GWIJI LA SANAA NCHINI MZEE GODWIN KADUMA (WA PILI KULIA WALIOKAA) HATUNAYE TENA.


HABARI ZILIZOTUFIKIA SASA HIVI NI KWAMBA MZEE KADUMA AMEFARIKI MCHANA HUU KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI ALIKOLAZWA KWA MUDA.


MZEE KADUMA ATAKUMBUKWA SIO TU KWA UMAHIRI WAKE KATIKA KUIGIZA BALI PIA AMEWAHI KUWA MKURUGENZI WA SANAA NA LUGHA KATIKA WIZARA YA UTAMADUNI NA MICHEZO, NA PIA ALIKUWA MSTARI WA MBELE KATIKA KUENDELEZA SANAA NCHINI.


PICHANI MZEE KADUMA AKIWA KAMA MKURUGENZI WA LUGHA NA SANAA AKIPOZI NA HAYATI MOSES NNAUYE NA BARAZA LA KWANZA LA MUZIKI WA DANSI ALMAARUFU KAMA CHAMUDATA MWAKA 1988 OFISI ZA BARAZA LA SANAA ILALA SHARIFF SHAMBA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Poleni sna wanasanaa wote wa Tanzania kwa msiba huu pia familia ya mzee Kaduma, Siuongo mzee wetu huyu amechangia sana maendeleo ya sanaa nchini kwetu. Mwenyezi Mungu ampumzishe pema peponi-Mlewa-Uk

    ReplyDelete
  2. VAA NGUO **NYEKUNDU** KESHO ISHARA YA
    KUUNGA MKONO HARAKATI ZA KUTETEA
    WATU WA BURMA.

    In support of our incredibily brave friends in Burma.
    May all people around the world wear a red shirt on friday,September 28(kesho)Please tell others.

    Kwa kufanya hivyo namna moja au nyingine na wewe unakuwa unashiriki katika kutetea haki za rai na kuunga mkono ngumu ya umma.

    Kwa kufanya hivyo utakuwa umesaidia na kushiriki.

    Naomba kuwasilisha.

    ReplyDelete
  3. du, alikuwa mkuu wa chuo miaka ya tisini enzi zetu pale bagamoyo college of arts...rip mzee kaduma

    ReplyDelete
  4. Poleni kwa kufikwa na msiba huu ndani ya mwezi mtukufu, Mwenyezi Mungu awajaalie ndugu, jamaa, marafiki, wasanii, wapenzi wa kazi zake uvumilivu ktk wakati huu mgumu.

    Tulimpenda lakini Mungu alimpenda zaidi hivyo hatuna buni kushukuru badala ya kulia na kulalamika kwanini?.....amina

    Dinah.

    ReplyDelete
  5. He was like a pillar on the centre of a roof of Arts.Tutamkubuka sana kwa mchango wake na busara aliyo kuwa nayo nayo.Kwa ndugu na jamaa poleni sana ingawa maisha lazima yaendelee "it is a path that we all have to follow. Rwambali-Germany

    ReplyDelete
  6. Nimepokea kwa masikitiko msiba wa mzee wetu mzee GodwinKaduma.

    Tunawaombea wanafamilia,jamaa na marafiki Mungu watie nguvu katika kipindi hiki kigumu walicho nacho.

    Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu Mzee kaduma mahali pema peponi.amina

    ReplyDelete
  7. Machozi juu ya mashavu yangu.Nimesikitika sana.
    Majita

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...