waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa mh. profesa athumani juma kapuya akipokewa na viongozi wakuu wa jeshi la ulinzi uwanja wa ndege wa airwing jioni hii akitokea tabora ambako alipata ajali ya gari iliyosababisha kifo cha mtu mmoja na kumjeruhi yeye na watu wengine watatu. alipowasili uwanja wa ndege alikuwa na fahamu zake na aliweza kusalimia wliokuja kumpokea bila shida sana. inasemekana gari alilokuwemo lilipasuka tairi la mbele na kupinduka mara tatu na kwamba alinusurika madhara makubwa kwa vile alikuwa amejifunga mkanda

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. naona umekosea jina la mheshimiwa,asante kwa breaking news!

    ReplyDelete
  2. naona umekosea jina la mheshimiwa,asante kwa breaking news!

    ReplyDelete
  3. Jeez kwani kapoteza fahamu?, we wish him quick recovery-Amen

    ReplyDelete
  4. Pole sana mh.Athumani Juma Kapuya,naona friends of simba mwenzako michael richard wambura kaja kukujulia hali hapo! kumbe anakumbuka fadhila eenh!

    ReplyDelete
  5. Heee jamani mbona ajali nyingi sana bongooo!!! juzi tu Mudhihir leo Kapuya tena!!!! Kulikoni!

    ReplyDelete
  6. Mhh!
    Pole sana. Nadhani zile tuhuma za Slaa sasa zijibiwe. VIngenevyo, tutapinduka wengi kwa kweli. Haiwezekani in three months mawaziri pamoja na wabunge watano wapate mikasa namna hii! KUna namna sasa. Haiwezi kuwa hivi hivi.

    Pole sana na pona salama Professor wangu wa Botany Physiology pale UDSM.

    ReplyDelete
  7. BLAZA MICHU HEBU KAFIKISHE HAKA KA UJUMBE...MISAFARA YA HAWA MABOSI INAKIUKA TARATIBU ZOTE ZA SPEED LIMIT MIJINI (I ASSUME NA VIJIJINI PIA)..HAYA MA 'VX' NA MA GRX YAO MOVE LIKE LIGHTNING...YANA SPIDI ILE MBAYA...WHY!!!...USHAUONA MSAFARA WA KIKWETE WAKIWA WANAENDA BAGAMOYO???...WANATIMUA VUMBI KWENYE LAMI!!!...WANAPITA MAKUMBUSHO WAKO AIRBORNE!!!...HIVI HAYA MASPIDI HUWA NI YA NINI???...i am 100 percent sure hii latest ya kapuya the thing was flying..."rolled over" 3 times!!!...WHY???...narudia tena kwani wakimuvu na 80kph itakuwaje???

    ReplyDelete
  8. WENYE MABASI WANAJARIBU KUZIBA ISHU YAO YA AJALI KWA HIZI AJALI ZA VIGOGO(CHUNGUZA VIZURI KAPUYA NA MUDHIHIRI)KIGEZO HATA WAKUBWA WANAPATA AJALI ?

    ReplyDelete
  9. Je, hao waliojeruhiwa walikuwa wamevaa Seat Belts?

    ReplyDelete
  10. mbona habari hazieleweki,,,wamekufa watatu au mmoja, anyway Professor ugua pole, mungu akujalie.

    ReplyDelete
  11. we unauliza waliojeruhiwa walikuwa wamevaa seat belts? ukishapata jibu, litakusaidia nini, ajali ndo ishatokea, kinachotakiwa sasa kuwaombea majeruhi wapone na kuombea faraja familia ya marehemu. Unauliza hivyo, we mtu wa usalama wa barabarani,,kaongeze alama na mataa huko vijijini, upunguze ajali,usianze kuuliza maswali yasiyo na msingi hapa...we hapo ulipokaa kwenye mtandao umefunga seat belt?

    ReplyDelete
  12. POLE SANA MHESHIMIWA KAPUYA,MTU WA WATU.JAMANI VIONGOZI WANAPASWA KUJIFUNZA KWA KAPUYA,AJALI YAKE IMEWAGUSA WATU WA KADA MBALIMBALI NA KILA MTU ANAMPA POLE NA KUMUOMBEA HERI HII NDIO RAHA YA KUWA MTETEZI NA MTU WA WATU..SASA WALE VIONGOZI WANAOJALI MATUMBO YAO WAANGALIE MFANO HUU..MBONA MTU MWINGINE AKIPATA AJALI WANANCHI WANAMLAANI NA KUMUOMBEA KIFO LAKINI INAKUWA TOFAUTI KWA MTU KAMA KAPUYA?? JAMANI SAUTI YA WATU NI SAUTI YA MUNGU NA KWA MAONI YA WATU PROFESA KAPUYA UNAPENDWA...VIVA KAPUYA PONA HARAKA UENDELEE KULIJENGA TAIFA ACHANA NA HAO WANAUZA NCHI KUPITIA MAHOTELINI UINGEREZA....

    ReplyDelete
  13. Wewe anon unaeshangaa mtu kuuliza kama majeruhi walikuwa wamevaa mikanda una matatizo.

    Unanishangaza zaidi kusema kuwa eti .."kinachotakiwa sasa ni kuwaombea majeruhi wapone"Wewe chizi nini??Majeruhi hawaombewi wakapona bali wanatakiwa kupelekwa hospitalini haraka wapatiwe matibabu wapone.Maombi maombi,kazi kukariri tu.Kubwa ziiiiii!!!!Fyuuu(msunyo).Acheni imani za ajabu za kuombea watu wapone.Wewewewe!!NIKIKUKAMATA????

    ReplyDelete
  14. Nafikiri umefika muda wa kurekebisha barabara zetu za vijijini na watu kufuata sheria za barabarani. Poleni na ugueni pole majeruhi wote

    ReplyDelete
  15. Hivi kwani huyu nae alisapoti ile hoja ya Mudhihir kule Bungeni Dodoma?
    Mweeh!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...