mrisho mpoto si tu mghani mashairi mashuhuri nchini bali pia yeye na maabara ya utamaduni ya parapanda ni wacheza ngoma na sanaa za jukwaani waliotukuka na ambao hawachoki kuendeleza libeneke. kwa habazi zao zaidi bofya hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 11, 2007

    Jamaa huyu ndite aliyetoa ile ngonjera ya "Salamu zangu Kwako" kwa staili ya muziki jamaa yupo juu namkubali katika fasihi.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 12, 2007

    aisee huyu jamaa kwa mashairi namkubali niliwahi kuwa naye kikundi kimoja cha sanaa wakati tukiwa watoto pale BASATA mimi nikaingia kwenye fani zingine lakini naona mrisho akabaki kwenye sanaa, safi sana kwakweli unafanya vizuri mno kwenye hii fani hongera kaka!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 12, 2007

    Tatizo la Wasanii wetu ni "kungonoka" kwa saaana... au kwa lugha nyingine "Kupigana MRUNDA..." ivo wee waangalie hao wadada walivyo vaa kanga moja na shanga kwa wingi...kisha baada ya shoo...KUKANDAMIZANA...

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 12, 2007

    Huyu bwana na mwenzie Mnyenyelwa wana vipaji vya hali ya juu. Sauti na mbwembwe zake vinaweza kutumika kupeleka ujumbe wowote na mahali popote bila ya kuchusha wasikilizaji. Namwomba amfundishe mtu mwingine mambo muhimu katika kugani.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 13, 2007

    Binafsi namkubali sana Mpoto kama MWANASANAA mahiri hapa Tanzania.
    ni mfano dhahiri wa mwanasanaa mwenye elimu ya sanaa. wanasanaa wengi huchukulia sanaa kama kipaji na kuishia hapo. MPOTO, Mgunga, Richard Ndunguru, Dr Nyoni ni baadhi ya wanasanaa ambao wameenda hatua moja zaidi na kuongeza ujuzi na maarifa ktk vipaji vyao.

    huyu mpoto nimemkubali zaidi ktk huu wimbo wake wa salamu kwa mjomba, mashairi yake yamesimama na ujumbe upo very clear.

    na kuna mwanasanaa mwingine ambae pia namkubali ni dada Irene Sanga. sasa hivi anatamba na wimbo wake wa UTANDAWAZI.

    inasikitisha sana sasa hivi matapeli na vibaka kuitwa 'wasanii'. ndio maana ktk maoni yangu nimetumia neno wanasanaa. ni jitahada binafsi ktk kutofautisha pumba na mchele. poleni wanasanaa lakini mna nafasi ya kuwa chachu ya kuondoa fikra hizi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...