Home
Unlabelled
mzumbe
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Sisi wa Ilboru Secondary, tulikuwa tayari kuwa wa mwisho kwenye matokeo ya f4 au f6 lakini wa mwisho kabisa kabisa awe Mzumbe secondary. Na kwa kweli mchuano ulikuwa mkali na mpaka sasa hawa madogo wa Mzumbe hawatuwezi kabisa. Ilboru Juu, Mzumbe chini chini kabisa.
ReplyDeleteNyangusi Ndukai
THE SILENT STALKER says.....Damn!!! kumbe mbaya hivi.....msianze kuchonga sana, hata mimi nilikua selected kujiunga hapo A'level ila nikachomoa nikabaki BONGO. Kweli kama hapa ndio they say its kitivo cha maGenius wakibongo GOVT shud beta than this
ReplyDeleteMabweni ya Shaaban Robert haya njia ya kwenda IDM. Mkwawa 2 daima 1998-2000
ReplyDeleteDuh kumbe chama la Mzumbe limechoka namna hii ? Ndio maana jamaa walikuwa wakija town wana mambo ya kishamba shamba!
ReplyDeleteHaya akina Jerome Rugumyamghetho, Brian,James,Jarome,George Mgomella, mwaiona skuli yenu, wenyewe mlikuwa wajanja 1996.
ReplyDeletedu ebwana eeeh,si kitoto,nakumbushawa mbali kinoma yan!du hili skuli limetulea kinoma ndugu zangu! ijapokuwa limekaa kiana tu si unajua ili mradi buku linatembea kwenye njia yake watu tunalizika tu, big up mzumbe,for sure mzumbe is fantastic
ReplyDeleteNimesoma Mzumbe, nimekaa Mkwawa #5---nikaenda Ilboru (class of 93) nilikaa Tololwa (Biafra). huyo anaesema Mumbe ni mbaya, anafananisha na wapi? mbaya kimasomo, kimajengo au----angekuwa amesoma sehemu kama Mzumbe kauli finyu isiojitosheleza kama hiyo asinge toa.
ReplyDeleteJamani mnamkumbuka mzee TDK Msuka, N'darlu,Kidua,Bitwale,Minja,Mganda(sasa hivi ni top govt officila hiko Rwanda)Msabila,Minja,bila ya kumsahau marehemu Mkombothi(Wibo), na wengine wengi.
ReplyDeleteRemember Mzumbe guys:
"DETERMINATION IS OUR MOTTO"
Acheni kutuyeyusha nyie Mzumbe walikuwa wachovu tu kazi ilikuwa ni kupewa Maswali ya practicals za physics, chemistry na Biology ili kulinda heshima, Mzumbe wangekuwa wazuri wangekuwa wanaongoza hata Advanced mathematics ambayo Ilboru walikuwa wanaongoza miaka yote au mnaniambiaje vijana wa Kiringo na Akyoo. Hawa vijana wa mzumbe wasiwababaishe hao walikuwa ni watoto wa kubebwa, Wakati nyie mabaniwa na Shembilu na Msungu wenzsenu Mzumbe walikuwa wanapeteshwa tu, Mkitaka kuhakikisha angalia siku hizi Mzumbe wanavyochemsha
ReplyDeleteWewe mimi nimekaa mirambo namba 2, 1995-1997. Hiyo shule unaiona imechoka lakini madenti wa hapa tulikuwa tunaishi kama tupo peponi. Hapo unoko ni ziro, roll call ya jioni mara moja kwa wiki, jumapili tuu. Siku ya usafi wa mazingira mara moja kwa wiki, na hakuna ma-unoko mengine ya kifalafala hapo. Hapo ni buku tuu, pigia mstari usawa wa meno.
ReplyDeleteHivi kwa mrina bado kupo? Na wewe uliyewataja hao kina J-rugu mbona hujawataja vichaa wengine? Mkombachepa, sangusangu, alipembe, omari kinyonyoke, mwisongo, antena, kayandabila wekabia, na wengineo?
mimi nashangaa ni lini Ilboru wameipita mzumbe ktk advanced results?wewe anony wa 1 acha kuongea uwongo ulowazi,mzumbe ni vichwa na hilo litabki hivyo
ReplyDeleteBaada ya kutambiana A'Level kwa kupewa "mitutu" ya practical ili msiharibu jina na reputation ya shule zenu za Ilboru na Mzumbe Sasa hamieni UDSM ni wapi kati ya mzumbe na Ilboru waliongoza kwa kupata "First Class" University of Dar es Salaam???, Hakuna jibu hapo eee, Kule hakuna "mitutu" na u geneous wenu wengi pale ndio mwisho wa Reli na point tatu na nne zenu.
ReplyDeleteMzumbe na Ilboru kweli kulikuwa na 0.01% ya mageneous lakini the rest ni "VILAZA" tu mkifika pale UDSM.
Kwa mtazamo wangu, ilboru wanaweza kushindana na kuwagalagaza mzumbe kwa upande wa O'level. Ukija kwenye A'level, mzumbe ni ya kwanza na hakuna wa pili. Ilboru na wengine wanafuata nyuma kabisa huko.
ReplyDeleteNa wewe uliyezungumzia kuwa walboru na wazumbe kuwa hawaonyeshi uzuri wa vichwa vyao UDSM, kama umesoma UDSM, kuelewa mambo siyo silaha nzuri ya kufaulu vizuri ingawa pia inasaidia. UDSM kuna "unique techniques" za kumfaulisha mtu.
lazima annon hapo juu hukusoma UDSM. vitu ulivyoandika havina ukweli kabisa. kwa mfano kitivo kimojo tu cha sayansi mwaka 2003. kulikuwa na first class sita na tano kati ya hizo zimetoka mzumbe na ilboru tu. sasa hivi ni kweli shule hizo hazifanyi vizuri kwa sababu zimeshafutwa special school. sasa hivi wanakwenda watu wenye vichwa vibovu kama wewe. lazima asome tution kumi na apewe pepa ili uweze kupata division three.
ReplyDeleteKama UDSM kuna "unique techiniques"
ReplyDeletena nyinyi wa Ilboru na Mzumbe si mpo "unique" sasa inakuwaje hapo
Mwanangu hapo tumekumbushana mbali sana. Tulikuwepo hapo first Batch ya special school enzi hizo za mkuu Msuka. S/Robert 5 yalikuwa makazi. SHULE YETU MZUMBE SEKONDARI, YASIFIKA POTE....................... WAZUMBE MALIZIENI BASI.
ReplyDeleteKwa kweli Mzumbe kimandhali imechoka kinoma.sasa achilia mbali ile era ya 1995-7 ambapo chakula tena ikawa mgogoro...ngama (ugali)wa shangazi mbaya..tepu(maji ya bomba), malaria na Typhoid..nakumbuka kuna muda ilibidi tuwahi kufunga na tuchelewe kufungua.Lakini kitu kizuri ilikuwa manual work zilikuwa sio sana and after 2pm school is over so you have lots of time za kugwaduka kama Ligwa.Siku ya vilei (kilakala wakija disco) hadi sangusangu alikuwa ananyoa, wali unapikwa, parfume za yolanda na yu zinajitokeza. Ki shule sio kwamba tulikuwa na walimu wa kutisha saana lakini competition ilikwa juu in between students.Nawakumbuka all time teachers kama Wibo (RIP) he was dedicate teacher, Kabale (style yake ya kufundisha was unique) nzuri saana kwa kujiandaa na mikiki mikiki ya UD. Namkubuka Ibra jengo kwa uongozi wake wa mirambo...shule ilitujenga kwa kweli.Lakini mazingira mabaya.
ReplyDelete