promota na mfanyabiashara mashuhuri alex kajumulo akipiga stori na waandishi farouk karim (kati) wa itv na redio one na ibrahim maestro wa clouds fm leo uwanja wa amani. kajumulo kesho anatoa vifaa kwa timu ya taifa ya visiwani na vilabu vya daraja la kwanza. pia anasema ana programu ya elimu ya utawala anayotaka kusaidia kutoa kwa viongozi wa vilabu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Kama kweli atatekeleza safi sana. Lakini nina shaka sana na huyu bwana kwani alishawahi kuonyesha makeke sana miaka ya nyuma huko na kisha kutokomea ilhali akiacha mipango yake mingi bila ya kukamilika. Na sioni kama kuna tofauti yeyote kati yake na Jaki Pemba ambaye walitofautiana na TFF. Watu sampuli hizi hupenda sana kusifiwa na watu.

    ReplyDelete
  2. lakini huyu kidogo afadhali sio kama jack pemba alinunua timu ya sigara wachezaji walikuwa wanalipwa mishara alisaidia timu zote silizo shiliki ligi kuu na hakuwa na kashifa yoyote kwa kinadada sio kama huyo pemba

    ReplyDelete
  3. Naona uwanja wa Amani ulifurika sana siku hiyo...! Hapana shaka shaka kiingilio kilikuwa ni miguu...

    ReplyDelete
  4. Huyu BabuKaju huwezi mfananisha ma Jack Pemba.

    Huyo bwana yupo makini na ana nia sana ya kuendeleza soka la nyumbani tatizo anakwamishwa na sisi wenyewe.

    Alinunua Club ya sigara,kawapa kila huduma muhimu.Matokeo yake uongozi wa timu ukaanza kuvurunda.Unakumbuka wakina Julio ndio walikuwa makocha na kila siku wanajirusha kwenye kumbe za starehe mpaka majongoo sasa hapo utategemea nini.

    Kaza buti Kajumuro,saidia ndugu zako.najua wewe dio hao wanaotaka kusifiwa sifiwa kwenye nyimbo tuu za Fm academia utafikiri wao ni chorous....

    ReplyDelete
  5. Mwenzenu mie mgeni, mambo ya mjini siyajui kwa sana .
    ...haya ,... huyu kajumulo alinunua sigara kwa sh. ngapi? .. na alipoiacha alimuuzia nani, au alitoa bure kwa wanaoimiliki sasa ??????

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...