leo kwenye bustani ya gaden ya mnazi mmoja kulikuwa na hafla ya siku ya kuukemea umasikini na kuhamasisha njia za kuuondoa na kusherehekea malengo ya milenia

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Kukopa si wanakopa wenyewe? hakuna anayewafunga kamba na kuwapeleka WB au IMF. Sasa ukikopa ndo unakimbilia kukemea deni? LIPA. Siku hizi hata siona mikopo hii wanafanyia nini. Enzi za Nyerere hata nilikuwa napata daftari, kalamu, na vitabu bure. nilipoenda secondari angalua nilikuwa narudishiwa nauli yangu na kutibiwa bure. Hata viwanda vilijengwa mabomba ya maji ya kijiji yalikuwa karibu. Siku hizi MWE. Siku hizi nimerudi tena kuchota maji mtoni. Mikopo ni ya kuongezea mishara ya Wabunge tu. Mimi kamwe SITOWASAIDIA KUKEMEA MADENI!!!!!
    Kumbuka Tanzania ilichaguliwa kama nchi zinazostahili kufutiwa madeni just a few years ago-kama sikosei last year. Na kama sikosei ikawa imefutiwa kiasi kukubwa. Sijui kwa kufanyiwa hivyo wakaleta maendeleo gani- au ndo walicharuka na kukopa hata zaidi? Wadau nisaidieni hili.

    ReplyDelete
  2. Yaani huu ni ufinyu wa mawazo, madeni mnakopa nyinyi harafu mnataka yafutwe? mnafikiri kuna dezo? dawa ya deni ni kulipa!

    Unavaa Tshirt eti unasherekea malengo ya milenia, ama kweli bongo!

    Au mngeonyesha mmefanyia nini hizo hela, hapo mngekuwa na hoja!

    ReplyDelete
  3. Hivi mnakemea umaskini kwa Jina la Yesu?Kufanya matamasha tu hakutasaidia kutokomeza umaskini.Hii kitu inahitaji uwajibikaji sio kuomba kufutiwa mikopo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...