wadau naomba kufahamishwa asili ya neno 'ndafu'

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 25 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 10, 2007

    Ndafu inatumika kwa wanyama tu... na dafu inatumika kwa mimea.. samaki wanatumia... ooh ngoja nikumbuke......nafu!!. he he

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 10, 2007

    watu wa animal rights wako wapi? huu ni udhalilishaji wa wanyama.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 11, 2007

    Baada ya jamaa huko Sudan kuozeshwa mbuzi, hata hamu ya hiyo ndafu mimi sasa sina... Halafu nasikia huyo mbuzi mauti ilimpata baada ya kula mifuko kadhaa ya rambo!! Sitanii ndugu soma hapa: Mbuzi Mke Kafa!! soma pia hapa: Mbuzi Kaolewa!! SteveD.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 11, 2007

    Hivi kwenye kamusi ya kihehe hakuna neno ndafu kweli, hebu wasiliana na mjengwa.

    Ila ninavyojua neno ndafu linatokana na kabila moja hivi kama si wahehe sijui.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 11, 2007

    Ndafu neno la kichagga hilo

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 11, 2007

    Acha ushamba wako wa kutuletea mambo ya animal rights hapa we umeambiwa utoe maoni yako ya neno ndafu na siyo kujifanya umestaarabika sana na kukosoa utamaduni wako, we ulitaka uwekewe Keki ya kizungu ndiyo ungeridhika.
    WATU WENGINE WANAKERA...!!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 11, 2007

    Kweli kabisa Anon wa 1:03 EAT, Haina maana ya kuanza kukosoana badala ya kueleza maana ya ndafu yaani nakuunga mkono kabisa WATU WENGINE BWANA!!.

    Ndafu ni neno la kihehe

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 11, 2007

    NDAFU ni neno ambalo limetoka huko uchagani,kuna wakati hapo zamani kidogo ali alikwa mzungu kwenye harusi moja ya kichaga,na walikuwa wameandaa mbuzi kama ndafu.lakini walikua hawana jina la hiyo kitu.sasa mzungu akaonja nyama ya ile mbuzi na katika ku appreciate hiyo nyama ilivyopikwa kwa ufundi mzungu akasema
    "WONDERFUL" sasa ndugu zangu wachaga walivyosikia hivyo wakabakia na ndafu..ndafu..ndafu.....ndio hilo jina likapatikana.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 11, 2007

    hapo kitambo, wazungu walistaajabu kule uchaggani kuona mbuzi akifanywa namna hii.
    kutokana na mshangao huo, wakasema "this is very wonderful."
    kutokana na kuendelea kulirudia rudia neno "wonderful"
    wachagaa nao wakaondokea kulipenda liinglishi hilo. nao wakatamani kutamka kwa kiinglishi. wakaishia kusema "ndafu" wakiamini ndilo jina la mnyama huyo akiwa hivyo kwa lugha ya kikristo.
    nimemaliza mkuu!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 11, 2007

    Michuzi

    Asili ya neno "ndafu" ni Kilimanjaro kwa wachagga. Na ukitaka kuingia ndani zaidi ni kutoka mitaa ya old moshi.

    Stori yenyewe inakwenda hivi, wakati wamisionari walikwenda kumjulia hali Mangi wa Old Moshi ambaye alikuwa mhasimu na mangi Sina, Mangi wa Old Moshi aliwaandalia karama nono hawa wamisionari ili wamsaidie kumwangamiza Sina, na wakati walipofika walikuta mlo mzuri wa mbuzi wa kuchoma. Baada ya kula walisema "It is wonderful" basi wakibosho kwa kushindwa kushika maneno yote wakaishia kusema "ndafu"

    Hii stori ni sawa na ile ya "Kibo show" ambayo imekuwa Kibosho.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 11, 2007

    anon wa June 11, 2007 8:01:00 AM EAT, hebu tupe hiyo stori ya "Kibo Show" mie siijui

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 11, 2007

    neno ndafu limetokana na wandaful....

    spiking of wachagga watuni watu hawa wanaamini, maisha ni matamu kama nyama ya mbuzi, na maisha ni magumu kama mfupa wa mbuzi, ila wachaga hawa hawa wanahaha na maisha na kutafuta pesa kwa njia yoyote kwakuwa wamesahau kuwa maisha ni mafupi kama mkia wa mbuzi. tehe tehe

    mimi ni msambaa

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 11, 2007

    Nina shangaa ambavyo watu wote mmemiss the name!! Mimi mHehe na neno hilo ndafu ni la kichaga likimaanisha "yule mbuzi aliyehasiwa" yaani "nortured" kwa kizungu. Nimesahau kwa kiHehe anaitwa nini - matokeo ya kukulia mjini. Sasa huyu ndafu hawezi "panda" au "kufanya matusi" kwa hiyo hazain na jinsi hii anamarinate tuu tayari kwa mlo!!Na kwa waHehe zile nanihii ("marupu" au "balls" kwa kizungu, "p***u" kwa kiswahili)pamoja na mapafu na moyo ni haki ya wale waliochinja na kumtayarisha mbuzi yule - ifiryo ya vavina!!!!

    Kwa wale wataalamu wa kiChaga mbuzi dume tu aliyehasiwa ndiye anaitwa ndafu au ana hadhi ya kuwa ndafu - jike daima haliitwi ndafu! Hakuna cha wonderful wala nini - ndafu walikuwepo tangu kabla ya kufika wamisionari na wazungu!!!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 11, 2007

    Anony 5.01 asante kwa maelezo yako lakini ni "neuter" or "spray"

    Na huyo msambaa teh teh teh ndio maana hamuendelei teh teh teh kwa kutupiana voodoo kila siku teh teh teh na kuogopa kufanya lolote la maana kila siku ohhh life is too short teh teh teh You are the only person on earth who can use your ability. You were born to win, but to be a winner, you must plan to win, prepare to win, and expect to win. teh teh teh I think life is too short to blend in. teh teh teh

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 11, 2007

    nyie watu hebu acheni ujinga, yaani nyie mngekuwa mnachunwa na kuanikwa hivyo mngefurahi? Lazima tutetee animal rights pia. Ni udhalilishaji tu hakuna cha Ndafu wala ndufa. Ndio maana siku hizi huoni hizo ndafu kwenye harusi. Zamani pia ndafu hakuna harusi, ila kwa kuwa watu wameanza kuelewa animal rights ndio maana unaona keki tu siku hizi kwenye maharusi. Acheni kutesa wanyama.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 11, 2007

    Naona tunarudia ndafu za MBUZI. Bora maana keki zinaozesha meno.

    ReplyDelete
  17. AnonymousJune 11, 2007

    Anonymous unatoka wapi wewe, sio mtanzania au umeloea hata hujawahi kurudi nyumbani. Animal right hukohuko huku watu wanakufa kama kuku tuanze kuangalia animal rights. Tupe human rights kwanza. Au hujaonja ndafu bei mbaya huko? rudi basi.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJune 12, 2007

    Wee msambaa gani koko nini au mnyika teh teh ndio nini. Sema ufundishwe hambuze.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJune 12, 2007

    kwanza wachanga sio wtani wa wasambaa...kama unatupenda utwambie lakini siye wala hatuwataniiiiii tuache

    ReplyDelete
  20. AnonymousJune 12, 2007

    DONT GET ME WRONG. HIVI HUYU MBUZI (NDAFU) AMECHINJWA KIHALALI KWELI AU AMENYONGWAAAAAA.
    HATA AWE AMENONA VIPI KAMA HAJACHINJWA NA KUTENGANISHA KATI YA KICHWA NA KIWILIWILI, SITII MKONO WANGU HAPO HATA KAMA NINGEKUWA MI NDIYE BWANA HARUSIII.
    SIYO SABABU YA UDINI AU NINI. LAKINI HATA MILA ZA MABABU ZETU, WALIKUWA WAKICHINJA. NINI BABU ZETU, ENZI ZA MAWE, JAMAA WALICHINJA KWA KUTUMIA VISU VYAO MAALUM VILIVYOTENGEZWA KWA MITI AU MAWE.
    MWENYE HOJAAA....... SILI KIBUDU

    ReplyDelete
  21. AnonymousJune 13, 2007

    nyie hebu acheni kudhalilisha wanyama. Inatakiwa muwe vegitarians manake nyama sio nzuri kwa maumbile ya binadamu. Animal rights lazima ziangaliwe, watetezi wa wanyama tupo. Hata sisi walala hoi hutufanyi mambo hivi, tunakula mchicha ama sukuma wiki mambo yanapita. Sasa nyie kuanika mnyama namna hii ndio nini?

    ReplyDelete
  22. AnonymousJune 13, 2007

    Sir ISSA NAONA..KURA NA WASEE..MBUSI HIYO BWANA...PICHA SAFI SANA HII MIMI NAPENDA SANA MBUZI..SASA HUYU WALICHINJA SHINGO AU..MAMBO YAENDA YAKIONGEZEKA..???

    ReplyDelete
  23. AnonymousJune 13, 2007

    Nyie mnaosema animal rights mnaishi nchi gani? Labda hamtembei au hamsocialize na watu wengine but TZ only.

    Kila siku harusi za wataliano kuna nguruwe mzima kawekwa mezani. Na ni hapa USA na hamna anayelia animal rights. Halafu huyuo ni nguruwe...hebu angalia yale mafuta na all that...

    Wewe huli nyama ...??? !!!! Kumbuka hata majani yana uhai...

    Kama wewe umeanza kuwa fashion vegan waachie wenzako wale wanachopenda ...??? Anything in moderation will not kill you..

    ReplyDelete
  24. AnonymousJune 14, 2007

    Ndafu imetokea uchagani wakuu, tuache ligi.

    ReplyDelete
  25. AnonymousJune 14, 2007

    Animal right hukohuko ambako mifugo ni paka na mbwa huku kwetu sisi rights zao ziko mzani tu.Hiyo ni art ya kichaga

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...