mdau dk. narman wa kitivo cha sayansi ya majini cha chuo kikuu cha dar katuletea picha hii ya wakazi wa kitongoi cha paje huko unguja wakijipatia mafuta toka katika mzoga wa nyangumi uliokutwa umepwelea pwani ya hapo. inasadikika mafuta hayo ni dawa ya maradhi kadhaa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Jamani, hawa watu wanafahamu huyu Nyangumi amekufa kwa tatizo gani? Inaweza ikawa hatari sana kufaya kitu kama hiki ukizingatia kuna kasi kubwa sana ya magonjwa kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu "zoonotic diseases" sasa tukipata na ya samaki, sijui itakuwa vipi. Wataalamu wa viumbe wa majini inafaa kuwahi kwenye matukio kama haya kwa lengo tu la kuhakiki kama wafanyacho watu kama hawa ni salama kwa afya.
    Ni mtazamo tu...msinizodoe jamani

    ReplyDelete
  2. wangekula hata nyama kwani samaki hachinjwi. Huo sio mzoga...kwani samaki wote wanakufa kifo hicho hicho jamani

    ReplyDelete
  3. NG'OMBE alileta Rift Valley.

    SUBIRIA huyo samaki kama hujasikia OCEAN VALLEY mimi nimejitoa.Yaaaaee angalieni ukilionja tu hilo lijinyangumi utashangaa walegea unakuwa MDEBWEEEEEDO

    ReplyDelete
  4. Siku huzi nyama ya mzoga inaitwa mafuta. Wabongo kwa terminolgies, hawajambo!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  5. Tobaaa!
    Na Ramadhani yote hii watu wako katika mzoga. Halafu visiwani!

    ReplyDelete
  6. wapemba bwana nishai tupu!!!!!mpaka mizoga kha!!!!

    ReplyDelete
  7. dr Narman mtaalam wa maswala ya sayansi ya majini, labda wamefanya test, i don't know

    ReplyDelete
  8. MWEZI WA TOBA HUU... NA WANAOSAMBAZA MAGONJWA WANAJUA IMANI ZETU.

    ReplyDelete
  9. Huu ni ulaku tu. Mbona Kikwete hayupo kwenye picha kuchukua mafuta ya samaki kama ni dawa. Nyie mnataka kutumaliza tu. Au ni watu wa ughaibuni ndiyo waliosema kuwa mafuta ya mzoga ni dawa. Kaka Michu, tusaidie, kwani twaangamia. Mafuta ninayojua mimi ni yale ambayo yamekwisha kupimwa na kuhakikishwa kuwa ni salama kwa binaadamu na sio hayo. Jamani huu ni ulaku tu wa watu.

    ReplyDelete
  10. Ndugu zangu hamujui huyo Nyangumi amekufa kwanini- Ni kutokana mazozi ya kijeshi yanayofanywa na mataifa flani kwakutumia technologia iitwayo SONAR (SOund Navigation And Ranging)—or sonar — is a technique that uses sound propagation under water (primarily) to navigate, communicate or to detect other vessels. There are two kinds of sonar — active and passive
    Hivyo basi technologia hii huwadhuru sana Nyamangumi na samaki wengine wakubwa waishio kwenye kina kilefu cha bahari - Mataifa hayo hayawezi fanyia majaribio kwenye bahari walizopakana nazo kwania wana jua matatizo hayo - Huyo profesa anasemaje?

    Poleni - sijambo la kufurahia
    KUNTA-KINTE

    ReplyDelete
  11. Ujinga mtupu mafuta yako wapo hapo? yaani "FAT" ndio matibabu au kuongenza ugonjwa tena mzoga??? Halafu eti bongo New York..mmh

    ReplyDelete
  12. "Sayansi ya majini" ni kitu gani?

    Utotoni niliwahi kuambiwa kuwa majini ni viumbe vya kufikirika ambavyo vinaweza kutumiwa kumletea mtu madhara. Je kuna sayansi yake? inasomewa wapi?

    ReplyDelete
  13. Tafsiri ya Kibudu please!!! Maana huyo ni kibudu au kibudu kwa mnyama aliyechinjwa???

    ReplyDelete
  14. Hello! Kichuguu nathani wewe unataka kuchekesha watu, sayansi ya majini it means that ni sayansi ya ndani ya maji. hebu jaribu ku post ujumbe wenye maana and usipotezee watu muda wao.

    ReplyDelete
  15. sayansi ya majini nahisi imetafsiriwa toka kwa maneno ya kiingereza AQUATIC SCIENCES AMBAPO HUMO IKO MARINE SCIENCES,sio majini unayoyafikiria wewe kichuguu.Haya na wewe kichuguu inakuwaje unaweza kuandika? ni miujiza kwa vile twajua kichuguu ni nyumba ya mchwa iliyojengwa kwa udongo!

    ReplyDelete
  16. Jamani mbona IPP inasema nyangumi huyu alikuwa DAR.
    Re: http://www.ipp.co.tz/ipp/itv/2006/01/15/57852.html

    ReplyDelete
  17. LABDA MICHU UNGEWEKA WAZI KUWA HILI TUKIO LILITOKEA LINI.MANA NAONA KAMA VILE HII NI PICHA KUTOKA MAKTABA,NI TUKIO LAAA HIVI KARIBUNI KWELI?
    I DOUBT.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...