juu mkurugenzi wa idara ya muungano katika ofisi ya makamu wa rais mh. anitha ngowi (samahani, sio swai kama nilotaja kwa makosa awali) akielezea kazi ya idara hiyo kwenye banda la idara ambamo pia kuna nyaraka, picha na maandiko ya kumbukunbu ya muungano wa tanganyika na zanziba kama hizo picha zinavyoonesha. ya kati ni wah. wakisherehekea kutiwa saini kwa makubaliano ya muungano na chini ni toleo la tanganyika standard la aprili 27, 1964 siku moja kabla ya wino wa muungano kumwagwa na mwalimu nyerere na hayati sheikh abeid karume. hii ni katika uzinduzi wa wiki ya utumishi wa umma ambapo idara za serikali na taasisi zake zinafanya maonesho kuonesha shguhuli zao

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 18, 2007

    Serikali ya awamu ya nne bwana? kuanzia mwenyewe,mawaziri,wabunge mpaka madiwani asilimia 75% ni vijana na wanamvuto sijui utendaji.halafu hiyo picha ya chini kama walikuwa wanacheza mduara vile? na aliyekuwa mbele ya mwalimu lazima katokea visiwani

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 18, 2007

    EEh Huyu mdada ameisha kuwa mheshimiwa, hongera sana!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 18, 2007

    Michuzi huyo Dada anaitwa ANITHA NGOWI sio SWAI au Mary Ngowi, sio swai.
    Namjua huyo nimesoma nae. Labda kama siku hizi kaolewa na Mr. Swai kwa hiyo ni Mrs. Swai.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 18, 2007

    Michuzi can you come again!huyo dada naelewa anaitwa Anita Ngowi na siyo Swai kama nami sijakosea.Please would correct or comment otherwise.Yeye ni Mkurugenzi wa muungano,alitokea wizara iliyokuwapo awamu ya Mkapa na ni mke wa mwanasheria mmoja maarufu hapi Tanzania.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 18, 2007

    Tusaidiene lugha hivi hilo bunge lilioindinisha muungano lilikuwa la wasenge? Maana naona gazeti la Standard liliopigwa picha hapo limeandika NATIONAL ASSEMBLY GOES GAY.Mnaojua lugha mtusaidie.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 18, 2007

    NATIONAL ASSEMBLY GOES GAY. The three-hour debate during the emergence sitting of the tanganyika national assembly on saturday night was the liveliest since the country became independent.
    Members were in ....(Michuzi re-take small fonts).
    nadhani walichangia sheria na kukubaliana watu wanaruhusiwa kuwa wasenge (true until small text are retaken by michuzi)

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 18, 2007

    utabaki hivyo hivyo ulisoma nae ulisoma nae wewe unafanya nini mkurugenzi wa kulea wabibi ughaibuni

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 18, 2007

    picha zote zina wajihi wake, lakini mimi picha iliyonifurahisha ni hii ya huyo dada anaefanya mahojiano, kweli kazi ya uandishi wa habari bongo ngumu, huyo dada anaonekana kajichokea!! na shati lake kubwa kuliko mwenyewe!! limepauka kwa jua kali, kashikilia Mic yake kweli anatia huruma,sijui kama amekula au ndio anawahi kukimbiza story, uandishi mgumu nyumbani jamani, Michuzi unasemaje! ukipata muda anzisha mjadala juu ya hali za kiuchumi za waandishi

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 18, 2007

    Michuzi tafadhali tupatie majina ya hao wanaoonekana kwenye picha ya kusherehekea muungano. Najua akiyeko nyuma ya Mwalimu ni mzee Kawawa, nyuma ya kawawa ni Boke Munanka kama sijakosea, na wengine ni akina nani?

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 18, 2007

    Anon. wa June 18, 12:12: PM EAT, naungana nawe, hata mie sielewi.
    mmhhh umeniuwa, nimecheka hadi mbavu zinauma. Unajua nilikuwa sijashtukia.
    Hivi kweli "NATIONAL ASSEMBLY GOES GAY" Jamani tusaidieni wenye kujua lugha what does it mean. Unajua sisi kiingereza kimetupiga chenga wengine wajameni. Msaada wa bure plizz

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 18, 2007

    Neno gay lina maana zaidi ya moja na maana iliyotumika katika kichwa cha habari katika Tanganyika Standard ni ile hali ya kuwa katika hali ya furaha, bashasha na nderemo (jovial, glad, joyous, happy, cheerful n.k.)na si ile maana ingine ya usenge.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 18, 2007

    gay means a homosexual person, especially a man.sijui kwenye magazine walikua wana maana gani

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 18, 2007

    Hakuna maana nyingine mbali na ile aliyotoa Anonymous wa June 18, 2007 6:57:00 PM EAT!

    Wenye kuunganisha na usenge, yafaa sana etymology (the study of the history of words) ni limi lilianza, kutoka wapi, na jinsi maana yake inavyobadilika.

    Matumizi ya neno gay kuwa usenge (kwa Kiswahili) ni ya siku hizi!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 18, 2007

    Maana iliyotumikahapo siyo ya usenge kumbuka wakati huo usenge ulikuwa taboo karibia dunia nzima. Muandishi alikuwa na maana ifuatayo:

    gay: happily excited, MERRY, keenly alive and exuberant, having or inducing high spirits.

    However, this is one of those controversial words, I would't use it...I would find another word.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 18, 2007

    Huyo dada anitwa Anitha ngowi, amekulia ilala shariffu shamba jirani kabisa na chuo cha dsj. Sasa hivi anakaa mikocheni anajumba la kifahari

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 18, 2007

    Hongera na pole Mkurugenzi, kazi yako ni ngumu sana.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 18, 2007

    hicho kijamaa mbele ya nyerere kimekenua kimefurahi kishenzi, cheki ka kawawa tumbo kubwa

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 19, 2007

    Mnaochanganywa na neno GAY ni kwamba Gay ina maana kama tano hivi sasa nafikiri ilikuwa ni maana ya pili kati ya hizi

    GAY:
    1. homosexual: homosexual in
    sexual orientation

    2. merry: full of light-
    heartedness and merriment
    (dated)

    3. bright in color: brightly
    colored (dated)

    4. carefree: having or showing a
    carefree spirit (dated)

    5. debauched: leading a debauched
    or dissolute life (dated)

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 19, 2007

    Dictionary said... kama ulivyoandika.

    Hiyo kamusi ni ya mwaka gani?

    Wakati Tanganyika Standard linakipa kicha cha habari kama hiyo, neno "gay" lilikuwa halina maana ya usenge!!!!!!!!!!!!!!

    Lilikuwa na maana ya "hali ya kuwa katika hali ya furaha, bashasha na nderemo (jovial, glad, joyous, happy, cheerful n.k.)", kama alivyosema anonymous hapo juu na wengineo.

    Don't conscript hali ya wakati ule kukubali hali ya leo.

    Let us be not only be educated but educatable!

    Anayebisha, aulize Waingereza wenyewe au wataalamu wa etymology, kama alivyoshauri Fanya Utafiti Ujue hapo juu.

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 19, 2007

    NAKUBALIANA NA MDAU ALIYESEMA KUHUSU MATUMIZI YA HIVI KARIBUNI NENO "GAY".
    HILI NENO KUANZA KUTUMIWA KWA KUMAANISHA WASENGE NI HIVI KARIBUNI,HATA UKIANGALIA KAMUSI MBALIMBALI.
    WASENGE WAKIKUULIZA "ARE YOU HAPPY OR STRAIGHT " ? WANAKUWA WAMEKUTEGA KWANI NENO HAPPY LINAUHUSIANO NA NENO GAY KWA KUMAANISHA FURAHA,BASHASHA.KWA JIBU LA HARAKA NA LINALOPENDEZA KINYWANI NI KUSEMA HAPPY......SASA UKISEMA HAPPY UNAKUWA UMEMTAARIFU MUULIZA SWALI KUWA WEWE NI MSENGE.UKISEMA STRAIGHT UNA MAANA UHUSIANO WAKO NI WA MWANAUME & MWANAMKE NA SIO DUME KWA DUME AU JIKE KWA JIKE.
    HATA KWENYE ILE PARADE KUBWA HAPA USA.....SLOGAN YA WASENGE UTASIKIA WAKISEMA "HAPPY PRIDE".MWANZO WA JUNE WALI- WARM UP PALE NATIONAL MALL, NJE YA CAPITOL HILL(MABUNGE YA MAREKANI) NA WIKIEND YA MWISHO JUNE NI NYC(5TH AVENUE FROM 59 ST. TO GREENWICH VILLAGE).
    KUHITIMISHA, NENO GAY LILIVYOTUMIKA KWENYE MUUNGANO HALIKUMANISHA WASENGE HATA KIDOGO.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 19, 2007

    Mheshimiwa ISSA..NAONA WAHESHIMIWA WAMEPANGA STARI WANA SHANGILIA..KUNAJAMAA KAKENUA VIZURI TU.."..MAMBO YALIKUWA YAKIENDA YAKIONGEZEKA.."..

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 19, 2007

    Katika kuipokea Timu ya Taifa yetu katika Bunge na kwa Dar kurindima kwa shangwe, tungetafsiri kama wakati huo wa Tanganyika Standard kuwa "Bunge and Dar Go Gay"!

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 19, 2007

    Jamani computer ina kazi nyingi sio tu kutype na kuprint hili neno utaweza lipata kama unatumia "MICROSOFT WORKS WORD PROCESSOR".

    gay

    gay [gay]
    adj (comparative gay·er, superlative gay·est)

    1. homosexual: homosexual in sexual orientation

    2. merry: full of light-heartedness and merriment (dated)

    3. bright in color: brightly colored (dated)

    4. carefree: having or showing a carefree spirit (dated)

    5. debauched: leading a debauched or dissolute life (dated)


    n (plural gays)
    homosexual person: a homosexual, especially a homosexual man


    [13th century. From Old French gai “happy,” of uncertain origin: probably from Frankish .]


    -gay·ness, n
    Encarta ® World English Dictionary © & (P) 1998-2004 Microsoft Corporation. All rights reserved.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 21, 2007

    Kwa nini nyie watu hamtaki kukubali kuwa neno gay lilitumiwa na Tanganyika Standard katika masafa ya yale ya zamani "happy" ndani ya kurindima? Akili zenu finyu, nini?

    Lakini siku hizi limebatizwa na maana nyingine ya usenge!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...