SWALI: BENDERA YA TAIFA INA RANGI NGAPI, ZITAJE MOJA MOJA NA ELEZA MAANA YAKE.
MASHARTI:
1. WABONGO WOTE NDANI NA NJE YA NCHI RUKSA KUSHIRIKI
2. ANONYMOUS ATAKUWA AMEJIDISKUALIFAI MWENYEWE, JINA LINAHITAJIKA
3. USILETE UFUNDI, JIBU SWALI KAMA LILIVYO
4. ENDAPO WASHINDI WATAKUWA ZAIDI YA WATATU TOMBOLA ITACHEZESHWA KUPATA WASHINDI WATATU - WA KWANZA, WA PILI NA WATATU
5. UAMUZI WA MAJAJI NI WA MWISHO, HAMNA KUKATA RUFAA
6. MSTARI MFU NI JUMAMOSI HII IJAYO SAA SITA MCHANA SAA ZA BONGO
7. MSHINDI ATATANGAZWA JUMATATU
ZAWADI;
1. PICHA YOYOTE MSHINDI ATAYOTAKA
2. ZAWADI INAPENDEZA IKIBANDIKWA BLOGUNI, KAMA MWENYEWE HATAKI ATATUMIWA
Bendera ya Taifa ina Rangi NNE zifuatazo na maana ya rangi mbele ya rangi:
ReplyDeleteKIJANI- Ardhi
DHAHABU-Madini
NYEUSI-Watu
BLUU-Bahari na Maziwa.
Rangi nne
ReplyDeleteKijani = misitu yetu
manjano= madini yetu
nyeusi = sisi wenyewe raia wa nchi
blue = maziwa na bahari zetu
MICHUZI NAONA SASA UMEANZA KUTUZARAU. HILO SWALI NI LA WATOTO WA CHEKECHEA.WEBSITE YAKO INA SOMWA SANA NA WATU WALIO SOMA NA WANA MADARAKA NA HAYO ULIYO ULIZA WANA YAJUA SANA.PLEASE MICHU, TUHESHIMU KIDOGO.
ReplyDeleteNDAGA FIJO.
Bendera ya Taifa ina rangi Nne,Nazo ni:
ReplyDelete1.Nyeusi -Watu(ambao ni sisi watanzania au raia wa nchi hii ambayo ni moja ya nchi barani mwetu Afrika)
2.Manjano- Madini(Utajiri wetu wa Madini)
3.Blue- Bahari(Maziwa,mito na bahari)
4.kijani-Ardhi(misitu na uanda wa asili)
1. BAHARI 2. MADINI 3.WATU 4.ARDHI
ReplyDelete1.bluu ni bahari,mito na maziwa 2.njano ni madini 3.nyeusi ni watu 4.kijani. ni ardhi,
ReplyDeleterangi za bendera ya taifa~
ReplyDelete1 nyeusi-wanachi wa tanzania
2.kijani-uoto wa asili ,ardhi
3.njano-madini
4.blue-bahari,maziwa na mito.
rangi nne
ReplyDeletekijani: misitu na mimea(mazao)
njano: madini
nyeusi: watu
bluu: Maziwa na bahari (vilivyomo?)
Nyakusya bwege tu wewe madaraka uliyonayo mwachie mwenye blog afanye atakalo. If you think you are too superior don't read his blog.
ReplyDeleteWatu wengine bwana...
Kuna watoto wakibongo wengi tu wanaishi nchi za nje na hawajui lolote kuhusu nchi yetu na haya maswali ni changa moto kwao kuelewa kidogo juu ya nchi yetu.
Nafagilia maswali haya kuliko yale yanayouliza ni sehemu gani hii. Keep up Michuzi with your good work. You will neverr please everyone.
Mambo Ndugu Michuzi!
ReplyDeleteWabongo hatuelewi Michuzi tunamuona tu kwenye picha , kwa wasiomjua wanamuona kama shwaini Fulani kumbe kichwa ! mkewe anapendeza watoto wake wanamtia gharama ya kuita gari la maji machafu kunyonya choo chake wanavyoshiba Hii sio dharau sisi wabongo tunajua rangi ya bendera yetu lakini hatujui maana yake ! nakwambia mimi naishi ulaya najua maan ya rangi ya bendera ya nchi yangu, nakumbuka mungu mrehemu baba wa taifa ametufunza mengi enzi hizo vijana wa leo michuzi hawajui hata maana ya JKT ! it means hawana jibu zaidi ya kujua club za starehe za bongo , kuishi ulaya michuzi tumekimbia mengi nyumbani ! school fees zenu za international school ni mtaji tosha kujenga nyumba huku ughaibuni elimu kwa mtoto ni bure baba !
Nakumbuka na wewe una mbwembwe ila nakuzimia ulipokuja London majivuni huna kila mmakonde uliongea naye aliyekukaribisha ulikwenda wewe mjanja , god bless you unakoelekea mwanga umeuona na utafunuliwa mkuu !
BENDERA YA TAIFA INA RANGI NNE
NJANO – INA MAANA KUWA TANZANIA TUNA MADINI NDANI YA NCHI
YETU (UTAJIRI WETU WA MADINI)
BLUE – INAASHIRIA BAHARI ILIYOTUZUNGUKA NA MAZIWA
TUNAYOJIVUNIA
KIJANI – NI MISITU YETU KUONYESHA NCHI YETU INA GREEN
VEGETATION (SAVANNA)
NYEUSI – INA MAANISHA YA SISI WAAFRICA TUNAOISHI BONGO NI
WEUSI WA RANGI
NYERERE MUNGU AMBARIKI SANA
NAOMBA PICHA YA KUONA RAISI MSTAAFU KAMA ALIKWENDA JKT
Zawadi zetu (za Fire,ile picha) vipi hadi lini? Na lile shindano jingine watu wapo club wanaruka mbona hutangazi mshindi/washindi?
ReplyDeleteYOO Waosha vinywa wenzangu wote mmekosea bendera yetu ina rangi nne ni kweli.
ReplyDeleteKIJANI: MAJANI YA NYANI YALIYOPO
KILIMANI
MANJANO:
UWANJA WA MAPAMBANO TUNAO JARIBU KUPAMBANA NAO KILA LEO(MCHANA KUTWA NA USIKU KUCHA SISI WALALA HOI WAVUJA JASHO WA NCHI HII WAKATI WENYE MENO MAKALI WAKITAFUNA NCHI KIULAINI BILA UCHUNGU WOWOTE).
NYEUSI:WATU WEUSI MSIOTAKIWA NA
WAZUNGU, WAARABU, WAHINDI
KILA LEO KAZI KUJIPENDEKEZA
KWAO.
MANJANO: MKUJANO KWA MADEMU
BLUE: HAKUNA BURUDANI NZURI
KAMA KUMPATA DEMU
NA KUVINJARI NAYE VIWANJA
BRO MICHU USITUPE KAPUNI HII KOMENT YANGU AISEEE NITAKUFUATA HUKO HUKO ULIPO UKIFANYA HIVYO.
Bendera ya Taifa ina rangi nne(4)
ReplyDelete1.KIJANI-inawakilisha ardhi na misitu (mali asili)
2.NJANO-inawakilisha madini
3.NYEUSI-inawakilisha watu (raia/wananchi)
4.BLUU-inawakilisha maziwa, mito na bahari.
Kijani = Uoto wa asili- misitu, mimea
ReplyDeleteNjano = Madini yetu
Nyeusi = Watu, wananchi wa Tanzania.
Buluu = Bahari- Kielelezo cha kitu kinachoonyesha Muungano wetu wa nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar
hellow
ReplyDeleteBendera yetu ina rangi 4. kama zifuatavyo :-
Kijani inamaanisha jinsi ilivyo jaaliwa kuwa na mimea mingi ya rangi ya kijani.(mimea yenye rutuba)
Manjano inaonesha jinsi ilivyo jaaliwa kuwa na madini mengi.
Nyeusi ni watu wake asilimia kubwa ni weusi.
Buluu inaonesha jinsi ilivyozungukwa na Bahari ya Hindi.
Byee
KIJANI-Bank iliyokufa ya GREENLAND.
ReplyDeleteNJANO-Mchanga wetu wenye madini ya dhahabu unaopelekwa Ng'ambo.
NYEUSI-Rangi yetu wavuja jasho,waponda kokoto,Vibarua etc.
BLUU- Bahari yetu maziwa yetu yanayochafuliwa kwa pollution na Magugu maji...
Mpenda keroro...
Michuzi naomba zawadi yangu...
Bendera ya Taifa ina rangi nne, nazo na maana yake ni:
ReplyDelete1. Kijani - Misitu na mali ya asili
2. Njano - Madini
3. Nyeusi - Watu (japo ni politica incorrect kwani tuna waarabu, wahindi na wazungu watanzania)
4. Bluu- Bahari inayounganisha nchi yetu.
Aaaaaaaa,teh teh teh ,kwiiiiiikwikiki,do hapa watu wanaigiliziana tuuu .kudesaaaaa hukooo kwa nguvu.
ReplyDeletehii kweli kutufanya wajinga, mambo haya tulifundishwa shule,hakuna mtu ambaye hakufundishwa maana ya bendera ya taifa hata chekechekea siku hizi wanajuwa! uliza mambo ya maana sio upuuzi
ReplyDeleteNINYI SWAHILI HAKUNA TAHA MOJA NAJUA RANGI YA BENDERA YENU. NYIE OTE NALOPOKA TU JIFANYA NAJUA KILA KITU.
ReplyDeleteUKITAKA JUA MAANA HALISI YA RANGI YENU, ANGALIA HII HAPA.
NYEUSI-NYIE WOTE WACHAFU HAKUNA HATA MMOJA ANATAKA KUOGA.
NJANO-MENO YENU YAMEKUWA NJANO KWA SABABU HAKUNA MOJA YENU ANAPIGA MSWAKI.
KIJANI-KILA MOJA YENU ANALALA HUKO MASHAMBA KUAMKIA KWENYE MAJANI.
BLUU-KILA MOJA ANAKUNYWA MAJI YANAYOTOKA BAHARINI AU CHIMBA CHIMBA KISIMANI.
WE MICHUZI NAONA HUNA KITU SASA. BLOG YAKO KWISA ISHA NGUVU YAKE MITU MINGI SASA NAKIMBIA WEWE. JINGA KUBWA WEWE.
WE MICHUZI UMEISHIWA KWELI. BORA UNGEWAULIZA WATU WAKO BENDERA YA ZANZIBAR INA RANGI GANI?
ReplyDeleteAU BENDERA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO INA RANGI GANI?
UNAULIZA BENDERA YA TAIFA...KWELI SHULE MUHIMU.RUDI UKASOME.
Michuzi mimi ningeona usingekua unaweka majibu ya watu right away. Watu wengine wanasoma majibu ya watu halafu wao wanaweka more creative halafu wao ndio wanakua washindi. Ingewezekana kama ungewacha mpaka siki ua mwisho halafu ndio unaweka yote kwa pamoja na kumtangaza aliyeshinda na watu tunaona nani kajibu vipi.
ReplyDeleteThank you
Bendera ya Tanzania ina rangi nne.
ReplyDelete1-Rangi ya Kijani inawakilisha misitu ya tanzania.
2-Rangi ya Manjano inawakilisha madini ya tanzania.
3-Rangi nyeusi inawakilisha watu wa tanzania.
4-Rangi ya Bluu inawakilisha mito, waziwa na bahari za tanzania.
Thanks.
Katty.
Mdau wa NY.
Ama
ReplyDeleteI. Kwa vile mpaka sasa duniani hakuna bendera inayojulikana kama BENDERA YA TAIFA. Haiwezekani kutaja idadi, aina wala maana ya rangi zake.
AU
II. Kama swali lako lilimaanisha BENDERA YA TAIFA LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, majibu ni kama ifuatavyo:-
1. Ina rangi NNE TOFAUTI
2.RANGI NA MAANA (UWAKILISHI)
i.KIJANI- ARDHI
ii.DHAHABU - MADINI
iii.NYEUSI - WATU
IV.BULUU (BLUU) - BAHARI NA MAZIWA
TANBIHI:
Asidese mtu hapa. Michuzi swali zuri na ndio maana kuna majibu anuwai.
Chirangi
AMA
ReplyDeleteI. Kwa vile mpaka sasa duniani hakuna bendera inayojulikana kama BENDERA YA TAIFA, basi HAIWEZEKANI KUTAJA IDADI, AINA WALA MAANA YA RANGI ZA BENDERA ISIYOKUWEPO.
AU
II. Kama swali lako lilimaanisha BENDERA YA TAIFA LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, Majibu yake
ni kama ifuatavyo:
1. Ina rangi NNE TOFAUTI.
2. Rangi na maana (uwakilishi wake)
i. KIJANI - ARDHI
ii. DHAHABU - MADINI
iii. NYEUSI - WATU
IV. BULUU(BLUU) - BAHARI NA MAZIWA
Tanbihi:
Asidese mtu hapa maana watu wameshabaki! Michuzi swali zuri sana ndio maana kunatokea majibu anuwai.
Chirangi
AMA
ReplyDeleteI. Kwa vile mpaka sasa duniani hakuna bendera inayojulikana kama BENDERA YA TAIFA, basi HAIWEZEKANI KUTAJA IDADI, AINA WALA MAANA YA RANGI ZA BENDERA ISIYOKUWEPO.
AU
II. Kama swali lako lilimaanisha BENDERA YA TAIFA LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, Majibu yake ni kama ifuatavyo:
1. Ina rangi NNE TOFAUTI.
2. Rangi na maana (uwakilishi wake)
i. KIJANI - ARDHI
ii. DHAHABU - MADINI
iii. NYEUSI - WATU
IV. BULUU(BLUU) - BAHARI NA MAZIWA
Tanbihi:
Asidese mtu hapa maana watu wameshabaki! Michuzi swali zuri sana ndio maana kunatokea majibu anuwai.
Chirangi
Hee !! smahani nimesahau nitaenda "google"
ReplyDeleteNaitwa Zamda
ReplyDeleteKijani - Mimea
Nyeusi - Rangi ya waafrica
Bluu - Bahari
Manjano - Madini