani tubadilike jamani tusingoje kuambiwa vitu vidogovidogo tujitume jamani!!!!DUU Hivi Rais wetu atafanya mangapi ikiwa hata madogo mnashindwa kumsaidia.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 05, 2007

    that car goes with that pit hole.We should all buy such cars.ahahahhhhh

    Michu umetupa swali na jibu.Tutanunua na sie M/Mungu akipenda.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 05, 2007

    Bongo kungekuwa na sheria ya ku-sue kama mtoni naona ingekuwa fundisho kwa hao mawaziri. Judge ni mtu mwenye wadhifa sana, kama ndio atakuwa anapitishwa mtaani taratibu hivi ni hatari kutokana na kazi zao. Tushukuru Mungu tu kuna Amani nchini vinginevyo ni hatari sana. Inabidi hao mawaziri/wakuu wa wilaya/IGP/ waamgalie hilo....

    ReplyDelete
  5. What a stress!!Mtu unanunua gari bei mbaya,lipia kodi hapa na pale na bado unalidhuru gari hilo kwa kulipitisha barabara kama hii?
    Sasa hao wahusika wanafanya nini hasa masaa 8 waliyoko kazini?Au inabidi Rais au makamu wake atake kupita ndo pafanyiwe ukarabati?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...