SWALI: BENDERA YA TAIFA INA RANGI NGAPI, ZITAJE MOJA MOJA NA ELEZA MAANA YAKE.

MASHARTI:
1. WABONGO WOTE NDANI NA NJE YA NCHI RUKSA KUSHIRIKI
2. ANONYMOUS ATAKUWA AMEJIDISKUALIFAI MWENYEWE, JINA LINAHITAJIKA
3. USILETE UFUNDI, JIBU SWALI KAMA LILIVYO
4. ENDAPO WASHINDI WATAKUWA ZAIDI YA WATATU TOMBOLA ITACHEZESHWA KUPATA WASHINDI WATATU - WA KWANZA, WA PILI NA WATATU
5. UAMUZI WA MAJAJI NI WA MWISHO, HAMNA KUKATA RUFAA
6. MSTARI MFU NI JUMAMOSI HII IJAYO SAA SITA MCHANA SAA ZA BONGO
7. MSHINDI ATATANGAZWA JUMATATU
ZAWADI;
1. PICHA YOYOTE MSHINDI ATAYOTAKA
2. ZAWADI INAPENDEZA IKIBANDIKWA BLOGUNI, KAMA MWENYEWE HATAKI ATATUMIWA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 28 mpaka sasa

  1. Bendera ya Taifa ina Rangi NNE zifuatazo na maana ya rangi mbele ya rangi:
    KIJANI- Ardhi
    DHAHABU-Madini
    NYEUSI-Watu
    BLUU-Bahari na Maziwa.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 11, 2007

    Rangi nne
    Kijani = misitu yetu
    manjano= madini yetu
    nyeusi = sisi wenyewe raia wa nchi
    blue = maziwa na bahari zetu

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 11, 2007

    MICHUZI NAONA SASA UMEANZA KUTUZARAU. HILO SWALI NI LA WATOTO WA CHEKECHEA.WEBSITE YAKO INA SOMWA SANA NA WATU WALIO SOMA NA WANA MADARAKA NA HAYO ULIYO ULIZA WANA YAJUA SANA.PLEASE MICHU, TUHESHIMU KIDOGO.
    NDAGA FIJO.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 11, 2007

    Bendera ya Taifa ina rangi Nne,Nazo ni:
    1.Nyeusi -Watu(ambao ni sisi watanzania au raia wa nchi hii ambayo ni moja ya nchi barani mwetu Afrika)
    2.Manjano- Madini(Utajiri wetu wa Madini)
    3.Blue- Bahari(Maziwa,mito na bahari)
    4.kijani-Ardhi(misitu na uanda wa asili)

    ReplyDelete
  5. 1. BAHARI 2. MADINI 3.WATU 4.ARDHI

    ReplyDelete
  6. 1.bluu ni bahari,mito na maziwa 2.njano ni madini 3.nyeusi ni watu 4.kijani. ni ardhi,

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 12, 2007

    rangi za bendera ya taifa~
    1 nyeusi-wanachi wa tanzania
    2.kijani-uoto wa asili ,ardhi
    3.njano-madini
    4.blue-bahari,maziwa na mito.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 12, 2007

    rangi nne
    kijani: misitu na mimea(mazao)
    njano: madini
    nyeusi: watu
    bluu: Maziwa na bahari (vilivyomo?)

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 12, 2007

    Nyakusya bwege tu wewe madaraka uliyonayo mwachie mwenye blog afanye atakalo. If you think you are too superior don't read his blog.


    Watu wengine bwana...

    Kuna watoto wakibongo wengi tu wanaishi nchi za nje na hawajui lolote kuhusu nchi yetu na haya maswali ni changa moto kwao kuelewa kidogo juu ya nchi yetu.

    Nafagilia maswali haya kuliko yale yanayouliza ni sehemu gani hii. Keep up Michuzi with your good work. You will neverr please everyone.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 12, 2007

    Mambo Ndugu Michuzi!
    Wabongo hatuelewi Michuzi tunamuona tu kwenye picha , kwa wasiomjua wanamuona kama shwaini Fulani kumbe kichwa ! mkewe anapendeza watoto wake wanamtia gharama ya kuita gari la maji machafu kunyonya choo chake wanavyoshiba Hii sio dharau sisi wabongo tunajua rangi ya bendera yetu lakini hatujui maana yake ! nakwambia mimi naishi ulaya najua maan ya rangi ya bendera ya nchi yangu, nakumbuka mungu mrehemu baba wa taifa ametufunza mengi enzi hizo vijana wa leo michuzi hawajui hata maana ya JKT ! it means hawana jibu zaidi ya kujua club za starehe za bongo , kuishi ulaya michuzi tumekimbia mengi nyumbani ! school fees zenu za international school ni mtaji tosha kujenga nyumba huku ughaibuni elimu kwa mtoto ni bure baba !
    Nakumbuka na wewe una mbwembwe ila nakuzimia ulipokuja London majivuni huna kila mmakonde uliongea naye aliyekukaribisha ulikwenda wewe mjanja , god bless you unakoelekea mwanga umeuona na utafunuliwa mkuu !

    BENDERA YA TAIFA INA RANGI NNE

    NJANO – INA MAANA KUWA TANZANIA TUNA MADINI NDANI YA NCHI
    YETU (UTAJIRI WETU WA MADINI)
    BLUE – INAASHIRIA BAHARI ILIYOTUZUNGUKA NA MAZIWA
    TUNAYOJIVUNIA
    KIJANI – NI MISITU YETU KUONYESHA NCHI YETU INA GREEN
    VEGETATION (SAVANNA)
    NYEUSI – INA MAANISHA YA SISI WAAFRICA TUNAOISHI BONGO NI
    WEUSI WA RANGI


    NYERERE MUNGU AMBARIKI SANA


    NAOMBA PICHA YA KUONA RAISI MSTAAFU KAMA ALIKWENDA JKT

    ReplyDelete
  11. Zawadi zetu (za Fire,ile picha) vipi hadi lini? Na lile shindano jingine watu wapo club wanaruka mbona hutangazi mshindi/washindi?

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 12, 2007

    YOO Waosha vinywa wenzangu wote mmekosea bendera yetu ina rangi nne ni kweli.
    KIJANI: MAJANI YA NYANI YALIYOPO
    KILIMANI

    MANJANO:
    UWANJA WA MAPAMBANO TUNAO JARIBU KUPAMBANA NAO KILA LEO(MCHANA KUTWA NA USIKU KUCHA SISI WALALA HOI WAVUJA JASHO WA NCHI HII WAKATI WENYE MENO MAKALI WAKITAFUNA NCHI KIULAINI BILA UCHUNGU WOWOTE).

    NYEUSI:WATU WEUSI MSIOTAKIWA NA
    WAZUNGU, WAARABU, WAHINDI
    KILA LEO KAZI KUJIPENDEKEZA
    KWAO.

    MANJANO: MKUJANO KWA MADEMU

    BLUE: HAKUNA BURUDANI NZURI
    KAMA KUMPATA DEMU
    NA KUVINJARI NAYE VIWANJA

    BRO MICHU USITUPE KAPUNI HII KOMENT YANGU AISEEE NITAKUFUATA HUKO HUKO ULIPO UKIFANYA HIVYO.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 12, 2007

    Bendera ya Taifa ina rangi nne(4)
    1.KIJANI-inawakilisha ardhi na misitu (mali asili)
    2.NJANO-inawakilisha madini
    3.NYEUSI-inawakilisha watu (raia/wananchi)
    4.BLUU-inawakilisha maziwa, mito na bahari.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 12, 2007

    Kijani = Uoto wa asili- misitu, mimea
    Njano = Madini yetu
    Nyeusi = Watu, wananchi wa Tanzania.
    Buluu = Bahari- Kielelezo cha kitu kinachoonyesha Muungano wetu wa nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 12, 2007

    hellow

    Bendera yetu ina rangi 4. kama zifuatavyo :-

    Kijani inamaanisha jinsi ilivyo jaaliwa kuwa na mimea mingi ya rangi ya kijani.(mimea yenye rutuba)
    Manjano inaonesha jinsi ilivyo jaaliwa kuwa na madini mengi.
    Nyeusi ni watu wake asilimia kubwa ni weusi.
    Buluu inaonesha jinsi ilivyozungukwa na Bahari ya Hindi.

    Byee

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 12, 2007

    KIJANI-Bank iliyokufa ya GREENLAND.
    NJANO-Mchanga wetu wenye madini ya dhahabu unaopelekwa Ng'ambo.
    NYEUSI-Rangi yetu wavuja jasho,waponda kokoto,Vibarua etc.
    BLUU- Bahari yetu maziwa yetu yanayochafuliwa kwa pollution na Magugu maji...
    Mpenda keroro...
    Michuzi naomba zawadi yangu...

    ReplyDelete
  17. AnonymousJuly 12, 2007

    Bendera ya Taifa ina rangi nne, nazo na maana yake ni:
    1. Kijani - Misitu na mali ya asili
    2. Njano - Madini
    3. Nyeusi - Watu (japo ni politica incorrect kwani tuna waarabu, wahindi na wazungu watanzania)
    4. Bluu- Bahari inayounganisha nchi yetu.

    ReplyDelete
  18. AnonymousJuly 12, 2007

    Aaaaaaaa,teh teh teh ,kwiiiiiikwikiki,do hapa watu wanaigiliziana tuuu .kudesaaaaa hukooo kwa nguvu.

    ReplyDelete
  19. AnonymousJuly 12, 2007

    hii kweli kutufanya wajinga, mambo haya tulifundishwa shule,hakuna mtu ambaye hakufundishwa maana ya bendera ya taifa hata chekechekea siku hizi wanajuwa! uliza mambo ya maana sio upuuzi

    ReplyDelete
  20. AnonymousJuly 12, 2007

    NINYI SWAHILI HAKUNA TAHA MOJA NAJUA RANGI YA BENDERA YENU. NYIE OTE NALOPOKA TU JIFANYA NAJUA KILA KITU.
    UKITAKA JUA MAANA HALISI YA RANGI YENU, ANGALIA HII HAPA.
    NYEUSI-NYIE WOTE WACHAFU HAKUNA HATA MMOJA ANATAKA KUOGA.
    NJANO-MENO YENU YAMEKUWA NJANO KWA SABABU HAKUNA MOJA YENU ANAPIGA MSWAKI.
    KIJANI-KILA MOJA YENU ANALALA HUKO MASHAMBA KUAMKIA KWENYE MAJANI.
    BLUU-KILA MOJA ANAKUNYWA MAJI YANAYOTOKA BAHARINI AU CHIMBA CHIMBA KISIMANI.
    WE MICHUZI NAONA HUNA KITU SASA. BLOG YAKO KWISA ISHA NGUVU YAKE MITU MINGI SASA NAKIMBIA WEWE. JINGA KUBWA WEWE.

    ReplyDelete
  21. AnonymousJuly 12, 2007

    WE MICHUZI UMEISHIWA KWELI. BORA UNGEWAULIZA WATU WAKO BENDERA YA ZANZIBAR INA RANGI GANI?
    AU BENDERA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO INA RANGI GANI?
    UNAULIZA BENDERA YA TAIFA...KWELI SHULE MUHIMU.RUDI UKASOME.

    ReplyDelete
  22. AnonymousJuly 12, 2007

    Michuzi mimi ningeona usingekua unaweka majibu ya watu right away. Watu wengine wanasoma majibu ya watu halafu wao wanaweka more creative halafu wao ndio wanakua washindi. Ingewezekana kama ungewacha mpaka siki ua mwisho halafu ndio unaweka yote kwa pamoja na kumtangaza aliyeshinda na watu tunaona nani kajibu vipi.

    Thank you

    ReplyDelete
  23. AnonymousJuly 12, 2007

    Bendera ya Tanzania ina rangi nne.
    1-Rangi ya Kijani inawakilisha misitu ya tanzania.
    2-Rangi ya Manjano inawakilisha madini ya tanzania.
    3-Rangi nyeusi inawakilisha watu wa tanzania.
    4-Rangi ya Bluu inawakilisha mito, waziwa na bahari za tanzania.

    Thanks.

    Katty.
    Mdau wa NY.

    ReplyDelete
  24. AnonymousJuly 13, 2007

    Ama

    I. Kwa vile mpaka sasa duniani hakuna bendera inayojulikana kama BENDERA YA TAIFA. Haiwezekani kutaja idadi, aina wala maana ya rangi zake.

    AU
    II. Kama swali lako lilimaanisha BENDERA YA TAIFA LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, majibu ni kama ifuatavyo:-
    1. Ina rangi NNE TOFAUTI

    2.RANGI NA MAANA (UWAKILISHI)
    i.KIJANI- ARDHI
    ii.DHAHABU - MADINI
    iii.NYEUSI - WATU
    IV.BULUU (BLUU) - BAHARI NA MAZIWA

    TANBIHI:
    Asidese mtu hapa. Michuzi swali zuri na ndio maana kuna majibu anuwai.

    Chirangi

    ReplyDelete
  25. AMA
    I. Kwa vile mpaka sasa duniani hakuna bendera inayojulikana kama BENDERA YA TAIFA, basi HAIWEZEKANI KUTAJA IDADI, AINA WALA MAANA YA RANGI ZA BENDERA ISIYOKUWEPO.

    AU
    II. Kama swali lako lilimaanisha BENDERA YA TAIFA LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, Majibu yake
    ni kama ifuatavyo:

    1. Ina rangi NNE TOFAUTI.

    2. Rangi na maana (uwakilishi wake)
    i. KIJANI - ARDHI
    ii. DHAHABU - MADINI
    iii. NYEUSI - WATU
    IV. BULUU(BLUU) - BAHARI NA MAZIWA

    Tanbihi:
    Asidese mtu hapa maana watu wameshabaki! Michuzi swali zuri sana ndio maana kunatokea majibu anuwai.

    Chirangi

    ReplyDelete
  26. AMA
    I. Kwa vile mpaka sasa duniani hakuna bendera inayojulikana kama BENDERA YA TAIFA, basi HAIWEZEKANI KUTAJA IDADI, AINA WALA MAANA YA RANGI ZA BENDERA ISIYOKUWEPO.

    AU
    II. Kama swali lako lilimaanisha BENDERA YA TAIFA LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, Majibu yake ni kama ifuatavyo:
    1. Ina rangi NNE TOFAUTI.

    2. Rangi na maana (uwakilishi wake)
    i. KIJANI - ARDHI
    ii. DHAHABU - MADINI
    iii. NYEUSI - WATU
    IV. BULUU(BLUU) - BAHARI NA MAZIWA

    Tanbihi:
    Asidese mtu hapa maana watu wameshabaki! Michuzi swali zuri sana ndio maana kunatokea majibu anuwai.

    Chirangi

    ReplyDelete
  27. AnonymousJuly 13, 2007

    Hee !! smahani nimesahau nitaenda "google"

    ReplyDelete
  28. AnonymousJuly 13, 2007

    Naitwa Zamda
    Kijani - Mimea
    Nyeusi - Rangi ya waafrica
    Bluu - Bahari
    Manjano - Madini

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...