
mke wa waziri mkuu mama regina lowassa akifurahia zawadi ya kofia aliyotunukiwa alipowasili viwanja vya ukumbi wa karimjee holi jana kuzindua video ya shughuli za kupiga vita ukimwi za wanafunzi wa shule ya wasichana ya kifungilo kupitia klabu yao ya 'pasha' (prevention and awareness of hiv/aids in schools) ambapo pia ilifanyika harambee ya kutunisha mfuko wa klabu hiyo. mpango 'pasha' ni mradi ulioanzishwa na wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi ulioanzishwa mwaka 2004 kwenye shule za sekondari ambapo mkoa wa tanga uliteuliwa kuongoza mradi huu kitaifa. mpango wa pasha unahusika na kutoa ushauri nasaha kwa vijana walio mashuleni na kutoa elimu ya kujikinga na ngoma pamwe na magonjwa ya zinaa na stadi za maisha ambapo kifungilo ni shule iliyofanikiwa sana katika mpango pasha
I hope hizo kofia zimetengenezwa Tanzania na viwanda vyetu. Kwa vile kama zimeagizwa kutoka nje mbona nitasikitika?
ReplyDelete