
Waingereza wanasema ‘Many Happy Returns’, basi nami nimeona nikudunge na stoki ya YOSSO enzi zetu zilee vijana wa Isamilo Kids tukichachafya YOSSO pale mkoani Mwanza.
Shukrani kwa huduma yako nzuri ya buree na inayotufurahisha sote tulio mbali na nyumbani. Mimi kama mwanamichezo nimefurahishwa na maendeleo, japo kidogo, yaliyoonyeshwa na Taifa Stars. Ila ukweli ni kwamba, tunaomba nguvu ziwekezwe katika YOSSO, tuwe na mipango ya miaka.
Hilo jengo hapo, sio ofisi ya Idara Ya Michezo tena hapo Mwanza, bali ni moja ya majengo ya Kuleana (NGO inayosaidia watoto wa mitaani, ambayo pia ni kazi nzuri). Watoto/Vijana ndio taifa la kesho, na michezo ni njia moja ya kukutanisha marafiki bila kubaguana umetoka wapi.
Picha hii naipenda sana, kwani YOSSO yote hiyo ilikutanisha vijana kutoka familia mbalimbali (wenye maisha ya juu, na wenye maisha ya chini), lakini hatukubaguana hata siku moja. Bahati mbaya nimepotezana na marafiki hawa, wengine (YOSSO tuliocheza nao) wamekuja kucheza timu za madaraja ya juu hapo TZ.
Salaaaam,
Happy Birthday.
Defunkadelic
Defunkadelic
defunkdelic vipi mambo mkuu?jaribu ku up2 date website yako especial mambo ya muziki mi nilifikiri umepotea kusiko julikana.
ReplyDeletehahaha hapo namjua asaph walochuchumaa 3 toka kushoto na eric 2 toka kulia, long time
ReplyDeletedefunka...hapo ilikuwa mwaka gani? Manake sisi tulikuwa na timu yetu ya Isamilo miaka ya mwanzo wa 80? Basi tulikuwa twakaa njia ya kwenda nyanshana....
ReplyDelete