Mimi ni mtanzania, nimeishi Sweden kwa miaka 10, lakini kwa sasa hivi nipo hapa nchini, ila kuna taarifa za Mtanzania mmoja anayeishi Marekani; Kijana machachari ambaye taarifa zake hatuzipati lakini anaiweka nchi ya Tanzania katika ramani ya dunia.

Amefanya mambo mengi sana hapa nchini, kama vile kutoa misaada ya aina mbalimbali, na hivi Karibuni gazeti la majira la tarehe 02/12/2007 ilitoa makala maalum kumhusu. Na pia alipokuwepo hapa nchini, mwezi wa October, alishirikiana na dada mmoja (Khadija Mwanamboka) kuwasaidia watoto mayatima katika vituo mbalimbali hapa jijiji Dar.

Huyu kijana kwa habari tunazozipata toka ughaibuni, ni kwamba anapata umaarufu mkubwa sana kutokana na kazi zake za kimaendeleo katika jamii. Habagui, anasaidia watu wa kila rangi wanaoishi katika hali duni katika Jimbo la South Carolina Vyuo kadhaa, mashirika yasiyo ya kiserikali yamekuwa yakimwalika kutoa "speeches".

Hivi karibuni alialikwa kuongea na wasomi katika chuo kikuu cha Wake Forest. akiwa na umri wa miaka 29, anavuma sana, na wengi wanafananisha matendo yake au itikadi zake na zile za muasisi wa India Mahatma Ghandhi Cha kushangaza ni kwamba, Jarida la Business Week ilimnukuu kama hivyo unavoona hapo chini.


Mdau Jumanne Kavishe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Michuzi,
    Mwambie huyu jamaa hii link haina information yoyote juu ya huyo dada anaemwita Gandhi wa Bongo.

    ReplyDelete
  2. Hii ni habari njema.

    Michuzi mwambie huyo aliyekupa taarifa hizi akupatie tu jina kamili la huyo Mbongo tutatafuta data zake kupitia Google.

    Wasalaam

    ReplyDelete
  3. Ok guys I got the link. The news item has been syndicated and can also be seen here:

    http://www.charlotte.com/someck/story/413368.html

    ReplyDelete
  4. Michuzi, mwambie huyo jamaa kuwa sisi tunaishi huku ughaibuni lakini hatujawahi sikia mtanzania yoyote mwenye sifa kama hizo, mimi naona kuwa jamaa ameingizwa mitini.

    ReplyDelete
  5. Watu wengine wakitoa huwa hawajitangazi,kwahiyo hii sio ajabu,labda hataki umbea,msimjazie.

    ReplyDelete
  6. anonymous wa wed 1/2/ at 5:43 pm., Ni kweli kabisa huyu mhindi alikuwa very racy, lakini basi propaganda za dunia hii wanamfanya humanitarian of some sort, almost god like figure

    ReplyDelete
  7. I can recall reading about his guy and seeing him on a TV in Dar.Actually I was impressed by his work and tenacity to help the country.

    Not too many people are willing to go for 5 days without food for the needy. I cant recall the name, but I am not suprised to see him in the spotlight, i guess it is about time.

    ReplyDelete
  8. Hii link mpya aliyoituma Kavishe pia haina habari yoyote. Mie naona Bw. Kavishe tuandikie tu jina la huyo dada.Kwani hizo story unazozisoma si zinataja jina? Basi tuandikie tu jina la huyu Ghandi wa bongo.

    Halas

    ReplyDelete
  9. Huyu ni mwanaharakati mkubwa sana. Alishiriki katika dondoo ya kisiasa pamoja na Prof Issa Shivji, Mabere Marando naye Jonhie Mashaka......Ongera sana Bwana Mdogo, Babu kubwa Nakubaliana nanyi

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...