piga ua na si yanga si simba lakini hakuna kiongozi katika vilabu hivyo vya bongo aliyekuwa imara kama alivyokuwa jimmy david ngonya enzi alipokuwa katibu mkuu simba. pichani akiongea siku aliyochaguliwa kushuka nafasi hiyo na kulia kwake ni mwenyekiti wa simba mzee joachim kimwaga, mhazini rughani na katubu mwenezi juma ngondae. juu akihutubia wanachama klabuni mtaa wa msimbazi striti. hapo hakuna aliyeleta fyoooo...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Ngonya alikuwa mwanaume wa shoka lakini kwa hali ilivyokuwa wakati huo na kwa kuangalia historia ya Simba asingeweza kufua dafu.historically Simba ni timu ya watu wa rangi...........

    ReplyDelete
  2. Nauliza tu jamani..., Eti hakuna spell check ukiandika Kiswahili? Ni swali tu wajame......

    ReplyDelete
  3. Mpeli upo wapi siku hizi? Huyu jamaa alikuwa anakaa kitega uchumi enzi hizo

    ReplyDelete
  4. ngonya amefungiwa maisha kuwa kiongozi wa soka. Alifanya nini?

    ReplyDelete
  5. Simba kulikuwa na Ngonya huku Yanga kuna mtu mwingine alikuwa anaitwa BANDAWE sijui hawa jamaa wapo wapi. Wote wamfungiwa maisha kujihusisha na maswala ya soka bongo au FIFA? mwenye kumbu kumbu atujulishe

    ReplyDelete
  6. watu kama hawa walikuwa hawana vision yeyote katika soka na walisaidia sana kuua soka TZ na bora walifungiwa na walikuwa wababe tuu wasio akili yeyote ya soka zaidi ya kupika migogoro,na hii sampuli bado ndio viongozi wengi wa Afrika serikali na tunahitaji kusafisha akili kama hizi ili twende mbele

    ReplyDelete
  7. rafiki yangu Juma Ngondae alikuwa ni mtangazaji mahiri wa taarifa za habari kutoka radio Tanzania Dar-es-Salaam enzi hizo,sijui wangapi pia mnamkumbuka Abdul Masudi sasa marehemu

    ReplyDelete
  8. Taarifa za Jamaa kama hawa ilifaa tuzikute kwa kina Tenga (TFF).

    sasa kama hawana wanafanya nini pale??

    Si wale kona tu!!

    ReplyDelete
  9. Marehemu Juma Ngondae(RIP)nimeishi nae pale M/nyamala Komakoma huyu ni Simba damu damu.

    ReplyDelete
  10. mpeli ngonya yupo dar mzururaji alifikiri hela za baba zipo milele sasa ameona!!!!!alikuwa na dada wabaya kichwani hamna kitu ukoo mzima ubishoo tuu na wangekuwa warefu tungekoma

    ReplyDelete
  11. we anony hapo juu hujui mpeli kaolewa ilala hayupo tena kitega uchumi walifukuzwa.....

    ReplyDelete
  12. the tragedy ilikuwa wachezaji wa simba enzi hiyo walikuwa hawamtaki ngonya, huyo jamaa aliyekaa kulia kwake ni kimwaga, mkubwa wa magereza enzi hizo, kama m.t. mangara alikuwa mwenyekiti wa simba unadhani hawa jamaa wakiiba serikali ilikuwa kama vile inawaogopa. kimwaga na mangara walikuwa majambazi wakubwa, enzi ya miaka ya 60-70 mpira ulikuwa una pesa sana lakini wachezaji hawakufaidika cho chote, walikuwa wanacheza mpira halafu asubuhi wanaenda kazini, sasa mpira utaendeleaji hivyo? sunday,kassim manga,maulidi dilunga, wote leo masikini. aibu kabisa!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...