
dada mpita njia akishangaa kuona geti la bustani la mnazi mmoja likiwa limefungwa. walipa kodi wa dar wanalalamika kwa nini sehemu ya umma ifungwe wakati wote na kufunguliwa wakati wa sherehe za serikali pekee? wengi wanagoma kukubali kwamba hii inatokana na watu kutokuwa wasafi ama wastaarabu wakihoji endapo mababa wa jiji wana mgambo wa kukamata mama ntilie na gereji bubu watakosaje wa kulinda sehemu hizi??????
Hapo lazima pafungwe maana wakati mwingine Watanzania huwa hutuna ustaarabu. Kuna kipindi hapo watu waliweka sahelu ya kuvutia bangi, mailsiho ya mbuzi/mifugo na kuharibu hizo sanamu.
ReplyDeleteMimi nafikiri heri pafungwe hivyo hivyo
Mzee wa TBS
Kufungwa sio suluhisho, suluhisho ingekua wangekua wanaweka wana usalama kuangalia kwamba hio bustani inatumika kwa mambo ya kawaida na sio ya haramu.
ReplyDeletePakifungwa huna unachofundisha chochote kuhusu ustaarabu wa mtu kwani kama mtu sio mstaarabu atafanya mambo yake kwengine.
Ingekua pana ulizi na sheria basi watu wangejua maana ya ustaarabu.
Pamefungwa, kwahio mtu asiye mstaarabu ataendelea kufanya mambo yake pengine.
Ukiwa na kisu unajua kina kata lakini humkatazi mtu kukitumia bali unamuonyesha jinsi ya kukitumia, akishajua matumizi yake ndio atafaidika.
Turudi kazini kwetu tukashughulikie BUZWAGIIIIIIIIIII
ReplyDelete....
Mbunge Mudhihir kupelekwa nje ya nchi kuwekewa mkono wa bandia
2007-09-21 09:08:36
Na Said Hamdani, PST Lindi
Serikali inandaa utaratibu wa kumpeleka nje ya nchi Mbunge wa Mchinga, Bw. Mudhihir Mudhihir (59) kwa ajili ya kuwekewa mkono wa bandia.
Bw. Mudhihir kwa sasa anaendelea kupata matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Taasisi ya Mifupa (MOI).
Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Bw. Martin Shigela aliyasema hayo juzi alipokuwa akitoa salamu kwa wakazi wa Jimbo la Mchinga baada ya Balozi wa Uingereza nchini, Philipo Palmo kutembelea wilayani humo.
Akitoa salamu hizo kwa wananchi wa kijiji cha Mchinga 2, aliwaambia hali ya Mbunge wao inaendelea vizuri.
Bw. Shigela alisema pamoja na hali ya kiongozi huyo kuendelea vizuri, mipango inafanywa ya kumpeleka nchini Ujerumani kwa lengo la kuwekewa mkono mwingine wa bandia.
Aliwaomba wananchi kuendelea kumwombea dua njema kiongozi huyo aweze kupona haraka na arudi na kushirikiana nao katika ujenzi wa taifa.
Bw. Mudhihir alipata ajali baada ya gari alilokuwa akiendesha kuacha barabara na kupinduka mara tatu.
Sehemu ya umma au "public place" hapatakiwi pafungwe. Ni kazi ya halmashauri ya jiji kuhakikisha kuwa bustani hiyo ni safi na inatunzwa katika kiwango kinachohitajika.
ReplyDeleteWewe anony mvivu wa kufikiria hapo juu, hivi mtoto wako kama akishiba tuu anakunya kwenye chupi, utamfanyaje? Utamuweka na njaa au utamfundisha ajue cha kufanya kila akijisikia kunya? Mvivu wa kufikiri wee.
GOOD QUESTION!
ReplyDeleteHao askari wasio na haya wanaowekwa kukimbiza kina mama wanaotafuta ridhiki zao,ndo wangepewa kazi ya ulinzi na usafishaji wa bustani hii.Ni aibu kubwa sana kuona hilo kofuli hapo mlangoni masaa 24 kwa siku!
Halafu siku za mbeleni utaona panauziwa mwekwezaji,hapo basi ndo mlipa kodi pole.
HAPO PAFUNGWE HADI KITAKAPOKUJA KIZAZI KINACHOJUA USTAARABU NI NINI.
ReplyDeleteSIKUBALIANI NA WEWE ANONYMOUS UNAYESEMA WAWEKWE WANAUSALAMA, KAMA HUJUI USTAARABU WANAUSALAAMA WAWEKWE KUFUNDISHA USTAARABU?
ANGALIA UPANDE WA PILI JINSI HAO WASTAARABU WAKO WAVYOUTUMIA VIBAYA.
HAKUNA KUFUNGUA HUO MLANGO HADI USTAARABU UCHUKUE MKONDO WAKE.
HEBU ANGALIA PALE MAHAKAMA YA MWAMNZO KARIAKOO, UKARABATI UMEFANYIKA NA NJIA YA WAENDA KWA MIGUU IKAWEKWA NZURI TU, LAKINI MATOKEO YAKE WASTAARABU WENU WANAPITA JUU YA MAJANI NA KUACHA KUTUMIA NJIA AMBAYO KODI YA WA'CANADA IMETENGENEZA.
NARUDIA FUNGENI HADI HAPO WATU WATAKAPOJUA USTAARABU.
we anonymous unayesema wawekwe wana usalama kwa kulinda hili mtu asichafue ni upotezaji wa hela tu hapo ni kufunga yu mpaka mbongo aelewe nini maana ya ustaarabu,watu wazima hakuna kabisa ustaraabu mpaka muwekewe polisi?mfano mzuri ni uwanja mpya wa taifa jinsi wabongo walivyo ufanyizia.
ReplyDeleteMwee!!! we Anon hapo juu ulitoka usingizini ndio ukaandika ama vipi? kufungwe hadi kitakapo kuja kizazi cha wastaarab!!! nani atawafundisha ustaraab?.. hebu jitume, changamsha akili ufikirie kidogo mana dah!!! unatia aibu bora unyamaze kama huna lakusema.
ReplyDeleteHiyo sehemu ifunguliwe kuwekwe ulinzi, tena isiwe kero kwa raia bali kulinda ustaarab wa hilo eneo..
taratibu tutaelewa tu.. mtoto huanza kutambaa ndo akasimama dede.
niko upande wa wasemao PAENDELEE kufungwa kwanza...wengi wetu hapa mjini will take decades to at least introduce us to ustaarabu...look at public toilets...halafu kuweka askari polisi kulinda maybe it might work...sidhani kama kuna mtu atachutama kushusha mzigo au kwenda haja ndogo in the eyes of 'mzee' lakini come usiku watu watachafua tuu!...kazi ni kubwa sana, it is easier said than done...patavamiwa pale na jamaa wanaojua biashara aisee babaangu iwe vurugu za chipsi na mishkaki, "vigrosari"...mafundi viatu, vioski vya 'disableds', mafundi saa...authorities know that they do not have teeth no wonder it is closed for public...look at swimming club kule ferry, the place is surrounded by hata sijui niwaite kina nani wale...na hapo ni mbele ya ikulu...watasogea mpaka watafika ocean rd. hospital wale...DAR is crowded...some places need to be out of bounds...IF POSSIBLE KUWE NA PERIMETER FROM CITY CENTRE TO SOMEWHERE IWE KAMA HUNA SHUGHULI HUINGII WITHIN...itapunguza vibaka, wezi wa car parts, unnesessary crowds, kelele pia mji utapendeza...mjini wamejaa watu ambao eti ofisi ziko mikononi...wanakuju kutia wingi tu...ineffective, useless...hawa ndio wataoharibu hizo so called mnazi mmoja gardens
ReplyDeleteHATA KAMA NIMETOKA USINGIZINI KAMA UNAVYODAI ANONYMOUS HAPO JUU, BADO NASISITIZA KUWA PAFUNGWE HADI HAPO KIZAZI CHA WASTAARABU KITAKAPOKUJA.
ReplyDeleteHEBU ANGALIA MZUNGUKO WA BARABARA YA MSIMBAZI NA UHURU WASTAARABU WAKO BILA AIBU PALE NDIYO WAMEFANYA NI CHOONI KWAO, SEMBUSE HAPO?
PAFUNGWE!!!!!!!
Paachwe wazi tuwafundishe watu wanaokunya hovyo kuwa kuna mahali maalumu pa vinyesi. Sasa kufunga kutatufundisha ustaarabu lini? Lazima tujifunze kuwa wastaarabu kwa kujifunza namna ya kutumia bustani (parks) ipasavyo....!! Wanaopachafua wapewe adhabu ya kupasafisha..ndo watajifunza..na hao askari jiji waache njaa zao....!!
ReplyDeleteKofuli litoke,tufundishane ustaarabu,askari waache kuzurura na kunyanyasa raia wasio na hatia na badala yake waende kulinda na kusafisha bustani hiyo.Katika hali hii kodi za raia haziishi kusiko julikana.
ReplyDeleteUstaarabu hauji wenyewe bali kwa mafunzo, mifano na msisitizo.
Raia waBongo wana kila haki ya kufaiadika na ardhi yao bila bughudha!!!OK?OK..!
kwenye kutoa maoni humundani hakuna ustaarabu itakuwa kwenye hiyo bustani ?
ReplyDeletedada umependeza, hiyo kama sio suruali ni nyanya pensi.
ReplyDelete