kocha wa taifa marcio maximo na msaidi wake ittamar wakiwapa lekcha wachezaji wa timu ya taifa ya bara kilimanjaro staaz wakati wa tizi jioni hii neshno

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 23 mpaka sasa

  1. Mimi naunga mkono suala la kuwa na kocha wa kigeni lakini swali la kujiuliza mjomba ana vyeti vya kueleweka maana nobody knows nini alifanya kaka michuzi tutafutie habari zake zaidi huyo kocha maana hatumjui? Huyo msaidizi wake nae nafikili ni kutoka brazil sasa mbona kazi hiyo wapo wazalendo wanaweza kufanya nafikili ni kama kula pesa ya walipa kodi wa bongo bila sababu.Je kama ni kipimo cha huyo mjomba ni mashindano yaliyopita ktk historia ya tanzania haijawahi kutokea rais kuwa makini na timu ya taifa kama mwaka huu sasa hatujaona kipimo chochote au kitu chochote alichofanya huyo mheshimiwa.Kama ni hamasa hamasa ingekuwepo hata yeye kutokuwepo, nafikili muda umefika kuangalia umuhim wa huyo mjomba na mshahara anaolipwa kwani hiyo pesa ingeweza kusaidia sports development mashuleni. Na pili hao wasaidizi ni wa nini nafikili kama ni ma physician mbona mziray ndio alichosomea kuna umuhim wa kuheshim walimu wote kwanza. Mimi nafikili hiyo hali ya huyo mkambungu kuja na group lake toka kwao ni kama kugeuza bongo mradi na kujitengenezea good retirement swali kwani walim wa Tanzania hawataki good retirement kama mjomba anavyojikusanyia. Mimi nafikili kuna walimu wengi wa Kitanzania wazuri tu na hiyo pesa anayolipwa huyo mheshimiwa na group lake ingetumika kununua vifaa vya michezo kwani kuna baadhi ya shule hazina vifaa kabisa na huyo mjomba anachukua pesa nyingi.Kuna umuhim wa Watanzania kujua historia ya huyo kocha maana wengine hatujui historia yake na nini kafanya ktk ulimwengu wa soka na ni timu gani kafundisha.Mimi ninachosikia ni ulimbukeni wa wabongo kuanza kumsifia wakati sijaona alichokifanya.Ukweli ni kwamba alichokifanya bongo ni kututoa kwenye kichwa cha mwendawazimu na hakuna alichofanya zaidi ya hilo na swali la kujiuliza ni hii hamasa ya mpira sasa ndio imesaidia, dont get me wrong sitegemei miujiza nafikili nyinyi ndio mnategemea miujiza ambayo haionekanni na kutumia hamasa ya wabongo kwenye michezo kutunyamazisha.Swali kwani timu kwa mara ya kwanza ilipoingia kwenye mashindano ya african cup miaka ile kulikuwa na kocha wa kigeni? Nafikili ingekuwa busara kama tungeanza na kocha wetu kwanza do not underestimate our intelligency man.Ukichukulia mfano na nchi kama angola yenye watu kidogo na sisi tuna watu wengi lakini hatujafanya vizuri pia angola miaka 26 ya vita ya wenyewe kwa wenyewe lakini wanafanya vizuri nafikili hii ni kutokana na maandalizi ya timu hasa ukichukulia wa angoalaaa walikimbia kwao na kuzaa portugal kisha watoto kuwa developed ulaya na vifaa ndio maana mabadiliko yanaonekana, sidhani huyo mkambungu kama atafanya mabadiliko yoyote kama foundation ni poor.Nafikili washikaji tujiulize mambo mengi kabla ya kupelekwa kama kondoo. Pia mchezo kama soka bongo ni opium of the masses, hivyo kufanikiwa kwetu ndio furaha kwetu sote.Washikaji tujadili hii kiundani??????????????

    ReplyDelete
  2. wapo pamoja kwel? TATIZO NG'ENG'E MWANAWANE, mmh! yangu kipanya mie macho!

    ReplyDelete
  3. Kwanza napenda nianze kwa kumuunga mkono Gangwemsemakweli kwani huyo mjomba anatakiwa ajue kuna new generation on waiting, na maana ya new generation kusoma ili kupokea ngoma ngumu!sasa akichemka na hii chalenge ambayo ni rahisi he can go to hell. Na kuacha pesa ya walipakodi wa bongo.

    ReplyDelete
  4. Kweli gangwe lakini weweweeeeee!!!kamaa kweli anakula kiulaini hapa kwetu mbona hata timu halikuwa hana pale kwao, na hao wajomba aliokuja nao kaokota mitaani kishikaji tu! nafikili sasa tutafute makocha wanaoeleweka kama Kabila alipomchukua yule mshikaji ambae alikuwa anafundisha cameroon. Sasa huyo maximo kafundisha wapi kaka michuzi swali hilo?

    ReplyDelete
  5. Gangwe mshikaji alikuwa football tech director kwao pia kakochi Scotland bofya hapa utaona habari zake ila alilala mbele na record ni two win three draw na kachemsha tatu=http://thescotsman.scotman.com/sport.cfm?id=1139092003 ujaji mwenyewe.

    ReplyDelete
  6. Hivi huyo kocha wa Taifa anaongea Lugha gani??kama ni English je kuna mkalimani kutafsiri kwa wachezaji wa Taifa Stars nini anachofundisha??au anachosema??maana tusije walaumu serikali kutumia pesa nyingi kunoa Taifa stars lakini maendeleo hakuna na wanaishiwa kufungwa na safu ya ushambulizi hakuna kitu,Huwezi kuona labda ufanisi katika yanaongelewa na kocha hayafiki kwa mlengwa??

    ReplyDelete
  7. Simshupalii mjomba lakini la kujiuliza ni kuwa alitaka wachezaji waende kujifunza Brazil wakaenda, akataka Denmark wakaenda sasa walichojifunza hakieleweki na pia katimua timu yote iliyotumia pesa yote ya walipa kodi umuhim wa hizo safari kichaa kama watalii uko wapi na nini madhumuni ya safari hizo!Inashangaza na hakuna kinachoeleweka,kaka kachala washikaji sidhani kama hawaelewi na yeye kama ni kocha mzuri angelijua hilo kwani kama wachezaji hawaelewi unachoongea na pia hawapo tayari wewe kuutumia miili yao ata ukitumia kitabu cha ukocha kilichoandikwa na maprofesa mia mbili hakuna mafanikio.Swali kwanini alitaka timu iende kwao ?na denmark ? nini kilichofanyika na maana ya program ni kwa ajili ya long term plan sasa yeye kaunda timu mpya kabisa hebu wadau nijibuni hizi safari zimesaidia nini kama si kwenda kula raha kwao na kutalii? Alafu inaonekana amekamata umbea kwani kwa kuongea na wachezaji wachache waliocheza timu ya taifa na nikiwa pia mmoja wa wachezaji wa zamani nafikili hao kina kayuni na kujikweza kwao waende zao hakuna wanachofanya zaidi ya kula pesa ya walipa kodi.Vijana wanakuja kaeni chonjo tunataka ukweli na kama mtu anachemka go to hell!Bongo ni yetu sote na nyinyi mlikuwa vijana once na ndio maana watu wakawapa nafasi,washikaji we are the future now tuzidi kujadili ili.

    ReplyDelete
  8. Mpenda soka nashukuru kaka nimebofya hapo uliponambia nimeona alikuwa anafundisha livingstone Scotland ila cha kushangaza hata mwaka hakumaliza na sababu hazieleweki tujitose kumpa ukweli hamna kuogopa kwani ni uwazi na ukweli na hatuvunji sheria mjomba haingii kwenye kichwa changu kaka.Labda tukifanikiwa kupita kwenye world cup lakini kuna baadhi ya wachezaji wa zamani ni muhim awahusishe kaka unamkumbuka Salvatory Edward, nani kaona kiungo kama ile ktk bongo, kumbuka michezo ya umiseta jamaa alivyokuwa anakamua,kumbuka alivyomtesa George Weah ile siku taifa lakini kwa sasa no body cares nasikia yupo Oman anacheza mpira wa kulipwa pale unahitaji mtu kama yule kuwaambia vijana ukweli. Lakini wao walimchukua Renatus Njohole na wengine Rena ni bishoo na ktk vijana wengi tuliosoma nae nobody likes him ni mtu wa kujisikia.Ila Salva ni diamond for the country ngoja sasa tuongee hilo.Nashukuru mpenda soka kwa mawazo yako.

    ReplyDelete
  9. Kaka michuzi baadhi ya wana habari hamtutendei haki walipa kodi kwani hamuulizi maswali ya msingi huyo mjomba anatakiwa ajieleze vizuri what went wrong last time na nini kifanyike sasa? wanahabari wakienda kuuliza wakipewa soda na vyuku wanatulia kama cucumber inayosubiri kuwekwa kwenye kachumbali.Huyo mjomba aeleze kwa nini alishindwa kufanikiwa na anafikili atafanikiwa this time? kauli yake itamvisha kitanzi mwenyewe mimi staki kufundisha wana habari kazi yao ni sawa na kufundisha samaki kuogelea!do us a favour man make him explain all the time.Hivyo ndio pessa ya walipakodi itamuuma na pia atapata uchungu wa bongo.Sisi wabongo ni wakarim lakini sometime enough is enough.And we need to learn to hard enough ndio maana tunapelekwa.Sema nao Gangwe!

    ReplyDelete
  10. Angalia Walichotufanya Wanigeria mwaka 1980. Nigeria 3 Tanzania 1.http://www.youtube.com/watch?v=tggt9Ply9lc

    ReplyDelete
  11. Marcio Maximo, a Brazilian, appointed by the Government of Tanzania as the Head coach of the Tanzania National Football Team. He will be responsible for the Taifa Stars.

    His appointment follows a promise made by the President of Tanzania, Jakaya Kikwete to ensure improvement of football in the country.

    He had previously coached Livingston Football Club in Scotland in 2003/2004. He was also a member of Brazil's youth coaching staff (under-17 and under-20) in 1992 and 1993.

    ReplyDelete
  12. nyie waswahili kwa kulalamika. http://thescotsman.scotsman.com/sport.cfm?id=1139092003

    ReplyDelete
  13. Huyu mjomba hajui kuchagua wacheaji na ana kiburi cha wazungu koko. Zambia itatufunga kama watoto, tusubiri mtungi nne.

    ReplyDelete
  14. Salama Wazee? Mimi bwana sina kabila. Lakini huwa nachukia sana mtu anapofanya maamuzi yake kwa kuhusisha Ukabila. Nadhani wadau wezangu hamjaona kinachondelea hapo TFF. Kwanza siamini kama Maximo huwa anachagua hao wachezaji kwa upendo wake mwenyewe au kuna watu wanamfanyia hiyo kazi ya kuchagua. Pili nina utata na uchaguzi wa Mukebezi. Je ana elimu ya kutosha ya Kumanage team?? Au ndio ""Ukaijage na Umukebezi"" umeshaingia??. Timu hii imejaa ""Wkunyumba watupu"" na hata wengine wanawatoto wao ndani yake. Please "Mshomire" is 2007 msije mkatuletea yale yaleee ya Wizarani Kuanzia Waziri hadi Mfagizi kutoka kuleeeeeeeeee karibu na Uganda. Check this:
    Florian Kaijage (Afisa habari TFF)
    Denis Mukebezi ( Manager wa Team)
    Leopold Mukebezi (rookie)
    Frank Mutego ( Mwanawange)
    Mokili Lambosi (ohh God )
    Vircent Barnabas ( Kagera)
    Frank Mutego ( kagera).
    Na wengineo ambao kimajina huwezi kuwatmbua usije kushangaa timu nzima ni Iweeee!! lakini jina la timu ni ""Yesuuuu na Maria"" Wapi na wapi!!
    Dont get me wrong!!Kama wanakiwango na Elimu ya kutosha na experience kwa manager basi sio tatizo lakini kama kuna mkono wa mtu hapo please oneni aibu. Tuache ushamba wa kizamani wa kujazana sehemu moja kisa kuna Ulaji. This 2007 people.

    ReplyDelete
  15. Wewe mshikaji unaesema watanzania tunapenda kulalamika nafikili unaongea kitu ambacho hukijui kutaka kujua ni msingi na huyo mjomba hata kwenye net habari zinazoonekana ni mbili ya Tech Director kwao na ya kufundisha Livingstone Scotland, nyingine zote ni za bongo is he making is name from bongo?

    ReplyDelete
  16. mh, vigimbi miguuni!

    ReplyDelete
  17. Wajomba naomba kuwakilisha maana naona maoni mengi yanatolewa na wasiojua kitu katika huu ulimwengu wa soka.
    Kwanza kumbukeni nchi nyingi za Africa haziwezi ku afford kumlipa kocha wa kigeni anayefundisha timu kubwa Ulaya. Kama hivyo vi Tsh. milioni mia sita mnapiga kelele naona hiyo sasa sijui huyo "Sir.Alex Furgason" akija sijui itakuwaje. Kumbukeni huku nje kocha wa College tu anavuta mkataba hadi wa USD. milioni kumi au tuseme milioni kama mbili kwa mwaka. Hiyo inaonyesha hakuna kocha yeyote wa nje mwenye uwezo wa kufundisha hata College anaweza kuacha mshahara mkubwa ili aje kufundisha nchi kama Tanzania. Unless otherwise, atakuwa ana nia ya kutafuta jina zaidi katika proffesional (CV) yake lakini sio pesa.Ikumbukwe Maximo angeweza kwenda USA na kufundisha College moja na kuvuta mshiko kuliko huo mnaopigia kelele.
    Pia ikumbukwe hadi Wazungu wampe timu Mbrazil lazima walikuwa na imani nae. Na kama ukisoma vizuri hiyo habari ya timu ya Livingstone utaona kuwa Maximo aliamua kuondoka mwenyewe na hukuwa Sucked!! Kitu ambacho kocha yeyote mwenye busara anaweza kufanya kama iakiona hatimiziwi mahitaji yake au hapewi uhuru wa kazi yake. Si mnakumbuka yaliyotokea Dar. Young Africans kwa Micho??.
    So Wajomba tuache kupiga kelele "The guy is doing a good job". Angalau sasa vijana wengi wanafanya soka ajira instead of going to rob and kill people in the streets. Anafanya kazi yake katika mazingira magumu ya Bongo na naweza kufanya hivyo kwa sababu tu amekulia Brazil, kama ingekuwa Mzungu angekuwa maeshatimua. Si mnakumbuka yule Mjerumani aliyeletwa na FIFA na mshahara mnono wa FIFA lakini akaishia kuingia mitini. Go ahead Maximo, Do your Job!!

    ReplyDelete
  18. Kwanza mjomba hapo juu jifunze kiswahili na sio kuongea maneno kama unaharisha.Watu hawapigi kelele wanachangia hoja nini ulichoongea hapo juu ebu tuambie kama unajua mshahara wowote hau ndio tabia ya kibongo kujifanya kujua!watu hawajui huyo mjomba analipwa shilingi ngapi.Inaonekana wewe ni group la watu wanaoenda kusoma ulaya na sisi walalahoitunaumia na shule zetu za mitaani.Kama unataka value for money u need to ask.hivyo kama una mchango shut ur gob.Watu wanataka value for money idiot.Pia mjomba unatakiwa kujua kujadili ishu ndio ukweli upo na si kuongea none sense !!Unaongea nini kuhusu hiyo Timu ya Livingstone nani anaijua angefundisha timu ambayo imepata nafasi au kufanya kitu kabla.Sasa wewe unasema kulipa kocha ni gharama nani kakwambia na unajua mshahara wa huyo mkambungu.Pia wewe kirusi acha kunyenyekea wazungu na kuwaona ndio wanajua,unaishi dunia gani mkambungu wewe.

    ReplyDelete
  19. Huyo anonymous wa 3.57 acha kujipendekeza ongea ukweli maaana inaonekana huelewi nini unachoongea hebu tuambie huyo jamaa mshahara wake ni shilingi ngapi? Pia hao makocha unaowataja wanalipwa shilingi ngapi?unaonekana huelewi nini unachoongea.Tujadili ishu na sio kulopoka kama tunataka maendeleo ya haraka basi tungechukua mwalim mzuri na sio huyo wa kubagain acha kuongea utumbo kaka.Lete point nyingine ? Watu hawajasema asifanye kazi yake afanye ila ajue kuanzia sasa wapenda soka hatuta nyamaza ni watu kama werwe wanakubali kila kitu.

    ReplyDelete
  20. Kwa taarifa yako michezo ilikuwa ni pesa bongo toka zamani na ni sera za michezo hazina kichwa wala miguu na washikaji wanaanza kustukia maximo hamna halicho fanya kama livyosema gangwe katutoa kwenye kichwa cha mwendawazimu tu. na hiyo kazi ya kufundisha kilimanjaro angemwachia kocha mzalendo ni tamaa au nini?

    ReplyDelete
  21. Wewe anonymous hapo juu unayelalamikia ukabila, kwanza majina mengine umeyarudia, ili waonekane wengi, siyo?

    Hivi huwa nawashashangaa baadhi ya wabongo: Hivi mna tatizo gani na watu wa Kagera? Yaani wakiwepo watu watano kwenye institution yenye watu zaidi ya 100 tayari ni ukabila? Mbona hukutoa statistics za watu wa makabila mengine, ku-justify kuwa wahaya ndio majority hapo tff?

    Acheni inferiority complex, jadili issue zenye maana kwa timu ya taifa. Kwanza nani kakwambia Kaijage anaweza kumchagua Manager wa timu? Yeye si ni afisa habari tuu.?

    Mulokozi.

    ReplyDelete
  22. Kwanza nianze kwa kuungana na Mulokozi hapo juu hii tabia ya ukabila sio bomba bongo hatuna hiyo issue,kama wajomba wamejaa fat then tujadili wanachochemka na si ukabila wao.Mimi binafsi simuungi mkono mtu kama Sunday Kayuni ni wazee wanaong`ang`ania madaraka lakini hamna anacho fanya zaidi ya majigambo na kujisikia, he needs to go! au labda hana ajila nyingine zaidi ya hiyo.Alikuwa na timu miaka mingi lakini nini kafanya kwa ajili ya timu ya taifa god knows! amebakia kusengenya vijana wanaotaka kichwa yake.Tunahitaji nguvu mpya hapo tff, na wapiga kura safari hii wanatakiwa wajue nini maana ya hizo kura wanazopiga sio kuwa kama mapimbi halafu tunabaki kulaumiana ila mimi naamini uchaguzi ujao wa tff ni patashika nguo kuchanika hivyo chukueni vyenu mapema !!!!

    ReplyDelete
  23. Nasikia timu yetu imefanya vizuri hivyo ndio tunataka na isiwe tu sababu ni kujipima nguvu. Hta kwenye mashindano yajayo iwe poa pia hapa tunapata raha!wala hatuna cha kusema maana mimi naamini Zambia wana kiwango kizuri cha soka kuliko sisi ni nzuri for a change lakini ngoja tuone ikifika wakati wa kutafuta nafasi ya world cup ngoma itakuwaje maana hicho ndio kipimo na kila la kheri Taifa Stars sio kwamba watu tunammind maximo ila tunahitaji mabadiliko ya kweli ambayo yaendane na nguvu mpya kasi mpya..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...