JK LEO AMEMTEUA PROFESA BENNO NDULU KUWA GAVANA WA BENKI KUU, NA DK. ENOS BUKUKU ALIYEKUWA KATIBU MKUU WIZARA YA MIUNDOMBINU ANAKUWA NAIBU GAVANA MKUU AKICHUKUA NAFASI YA PROF. NDULU. YEYE DK. BUKUKU NAFASI YAKE INACHUKULIWA NA MH. OMAR CHAMBO ALIYEKUWA NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA MIUNDOMBINU.
AKITANGAZA UTEUZI HUO DAKIKA CHACHE ZILIZOPITA HUKO IKULU MTAA WA MAGOGONI, DAR, KATIBU MKUU KIONGOZI MH. PHILEMON LUHANJO KASEMA KWAMBA JK 'AME-REVOKE' (OYAAA! MSAADA KWENYE TUTA, TAFSIRI YA NENO 'REVOKE' NI NINI?) UTEUZI WA MH. DAUDI BALALI ALIYEKUWA GAVANA WA BENKI KUU ANAYESEMEKANA YUKO NJE KIMATIBABU....
Misupi mbona muda mrefu watu tulikuwa tunajua kuwa Bilali siyo gavana?
ReplyDeleteSema tu rais wetu naye anachukua muda mrefu kufanya maamuzi sijui ana tatizo gani? Au ndiyi kashfa za BOT ndizo zilimfanya achelewe?
Kwa wanaofuatilia kwa ukaribu wa watendaji wakuu katika serikali ya Kikwete, hakuna mtendaji serious na asiyedanganywa na vi-10 per cent kama bwana Bukuku. Ni mtumishi mwaminifu sana. zungumza na watu wa pale miundo mbinu watakuambia. He is the first in office, and he is the last to leave the office. Insiders say that at times he leaves his office after mid night.
ReplyDeleteBenki kuu kaeni chonjo. Mtaona mambo yatakavyobadilika hapo. Bukuku inaonekana ana maadili sana ya kazi. HONGERA JK KWA UTEUZI HUU.
Kwa uteuzi huu inamaana Balali sasa hata kama atapatikana na tuhuma za wizi katika hiyo ripoti ya BoT...hatua gani zitachukuliwa juu yake?...na kama akigoma rejea nchini akisema bado anaendelea na matibabu sijui itakuwaje!!
ReplyDeleteKujiuzulu kwake nadhan kutakuwa kumemwepusha na mengi...JK anatakiwa aseme kitu kuhusiana na riport na kuchukua hatua kali kama kuna ubadhirifu
Naomba niwe wa kwanza kuchangia!Kama Gavana ana soo halafu ukampa naibu wake nafasi si ni yale yale? Hivi kweli wabongo tutapona na gonjwa hili la uswahiba?
ReplyDeleteRevoke maanke ni kumuondoa mtu ktk nafasi(cheo chake) yake au kutomfanya mtu haendelee na position yake.in English Revoke meant(to cancel or make no longer valid)
ReplyDeletemichuzi utasutwa... REVOKE= kubatilisha au kutengua.. nadhani ndo maana yake kwa wale ambao tulikuwa tunamkimbia kifimbo cheza...
ReplyDeleteHaya naona JK kaanza kazi sasa lakini na hao wanaoteuliwa wanaweza majukumu?? .....
Ama kweli sie WADANGANYIKA, serikali ilikuwa inakataa kitu gani kuhusu ule waraka wa kujiuzulu kwa mheshimiwa Balali? Na vipi kuhusu tuhuma zinazomkabili... ama kweli hili ni changa la macho! Kumbe inawezekana kabisa kuwa mheshimiwa hajalazwa wala nini huko USA, anakula zake papai kwa kijiko ilhali sie tumebaki tunashangaa na kuvunwa kuwa anaumwa. Ama kweli inji hii ah! we acha tu. Fedha zote zile zilizotumika kufanya uchunguzi BoT zimekwenda bure, kwanini zisingetumika kununua dawa hapo Vigwaza au hata kujengea choo cha shimo cha shule hapo Hananasif!
ReplyDeleteaisee huyu prof ndulu namfahamu, ni chapa kazi vibaya sana.. hongera zake sana, hope kutakuwa na changes sasa bank kuu, sio mabadiliko tu bali mabadiliko ya mafanikio ktk nchi yetu. hapa jk nimekukubali kwa uteuzi wako
ReplyDeleteMichu, hii yote danganya toto tu. What we need to see is actions taken against waliotuhumiwa according to report. Asitupige changa la macho eti kabadili uongozi, walioboronga bado wanapeta .....fuga watu tujue kweli kunauwajibikaji
ReplyDeleteSasa kazi itafanyika.Hawa jamaa wawili nawakubali sana.Wakati Jk waziri wa fedha walikua timu moja katika kuanzisha mchanganuo kuundwa kwa TRA matunda yake yanaoneka.Mapato juu kila siku ila matumizi ya Gvt ndio soo kidogo.
ReplyDeleteSasa misupu jamaa watakaobainika kubanjuka na fedha za wavuja jasho pale BOT si wafungwe tu ka kina Babu seya ili iwe disiplini kwa waliobakia na katabia hako ka michongo ya kiaina.Hoja!
REVOKE:- Terminate,withdraw samahani na umaimuna wangu hapo kijasho kimenitoka kweli kweli
ReplyDeletewe anony hapo juu mbona unataka kutuchanganya unasema prof Ndulu ni mchapa kazi wakati tunaambiwa alikuwa naibu Gavana, alifanya nini wakati ule utumbo wa balali unafanyika,m tunapigwa mchanga wa macho tu hapo....ngoja tuone kama kutakuwa na jipya.
ReplyDeleteBalali amejiuzulu toka Dec. 02 2007. Serikali ilikuwa inakaa kimya tu, barua yake mbona watu tunayo.Ndulu amekuwa anaendesha BOT toka Balali aondoke, yaani amekuwa Gavana toka mwezi wa nane mwaka 2007. Wewe Michuzi ndio unatuwekea kuwa Breaking News leo 2008?
ReplyDeletehuyu JK naye aache kupendelea sana wakristo. Mambo gani haya?
ReplyDeleteMdahalo karibu
We anon wa pili kutoka mwanzo, kukaa muda mrefu ofisini haina mana ndio kuw amfanyakazi mzuri! huenda anakaa muda mrefu hivo kwa sababu hajui anafanya nini, manake mara anshika hiki mara kile au pangine anachelewa kondoka ili kufanya dili zake chafu kukiwa hamna mtu mwingine ofisini.
ReplyDeletePia kukaa muda mrefu hivo kazini inaonesha ni jinsi gani hayuko karibu na familia yake, ina mana hana muda kabisa wa kuspendi na watoto wake na mkewe!
REVOKE= NI kutangua jambo kabla ya muda wake kuisha, au kubadili jambo lilikuwepo awali kwa kuweka kwa jengine, au kughairisha jambo,au neno lililokuwepo almaaruf kwa masanja ni kumuvuzisha
ReplyDeleteBye mr Billlllll and rest in pc
God help Tanzania with Bukuku,MMMMMM
ReplyDeleteYaani Wabongo hapo tumeshapigwa changa la macho, yaani hiyo imetoka hiyo hakuna kigogo yeyote atakayekamatwa kutokana na wizi huo wewe subiri tu mtakuja kuniambia hapa. Unajua hawa viongozi wetu wanatufanya watanzania wote kuwa ni wapumbavu.
ReplyDeleteNgojeni Kwanza,
ReplyDeleteMbona mi sijayaona yale makampuni niliyoyataja? Au ni issue tofauti??
Na vipi kuhusu majengo ya TWIN TOWERS?
Embu mlioelewa mnifafanulie kidogo maana uzee unaniandama
Wee Anony 5:23, Benno hajafanya kazi chini ya balali, uteuzi wake kwa nafasi ya naibu gavana hauna hata miezi sita, vipi hufuatilii habari?
ReplyDeleteOlaa! Hamkutegemea kabisa haya yanayokuja, na bado pigeni kelelee wee tunataka ushahidi sio domo kaya!
ReplyDeleteNisahihishe kama nitakuwa nimekosea! Prof Ndulu alikuwa ni Naibu Gavana wa Benki kuu kwa kipindi kipi? Ubadhilifu wa pesa unaoonekana sasa si umetokea chini ya uongozi wake na Dk Balali! Au naibu gavana hana say katika maamuzi ya benki kuu! Kuna utata hapa! kama amemwajibisha Balali, kwanini kampandisha naibu wake kuwa Gavana mkuu wakati hali woote walikuwa woote hapo wakati ufisadi huu unatokea?
ReplyDeleteLakini google yangu inaniambia Ndulu amekuwepo hapo benki kipindi kirefu! haya kama ameteuliwa ametokea wapi? huu si mchanga wa macho?
We anony Jan 9, 2008 5:27:00 PM EAT, pale Benki Kuu kuna Gavana mmoja na manaibu gavana watatu ambao ni Prof. Benno Ndulu (Governor), Dr. Enos Bukuku (Deputy Governor - Economic & Financial Policies), Mr. Lila Mkila (Deputy Governor - Financial System & Deepening) na Mr. Juma Reli (Deputy Governor - Administration & Internal Control). Sasa issue ya udini inatokea wapi wakati wawili wa mwanzo ni wakristu na wawili wa mwisho ni waislam? Acheni hadithi zisizo na msingi na ambazo zaweza kuleta machafuko nchini, kama ilivyo issue ya ukabila kwa watani zetu wa jadi!
ReplyDeleteMICHU kama wewe bingwa fanya uipate ripoti hiyo na kuipost kwenye web hii ili tuijadili
ReplyDeleteKwa kweli wafanyakazi wa BOT mmekwisha! Bukuku! Huyo jamaa ni noma kwa kweli! Likizo yenu ya miaka mingi imeisha na mtailipia kwa kweli! Poleni sana na hongera Tanzania
ReplyDeleteNAOMBA BABU SEYA AFUNGULIWE ... HAKUFANYA MAKOSA WALIOFANYA MAKOSA NI HAWA NA WAFUNGWE MILELE
ReplyDeleteTujadili issue ndugu, na si kutumbukiza maneno yoyote. kama kuna mjinga mmoja (annon number 1 hapo juu) anasema eti alijua siku nyingi Bilali siyo Gavana, Nani kamwambia?! Tujadili issue kwa mapana. Ni issue kubwa sana na kwa kweli lazima tumuheshimu Rais wetu kwa hili. Maana wengi wataingizwa kundini. Nyie subirini.
ReplyDeleteNasisitiza sana tujadili issues hapa kwenye blog, na kuropoka hovyo hovyo! Wewe ulijua Bilali siyo Gavana na sisi tusijue!
Wewe unayesema Benno Ndulu alikuwa Benki kuu siku nyingi unamjua au unamsikia huyu mtu? Hebu tafuta wasifu wake vizuri kabla huropokwa maneno. Angalia tangu alivyofanya kazi hukoo mpaka akapitia World Bank Dar office na kwingineko!
ReplyDeleteJamani eeh Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Mie nampongeza JK angalau amechukua maamuzi ya maana wenye kubeza wabeze maana hao hata angefanyaje kazi ni kubeza kazi za wenzao. Niambine ni kipindi gani watu wamechukuliwa hatua kwa ubadhirifu wa mali ya umma zaidi ya kuhamishwa kutoka ofisi moja kwenda nyingine??? Lol haters wacheni hizo! Utafikiri mngepewa hiyo kazi mngeweza.
Hongera mheshimiwa angalau sasa tutaanza kuona mabadiliko ya kweli na wezi wengine huko waliko wajiandae wakae mkao wa kuondoka mapema, pamoja na wazembe wengine kabla hawajashukiwa na rungu la dola.
Kwa kweli ukisikia watu wasio na uchungu wa nchi yao ni kama hao watanzania, ambao wanadiriki kuiba pesa kiasi hicho bila huruma wala aibu. Naomba Kumpongeza raisi wetu jamani anahitaji pongezi, maana haya ni maamuzi mazito.Angaweza kukalia ripot, au kumpa bilali wadhifa mwingine. Kwa kweli akiendelea hivi anaweza kabisa kuwakomboa watanzania katika unyonge na utumwa wa kiuchumi. Watanzania wenzangu hasa wale ambao wanashika nyadhifa kubwa na nyeti tuwe na uchungu na nchi yetu jamani, yaani mtu unakula bila hata huruma, na hata hofu ya Mungu hakuna. Hii ni aibu saana
ReplyDeleteasante.
TANZANIAITAJENGWA NA WATU WENYE MOYO SAFI.
Professa Ndulu alikuwa akifanya kazi world Bank kabla ya kuja BOT.
ReplyDeleteAmebobea katika Economy..
weweanoni hapo juu kidogo mbn unaleta mambo yako ya udini hapa? wee vp! mbona baraza la mawaziri asilimia kubwa ni waislam watu hawajazungumzia chochote kuhusu hilo! na yote ni kwamba sisi watanzania hatuna udini wala unini, lakini wewe ndo unaanza.. nataka nijue elimu yako ndo labda nitajua tatizo liko wapi! weee anoni mwingine hapo juu nadhan ushjibiwa kuwa ndulu kaingia b.o.t wakati hawa jamaa washaharibu, hata hivyo hana hata miezi saba.
ReplyDeleteTime is a silent killer. Baada ya miezi 6 tutakuwa tumesahau kuhusu Benki Kuu maana tutakuwa tunapamabana na sooo nyingine.Baada ya miaka 2 utasikia aliekuwa Gavana sasa Balozi wetu Brunei. Au wadau mmeshasahau?Kama mtu anaweza kuuwa kwa kutumia silaha na kuepuka kifungo cha maisha au muda mrefu itakuwa wizi au ubadhilifu?
ReplyDelete1.Kama ni kweli asemavyo mdau mmoja; basi sasa prof. Ndulu badilika yaani WORK SMART AND NOT HARD maana kulala ofisini sio dawa ya BOT utawachanganya walinzi usiku na utagombana na mkeo na matokeo yake ni ama mtu mwingine kujiwahi huko huko ofisini au wewe mwenyewe kuhamishia hasira za nyumbani BOT. Na kama una watoto nao watakulaani maana laana hutoka kwa Mungu kupitia kwa vikongwe na hata watoto.
ReplyDelete2. Sijui ni mimi tu nimechanganya masomo hapa; Rais asante lakini lazima tujue sasa je kiutumishi Balali amestaafishwa, ameachishwa au fukuzwa kazi au amehamishwa. Maana kutangua (revoke) uteuzi wake wa Ugavana ni jambo moja na tamko juu ya hatima ya ajira yake serikalini ni jambo jingine maana lina implications katika maslahi yake ya mwisho (terminal benefit) na maisha yake ya baadaye kwa ujumla! Naomba msaada kuelewa hapa.
Mkata Issue.