
waziri wa ulinzi na jeshi la kujenga taifa mh. profesa athumani juma kapuya akipokewa na viongozi wakuu wa jeshi la ulinzi uwanja wa ndege wa airwing jioni hii akitokea tabora ambako alipata ajali ya gari iliyosababisha kifo cha mtu mmoja na kumjeruhi yeye na watu wengine watatu. alipowasili uwanja wa ndege alikuwa na fahamu zake na aliweza kusalimia wliokuja kumpokea bila shida sana. inasemekana gari alilokuwemo lilipasuka tairi la mbele na kupinduka mara tatu na kwamba alinusurika madhara makubwa kwa vile alikuwa amejifunga mkanda
naona umekosea jina la mheshimiwa,asante kwa breaking news!
ReplyDeletenaona umekosea jina la mheshimiwa,asante kwa breaking news!
ReplyDeleteJeez kwani kapoteza fahamu?, we wish him quick recovery-Amen
ReplyDeletePole sana mh.Athumani Juma Kapuya,naona friends of simba mwenzako michael richard wambura kaja kukujulia hali hapo! kumbe anakumbuka fadhila eenh!
ReplyDeleteHeee jamani mbona ajali nyingi sana bongooo!!! juzi tu Mudhihir leo Kapuya tena!!!! Kulikoni!
ReplyDeleteMhh!
ReplyDeletePole sana. Nadhani zile tuhuma za Slaa sasa zijibiwe. VIngenevyo, tutapinduka wengi kwa kweli. Haiwezekani in three months mawaziri pamoja na wabunge watano wapate mikasa namna hii! KUna namna sasa. Haiwezi kuwa hivi hivi.
Pole sana na pona salama Professor wangu wa Botany Physiology pale UDSM.
Pole sana Prof. Kapuya.
ReplyDeleteBLAZA MICHU HEBU KAFIKISHE HAKA KA UJUMBE...MISAFARA YA HAWA MABOSI INAKIUKA TARATIBU ZOTE ZA SPEED LIMIT MIJINI (I ASSUME NA VIJIJINI PIA)..HAYA MA 'VX' NA MA GRX YAO MOVE LIKE LIGHTNING...YANA SPIDI ILE MBAYA...WHY!!!...USHAUONA MSAFARA WA KIKWETE WAKIWA WANAENDA BAGAMOYO???...WANATIMUA VUMBI KWENYE LAMI!!!...WANAPITA MAKUMBUSHO WAKO AIRBORNE!!!...HIVI HAYA MASPIDI HUWA NI YA NINI???...i am 100 percent sure hii latest ya kapuya the thing was flying..."rolled over" 3 times!!!...WHY???...narudia tena kwani wakimuvu na 80kph itakuwaje???
ReplyDeleteWENYE MABASI WANAJARIBU KUZIBA ISHU YAO YA AJALI KWA HIZI AJALI ZA VIGOGO(CHUNGUZA VIZURI KAPUYA NA MUDHIHIRI)KIGEZO HATA WAKUBWA WANAPATA AJALI ?
ReplyDeleteJe, hao waliojeruhiwa walikuwa wamevaa Seat Belts?
ReplyDeletembona habari hazieleweki,,,wamekufa watatu au mmoja, anyway Professor ugua pole, mungu akujalie.
ReplyDeletewe unauliza waliojeruhiwa walikuwa wamevaa seat belts? ukishapata jibu, litakusaidia nini, ajali ndo ishatokea, kinachotakiwa sasa kuwaombea majeruhi wapone na kuombea faraja familia ya marehemu. Unauliza hivyo, we mtu wa usalama wa barabarani,,kaongeze alama na mataa huko vijijini, upunguze ajali,usianze kuuliza maswali yasiyo na msingi hapa...we hapo ulipokaa kwenye mtandao umefunga seat belt?
ReplyDeletePOLE SANA MHESHIMIWA KAPUYA,MTU WA WATU.JAMANI VIONGOZI WANAPASWA KUJIFUNZA KWA KAPUYA,AJALI YAKE IMEWAGUSA WATU WA KADA MBALIMBALI NA KILA MTU ANAMPA POLE NA KUMUOMBEA HERI HII NDIO RAHA YA KUWA MTETEZI NA MTU WA WATU..SASA WALE VIONGOZI WANAOJALI MATUMBO YAO WAANGALIE MFANO HUU..MBONA MTU MWINGINE AKIPATA AJALI WANANCHI WANAMLAANI NA KUMUOMBEA KIFO LAKINI INAKUWA TOFAUTI KWA MTU KAMA KAPUYA?? JAMANI SAUTI YA WATU NI SAUTI YA MUNGU NA KWA MAONI YA WATU PROFESA KAPUYA UNAPENDWA...VIVA KAPUYA PONA HARAKA UENDELEE KULIJENGA TAIFA ACHANA NA HAO WANAUZA NCHI KUPITIA MAHOTELINI UINGEREZA....
ReplyDeleteWewe anon unaeshangaa mtu kuuliza kama majeruhi walikuwa wamevaa mikanda una matatizo.
ReplyDeleteUnanishangaza zaidi kusema kuwa eti .."kinachotakiwa sasa ni kuwaombea majeruhi wapone"Wewe chizi nini??Majeruhi hawaombewi wakapona bali wanatakiwa kupelekwa hospitalini haraka wapatiwe matibabu wapone.Maombi maombi,kazi kukariri tu.Kubwa ziiiiii!!!!Fyuuu(msunyo).Acheni imani za ajabu za kuombea watu wapone.Wewewewe!!NIKIKUKAMATA????
Nafikiri umefika muda wa kurekebisha barabara zetu za vijijini na watu kufuata sheria za barabarani. Poleni na ugueni pole majeruhi wote
ReplyDeleteHivi kwani huyu nae alisapoti ile hoja ya Mudhihir kule Bungeni Dodoma?
ReplyDeleteMweeh!