


wadau wa ujerumani walisherehekea jana ushindi wa staaz pamoja na sherehe kubwa ya harusi ya Watanzania wawili walioamua kuupa kisogo ukapera.Hawa ni Bi Jasintha na bw. john bosco harusi hiyo iliyofana sana ilifanyika katika mji wa gelsenkirchen. juu ni maharusi hao, ikifuatiwa na wadau wa kutoka mjini wa augsburg, karibu na Munich. toka shoto ni malumbo s. malumbo, othman ukindo na mc wa shughuli hiyo aboubakar mwana wa liongo wa redio DWelle mjini Bonn. chini ni kinadada wa maua. nyepesi nyepesi ni kwamba idadi ya wabongo inazidi kuongezeka ujerumani.
michuzi hamna coment kweli mpaka saa izi? au unabana? kumbe tz tuna saloon nzuri kama majuu ni hivi?
ReplyDeleteinapendeza sana kuona wadau wanaubgana!!
ReplyDeleteWamependeza.. isipokuwa wangefunguia harusi yao bongo ndio wangependeza zaidi. Ebwana harusi za bongo siku hizi sio mchezo!!!
ReplyDeleteJamani kwa wabongo ambao wako Ujerumani tuwasiliane basi jamani. Hata mimi niko Ujerumani.Niko Saxony
ReplyDeleteJohn Bosco? huyu bwana anafanana mno na John Bosco niliyemaliza naye darasa la saba mwaka 1974 pale shule ya msingi Mfaranyaki, Songea. sijui ndiye?
ReplyDeletepoint of information,MC siku hizi anaitwa 'msherekeshaji',mpo hapo wadau?
ReplyDeleteMnawaonea wivu wamependeza sana na Harusi ilifana sana. Ulaya ni Ulaya tu hata kama hamna Saloon nzuri.wanameremeta.watu walikunywa na kula maanjumati mpaka wameacha
ReplyDeletearusi bab kubwa, sema gym ni muhimu
ReplyDeleteHivi huyo wa pili kutoka kulia siyo UMBE huyo?
ReplyDeletemumu aina gani??
ReplyDelete